Hoja za Dr. Slaa Siyo Rocket Science!

Hoja za Dr. Slaa Siyo Rocket Science!

Mleta mada umeangalia upande mmoja tu. Kitu ambacho hujagundua ni kuwa ni lazima mwanasiasa azungumze lugha inayoeleweka kwa watu anaowatetea. Hivi anayozungumzia Dr Slaa ndio kero halisi za wananchi na kwa kusema hivyo anazungumza lugha inayowaelea.

Kuzungumza data, takwimu za uchumi na mambo yanayofanana na hayo si majukwaani, ni kwenye makongamano, warsha, na kn
 
Nilijua lazima kuna kitu kitatokea kabla ya uchaguzi kuhakikisha vyama vya upinzani vyote vinasambaratika ovyo na naona imetokea kweli, CDM walivuma sana mwaka jana na upepo wote ulikua umehamia kwao, CCM walikua wanaonekana ovyo sana ila mambo yalivobadilika, sasa Magufuli anawaka si mchezo, CDM haina mwelekeo, ACT nacho kimekuja kuvuruga watu wa upinzani wanahama ovyo, in short ni kwamba Magufuli mwaka huu anabeba urais kwa kura zaidi ya 80%, viti vya CDM navyo vitapungua kwa kasi sana bunge lijalo. Unless wawe na a card to play kuturn everything around huu muda uliobaki which is next to impossible.

Naona bado unaota so better Rudi kulala
 
Tangu nimeanza kufuatilia Upinzani Tanzania hasa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kupitia nyota wao Bw.Slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na CCM zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi WatanZania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (Watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila Mtz analijua hili?
Hata mtoto wa Shule ya msingi anajua kwamba kuna Watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (CHADEMA) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza Shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara Hospitali hakuna Dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua Sayari mpya na sasa anatuarifu...

Ni kweli wao ni kutaja kasoro za watu lakini sijasikia ahadi yeyote ya kuondoa kero za watanzania kama ni jinsi gani elimu itaboreshwa, kuondoa kero ya foleni ambayo inaligharimu taifa hili kuliko kawaida. Nataka kusikia kuimarishwa miundombinu hasa reli na bandari. Uchumi wa nchi, Maisha na kipato cha mtanzania wa kawaida kitaboreshwa vip kwa kutumia rasilimali zetu za ndani( kwani wenzetu Rwanda na Kenya wameweza). Ndio ninataka kusikia sio huyu kazaa na fulani, huyu kaiba je tuna uhakika gani wewe hutaiba? Tunataka mtuambie kwa kweli nchi hii iko hoi sana

Hivi mnajua maana ya chama cha upinzani?
Guys duu mbona weupe hvyo?
mahaba na chama au ndo hamna kitu kichwani?
So shame
 
hoja kubwa aliyonayo na ambayo ni ya msingi sana ni kutokomeza ccm .
 
mkuu sio yeye aliyesema elimu bure,kupunguza vifaa vya ujenz?....atakula mihogo ikulu,kuanza mchakato wa katiba ndani ya siku mia moja akichaguliwa,mishhara ama ushasahau?
 
Dk.slaa kaahasi kanisa kaenda kumtumikia kaisari asahau uraisi ww ulikua unambipu,,,ulikiri kwa ulimi kua utakua mwaminifu kwake kumtumikia katika upadrii leo umeutupa aisee,,,
 
tangu nimeanza kufuatilia upinzani tanzania hasa chama kikuu cha upinzani chadema kupitia nyota wao bw.slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na ccm zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi watanzania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila mtz analijua hili?
Hata mtoto wa shule ya msingi anajua kwamba kuna watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (chadema) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara hospitali hakuna dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua sayari mpya na sasa anatuarifu...

kwa hyo ultaka atoe mbinu kwa adui? Acha ujnga ww...
 
Naona bado unaota so better Rudi kulala

Mkuu utaongea sana ila in the end ull realize nothing changes mwaka huu...
Ningependa kuona upinzani wanashinda though sio likely kabisa.. Sasa wewe endelea kubisha huku huna kitu chochote ku-back you up nakushangaa sana.
 
Sasa hapo kosa langu liko wapi mimi kusoma Shule unazoziita za Kata, si ndiyo shule ambazo nchi yangu imezijenga na ndio Elimu ambayo nchi yangu inatoa? Ulitaka nisome wapi ndio nifit kwenye hiyo standard yako?

Ok usikonde mshirika; ndio maana tunataka mabadiliko ya msingi (fundamental changes) kabisa ili tuanze safari ya kuondokana na hayo mapungufu tuliyolishwa na chama kichovu CCM, Elimu bora na sio bora elimu!!! huduma za afya bora sio utitiri wa hospitali na zahanati zisizokuwa na waganga, manesi na dawa!! huduma ya maji salama sio mabomba yanayotoa kutu badala ya maji!! kurudisha misingi ya uadilifu katika utumishi wa umma na sio watumishi wanaotafuta na kutengeneza mianya ya wizi na ufisadi wakati wote!! Umma wa watanzania unaosifia mtu anayetajirika kupitia jasho lake halali badala ya kuwasifia wezi na mafisadi waliojitajirisha kwa kufisidi mali ya umma! jiunge na Gari kubwa la VUGUVUGU LA MABADILIKO YA MSINGI; UKAWA FOR FUNDAMENTAL CHANGE!
 
Umeongea ujinga, tafuta ilani ya CDM ya mwaka 2010, chukua na ya CCM 2010 zisome, halafu zifananishe ndio utajua tifauti yake. Maana umechukua CCM kama taasisi, ukaifananisha na Dr Slaa. Umechemsha ndugu yetu.
 
umetoa hoja nzuri, mbaya zaidi UKAWA wanajinadi lengo lake kuing'oa ccm, kumbe watakavyotimiza hilo wanwza wasiwe na cha kufanya kwa kuwa wanamkakati mmoja tu kuionoa ccm madarakani.
 
Hiyo ilani siyo wote wamesoma, tulitegemea ktk mikutano watueleze watanzania mikakati iliyopo katika ilani hiyo.
 
dr slaa anaongea vitu wanavyo kutana navyo watanzania kila siku mfano leo tunaambiwa uchumi wetu umekua ni kweli bt umekuwa ktk secta ambayo wengi hawanufaiki nayo the measure of intelligence is the ability to change na change huwa inaanzia kwa wengi na ndio Dr slaa anawalenga
 
mkuu sio yeye aliyesema elimu bure,kupunguza vifaa vya ujenz?....atakula mihogo ikulu,kuanza mchakato wa katiba ndani ya siku mia moja akichaguliwa,mishhara ama ushasahau?

Amesha sahau, hana kumbu kumbu kbsaaa. sasa kwanini asiwe mateka wa kijani?
 
Zitaje nchi hizo. Anza na Kenya . rudi tulipotoka kisha jiulize tulipaswa kuwa hapa?. Naomba nikukumbushe " kulijua tatizo ni hatua ya kwanza kulitatua".

Zambia wakati WA Chiluba na Malawi walijuta kwa nini walimtoa Banda
 
Hiyo ilani siyo wote wamesoma, tulitegemea ktk mikutano watueleze watanzania mikakati iliyopo katika ilani hiyo.

Ni kweli ni vema kwa sisi tusiokuwa na muda tukaambiwa through majukwaa. Hiyo ya Ccm yentewe siijui lakini ninaona Ni bora zimwi nilijualo kuliko hawa ambao siwajui. Na ukizingatia kwa sasa wahuni WA mtaani wameshasoma upepo kwamba Chadema ndio iko vizuri eti ndio makada na viongozi. Yaani sijui tunaenda wapi. Yawezekana katika ngazi ya Taifa wamejipanga ILA huko ngazi za chini bado hawaaminiki.
 
Tangu nimeanza kufuatilia Upinzani Tanzania hasa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kupitia nyota wao Bw.Slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na CCM zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi WatanZania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (Watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila Mtz analijua hili?
Hata mtoto wa Shule ya msingi anajua kwamba kuna Watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (CHADEMA) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza Shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara Hospitali hakuna Dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua Sayari mpya na sasa anatuarifu...

Uache kukurupuka mkuu, hizo siasa unafuatilia ukiwa gerezani?
 
1. Waliotoa hoja ya kuwa katiba ya sasa ni mbovu na inatakiwa ibadilishwe ni akina nani?
2. Waliosema elimu Shule ya Msingi na Secondary itakuwa Bure ni akina nani?
3. Waliosema ili kila mtanzania awe na nyumba bora watasababisha kupungua kwa bei ya vifaa vya ujenzi ikiwemo Cement kwa mfuko kuuzwa kwa Tsh 5000 kwa kuwaondolea au kupunguza kodi kwa bidhaa hizo ni akina nani?
4. Waliosema watahakikisha Rasilimali zote zilizotaifishwa na CCM ambazo zilijengwa na wananchi wote kabla ya mfumo wa vyama vingi vikiwemo viwanja vingi ya michezo ni akina nani?
5. Waliosema tutajenga Chuo kikuu Dodoma, pia kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa kitovu cha elimu ni nani. Ma-CCM wakaiba wazo hilo,maana halikuwepo kwenye ilani yao
 
mkuu utaongea sana ila in the end ull realize nothing changes mwaka huu...
Ningependa kuona upinzani wanashinda though sio likely kabisa.. Sasa wewe endelea kubisha huku huna kitu chochote ku-back you up nakushangaa sana.
its either u be part of the changes u want
or u shut the f.u.c.k up!
 
Back
Top Bottom