Hoja za Kingunge zilishajibiwa na mzee Mwinyi

Hoja za Kingunge zilishajibiwa na mzee Mwinyi

Mariswaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2015
Posts
201
Reaction score
2
Mzee Kingunge alisema "Kupanda mlima kunahitaji pumzi, CCM wameishiwa pumzi. Inatakiwa watu wapya wenye pumzi mpya waje kuleta maendeleo" Sasa Ni nani mpya ndani ya Ukawa mwenye pumzi mpya za kupanda mlima?

Edward Lowassa amehama CCM 2015, Fredrick Sumaye amehama CCM 2015, Laurance Masha amehama CCM 2015, Esther Bulaya amehama CCM 2015, James Lembeli amehama CCM 2015, na hata Mgeja nae amehama CCM 2015. Sasa watu hawa ndiyo wapya?

Watu hawa ndiyo wana pumzi mpya? Ndiyo maana Mzee Mwinyi alisema "Kama CCM A ipo, CCM B ya kazi gani ikiwa haina viwango?"

Hakuna sababu ya kuhangaika na CCM B, changamoto zilizopo ndani ya CCM A zimeshapata mtatuzi, Dr. John Magufuli ataleta mabadiliko chanya ndani ya chama na serikali bila kuathiri amani, utulivu na uchumi wetu. Haya ndiyo mabadiliko ya kweli, ili tuyapate hatuna budi kumchagua Dk. John Pombe Magufuli..
 
Unachanganya vitu viwili hapa changamoto ndani ya chama chenu na mustakabali wa Nchi. Kama Magufuli ndiyo mtatuzi wa changamoto ndani ya chama chenu awe Mwenyekiti sijui msemaji or whatever atakachokuwa ila si kwa Taifa.
 
Nadhani Mwinyi hajui kuwa kuna mchezaji anaweza asifanye vizuri timu a-kufunga magoli coz hakuna mtu wa kumlisha mipira murua ya mwisho, kwa sababu ya mfumo, mchezaji huyohuyo akafanya vizuri timu b.... Kwa sababu ya kuwa na viungo wachezeshaji wengi, kuna mtu aliwahi onja busara ya mama Regina Lowassa katika majukwaa hapo zamani??

Leo huyu mama anaoneka ni mtu makini. Dr. Slaa alionekana ni mtu makini sana alipokuwa timu ya watu makini, leo anaogopa hata kuonana na watu ni aibu imemjaa... Zitto alikuwa mtu mashuhuri sana alipokuwa CHADEMA, leo anapooneka kutumika na CCM vipi umashuhuri wake, bado ni wakiwango kile kile??
 
Mzee Kingunge haiwezekani kamwe nchi kuongozwa kutokana na Mahaba kwa Lowassa, yaani umejidhalilisha na hata ongea yako ilikuwa inakusuta.sisi CCM tunasema RAISI WA TANZANIA AWAMU YA TANO NI JOHN MAGUFULI
 
Babu kawashika pabaya, CCM kubali yaishe, sisi kilio chetu ni Katiba Mpya, kwenu iko hiyo? Kama Magufuli haongei lolote kuhusu Katiba Mpya, anatatwanga maji kwenye kinu, na hayo ndio mabadiliko MAMA.
 
Mzee Kingunge haiwezekani kamwe nchi kuongozwa kutokana na Mahaba kwa Lowassa, yaani umejidhalilisha na hata ongea yako ilikuwa inakusuta.sisi CCM tunasema RAISI WA TANZANIA AWAMU YA TANO NI JOHN MAGUFULI
hahah
kingunge aliongelea ukiukwaji wa taratibu......ambazo wenzake ndani ya ccm wanadai hazijakiukwa
 
HOJA ZA KINGUNGE ZILISHAJIBIWA NA MZEE MWINYI
Mzee Kingunge alisema “Kupanda mlima kunahitaji pumzi, CCM wameishiwa pumzi. Inatakiwa watu wapya wenye pumzi mpya waje kuleta maendeleo” Sasa Ni nani mpya ndani ya Ukawa mwenye pumzi mpya za kupanda mlima? Edward Lowassa amehama CCM 2015, Fredrick Sumaye amehama CCM 2015, Laurance Masha amehama CCM 2015, Esther Bulaya amehama CCM 2015, James Lembeli amehama CCM 2015, na hata Mgeja nae amehama CCM 2015. Sasa watu hawa ndiyo wapya? Watu hawa ndiyo wana pumzi mpya? Ndiyo maana Mzee Mwinyi alisema “Kama CCM A ipo, CCM B ya kazi gani ikiwa haina viwango?”
Hakuna sababu ya kuhangaika na CCM B, changamoto zilizopo ndani ya CCM A zimeshapata mtatuzi, Dr. John Magufuli ataleta mabadiliko chanya ndani ya chama na serikali bila kuathiri amani, utulivu na uchumi wetu. Haya ndiyo mabadiliko ya kweli, ili tuyapate hatuna budi kumchagua Dk. John Pombe Magufuli
Inaonekana huna kasumba ya kuwasikiliza wazee wanapozungumza na ndio maana laana haziwaachi!
 
hahah
kingunge aliongelea ukiukwaji wa taratibu......ambazo wenzake ndani ya ccm wanadai hazijakiukwa

Sasa kama wanasema hazijakiukwa yeye analazimisha je zimekiukwa? Kingunge mwenyewe ndie mmoja wa chanzo cha LOWASSA KUKATWA CCM maana alikwenda kwenye Mkutano wa hadhara wa SAFARI YA MATUMAINI kwa maana ya kwamba walianza kampeni mapema na kinyume cha utaratibu
 
Kingunge kasema watu wasipoongea basi hamna mabadiliko. Kasema lazma uwepo uhuru wa kuongelea mambo huwezi kutatua tatizo kama tatizo halizungumzwi.

Kaongeza lazma watu wakubali kusikiliza mawazo mapya pindi wanapokuwa wamekwama...au kuishiwa pumzi. Lowassa, Esta, Lembeli wamekubali kusikiliza mawazo mapya
..
 
Sasa kama wanasema hazijakiukwa yeye analazimisha je zimekiukwa? Kingunge mwenyewe ndie mmoja wa chanzo cha LOWASSA KUKATWA CCM maana alikwenda kwenye Mkutano wa hadhara wa SAFARI YA MATUMAINI kwa maana ya kwamba walianza kampeni mapema na kinyume cha utaratibu
anachozungumza kingunge ndicho alichokizungumza DAVID MWAKYUSU WA MBEYA na ndio ukweli ulio wazi kwamba JK alikiuka katiba ya ccm ili kumbeba MEMBE ingawa mwishowe hata JK alikosa alichokipanga

...be honest katiba ya ccm inasema baraza la maadili linahaki ya kukata majina ya wagombea au just kuwasikiliza na kutoa mizania ya alichojitetea mgombea?
hiki ndio kilio cha kingunge kwamba katiba inakiukwa na viongozi wa chama wanafumba macho na kusema hamna kilichokiukwa
 
Hii safari kila mmoja ataongea lake Je ni mara ya kwanza Lowassa haya kumtokea? Hii nchi haiko vile mnavyofikiri hata Kikwete alikuwa hambebi Membe. MAGUFULI ndio aliandaliwa mapema sana na hata alipochukua FOMU na kwenda kwa namna alivyoenda katika kutafuta Wadhamini ni maelekezo Lakini MAGUFULI NDIE aliekuwa chaguo na ndie Raisi awamu ya Tano
 
Babu kawashika pabaya, CCM kubali yaishe, sisi kilio chetu ni Katiba Mpya, kwenu iko hiyo? Kama Magufuli haongei lolote kuhusu Katiba Mpya, anatatwanga maji kwenye kinu, na hayo ndio mabadiliko MAMA.

Swala la katiba mpya ni mojawapo ya mambo ambayo yalimfanya Kikwete amwondoe Kinginge ikulu kuwa mshauri wake wa mambo ya siasa. Na hata baada ya kuondolewa ikulu aliwaita waandishi wa habari pale victoria na kueleza jinsi ambavyo hakuridhika namna Kiwete alivyolichukulia suala la katiba mpya na kusema haikuwa ajenda ya ccm na kwamba Kikwete amepora ajenda ya wapinzani.

Hata haya mabadliko anayoyasema yapo hata ccm ndio maana hata kingunge amesema Mkapa alikuwa jembe kwasababu wakati wa Mkapa chama kilikuwa na nguvu na nguvu upinzani ulikuwa unapungua siku baada ya siku(rejea matoke ya uchaguzi ya urais ya mwaka 1995 na ya mwaka 2000)
 
Maneno yako yamekaa ki propaganda sana, unataka tuamini kwamba chama siyo taasisi inayo simamia sera inazo amini ziki tekelezwa zina weza kuleta maendeleo kwa watu, ila ni mtu, kama hao ulio wa Taja.

Watu sasa wameamka ,kila kitu wanajuwa, propaganda kama hizi hazita saidia kitu.

Hoja alizotoa Kingunge zina mashiko wala huwezi kulinganisha na polojo za mzee Mwinyi.

Tulieni tu chama kiwafie na matusi yenu na mengine yote yanayo fanana na hayo kama unafiki, dharau , ufisadi ,kulindana , uzushi na uongo.
 
Kwa ninavyoelewa mimi si mtu kama mtu labda awe baunsa sana hapana. Hapa naona kama vile akimaanisha sera mpya zenye maono mapya kutoka katika chama kipya nje ya ccm ili kuingiza changamoto mpya maana ccm imedumaa. Ccm huenda kuna watu wenye misuli tu lakini ata ukiwa baunsa vipi ukishapanda kwenye chombo cha kusafiria kibovu ajari haziepukiki na ikitokea ajari huwezi sema kwa kuwa una misuli basi utakingana na kifo mmh hapo inabaki Mungu nisaidie na majuto kibao. Hapa tuzungumzie sera na chombo chenyewe cha kubebea hizo sera kimetoboka mpaka mwisho wa safari unajikuta umebaki na sera moja kati ya 20 ukiulizwa imekuaje unashindwa kujibu na kuanza na wewe mwenyewe unashangaa usijue kilichotokea
 
Mpaka muda huu anaeamini ukawa watashinda ni wakupimwa akili
 
Mpaka muda huu anaeamini ukawa watashinda ni wakupimwa akili

Na wewe unaelewa kinacho zungumzwa hapa au umekutupuka tu? Kwa mleta mada nikuombe huwe unasoma sana ili uweze kufahamu tofauti ya mtu kama Kingunge na watu wa kuja kama Ally Hassan Mwinyi ktk chama cha CCM!
 
Na wewe unaelewa kinacho zungumzwa hapa au umekutupuka tu? Kwa mleta mada nikuombe huwe unasoma sana ili uweze kufahamu tofauti ya mtu kama Kingunge na watu wa kuja kama Ally Hassan Mwinyi ktk chama cha CCM!
Mkuu huyo asikumize kichwa ona id yake kwanza.. Mavipunda, hiyo inadhirihisha akili yake imechafuka.
 
Last edited by a moderator:
Ni lazima ujiulize kwann hao watu waliondoka ccm na kujiunga chadema...sio unasema tu hawana nguvu hawana pumzi, fanya chunguzi kwanza ndipo uje useme kitu hapa....hatuhitaji siasa za maji taka
 
Babu kawashika pabaya, CCM kubali yaishe, sisi kilio chetu ni Katiba Mpya, kwenu iko hiyo? Kama Magufuli haongei lolote kuhusu Katiba Mpya, anatatwanga maji kwenye kinu, na hayo ndio mabadiliko MAMA.

Mbona katiba Mpya watu walishamaliza bado kura ya maoni, mkipasuka tarehe 25 mnapelekwa katika kura ya maoni wakati huo mtakuwa mshaanza kugawana fito na mzee wa watu mumeshatia hasara kwa tamaa zake za uraisi hamu hatokuwa nayo hata ya kuwa mbunge viti maalum.
 
Back
Top Bottom