Hoja zinazotutumbukiza kwenye udini zipewe "zero tolerance" jf!!

MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
1,826
2,000
Kumekuwa na hali ymbaya sana ya kupoteza muda na maana ya hoja nyingi hapa JF haswa kwa kuwa inaonekana kabisa kuwa wapo watu ama waliopandikizwa humu kuhakikisha ule mtiririko wa mawazo hapa JF unafifia, haswa maswala ya kisiasa. Mpaka sasa kwa kweli inaonekana wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya wana JF wakiona tu mtu kaandika hoja nzuri mara moja hutumia nafasi hiyo kuichafua kwa kutumbukiza udini makusudi kabisa na wazi wazi, bila hata kuona haya.

Hii ni mbinu ambayo nadhani hatujaigundua na inazidi kuidhoofisha JF.

Kwa ajili hiyo nashauri kuchukuliwa hatua za mara moja kufuta mara moja hoja yoyote yenye udini kwa kutambua kuwa Taifa letu halikuundwa kwa misingi ya udini wala ukabila wala ubaguzi. Nina hakika pia kuwa hata JF haikuundwa kwa ajili ya dini moja au nyingine. Ndiyo maana hata wanaoifahamu Tanzania watashindwa kuelewa ni nini kinaendelea hapa JF. Jambo hili linanikera sana maana hoja nzuri inatiwa sumu mbaya ya udini mpaka watu wanaachana nayo wanakimbilia kwenye mambo yasiyosaidia sana Taifa letu.

Ninaomba jambo hili liangaliwe kwa makini sana na kama itawezekana hata lile jukwaa la dini lifutwe kabisa maana ndipo kule mijadala yenye hisia mbovu hufurika na kuenezwa kwenye majukwaa mengine.
Naomba kuwasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom