Hoja za Dr. Slaa Siyo Rocket Science!

Hoja za Dr. Slaa Siyo Rocket Science!

Haki ya nani mwaka huu mmeshikwa pabaya. Haya majizi ya CCM hayana ubavu wa kuzuia nguvu ya umma kuwatoa madarakani. Mwaka huu Urais mtauisikia kupitia kwenye bomba
Hapana mie sio mwanachama wa chama chochote cha siasa ila kama mtanzania nina haki ya kuamua wa kumpa kura. Na kwa taarifa yako huko nyuma nilikuwa mshabiki mkubwa wa upinzani. Uchaguzi wa mwaka 1995 tulishinda kwenye jua siku nzima tukisubiri kumpigia kura Mrema na vifaa vya kupigia kura havikuletwa katika kituo chetu kabisa. Mwaka 1994 ni mmoja wa waliopiga kura kuleta mageuzi ya udiwani pale moshi mjini kwa sababu ccm walimsimamishja mgombea mzee sana. Hivyo ninajua ninachokifanya.
 
Tangu nimeanza kufuatilia Upinzani Tanzania hasa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kupitia nyota wao Bw.Slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na CCM zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi WatanZania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (Watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila Mtz analijua hili?
Hata mtoto wa Shule ya msingi anajua kwamba kuna Watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (CHADEMA) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza Shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara Hospitali hakuna Dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua Sayari mpya na sasa anatuarifu...

Watu wengi ukiwemo na wewe hamtambui kuwa kuna maisha mazuri zaidi ya haya,mmeridhika na maisha mliyo nayo.Ukila nyama wakati jirani yako hana uwezo huo unajiona tajiri bila kutambua kwamba utajiri si kula nyama.
 
Hapa umenipa jibu kwani nataka unishawishi chama chako kitafanya nini kuboresha treni kwani Treni ni muhimu sana kwa nchi yeyote inayohitaji maendeleo, madini na mbuga za wanyama zitainufaisha vip Tanzania. Lakini vinginevyo unamchafua mtu wakati wewe hatuelewi kwamba unaweza kuiharibu nchi hii mara tatu zaidi ya hapa tulipo. Mifano ya nchi za Africa ambazo zilikuja kujutia maamuzi yake tunazijua ila si vizuri kuzitaja.

Zitaje nchi hizo. Anza na Kenya . rudi tulipotoka kisha jiulize tulipaswa kuwa hapa?. Naomba nikukumbushe " kulijua tatizo ni hatua ya kwanza kulitatua".
 
Ni kweli wao ni kutaja kasoro za watu lakini sijasikia ahadi yeyote ya kuondoa kero za watanzania kama ni jinsi gani elimu itaboreshwa, kuondoa kero ya foleni ambayo inaligharimu taifa hili kuliko kawaida. Nataka kusikia kuimarishwa miundombinu hasa reli na bandari. Uchumi wa nchi, Maisha na kipato cha mtanzania wa kawaida kitaboreshwa vip kwa kutumia rasilimali zetu za ndani( kwani wenzetu Rwanda na Kenya wameweza). Ndio ninataka kusikia sio huyu kazaa na fulani, huyu kaiba je tuna uhakika gani wewe hutaiba? Tunataka mtuambie kwa kweli nchi hii iko hoi sana

Hivi watanzania tumekuwa na akili finyu kiasi cha kutojua majibu ya kero zetu mpaka tusubiri tuambiwe? Hivi wewe hujui kipato cha mtanzania kitaboreshwa namna gani? Unajua kitu kinaitwa KAZI? Huku ni kujiaibisha mwenyewe na kutuaibisha watanzania. Bora unyamaze kwani wewe unafikiria unamuumbua Dr Slaa kumbe unaonyesha uzuzu wako. Basi kama hujui, fahamu kuwa maendeleo huletwa na UCHAPA KAZI na NIDHAMU YA MATUMIZI. Na uchapa kazi na nidhamu ya matumizi inakuwepo kunapokuwa na UONGOZI BORA. Dr. yeye yupo kuleta UONGOZI BORA na NIDHAMU KATIKA MATUMIZI ambayo CCM imeshindwa! Kwa mfano hebu changamsha ubongo wako kidogo: Kipi cha muhimu kwa watanzania? 1. Kuongeza shule AU 2. Kuongeza majimbo ya uchaguzi?
 
We kweli mgeni nchi hii!! au ndio mwanakitengo uko kazni kutekeleza kazi za bwana zako!! Umesahau Dr Slaa alisema angepunguza kodi kwenye cement hadi mfuko mmoja uuze ths 6,000!! Wachovu wa magamba bana!

Hakumbuki wakati huo alikuwa mdogo!
 
Kwani ukitaja kasoro ni kwamba unamwamsha mtu atoke ndani ya box sasa wakati wa kutaja vipaumbele na strategies bado vumilia kua mpoleeee usikurupuke
 
Tangu nimeanza kufuatilia Upinzani Tanzania hasa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kupitia nyota wao Bw.Slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na CCM zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi WatanZania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (Watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila Mtz analijua hili?
Hata mtoto wa Shule ya msingi anajua kwamba kuna Watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (CHADEMA) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza Shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara Hospitali hakuna Dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua Sayari mpya na sasa anatuarifu...

Soma katiba ya chadema
Kwenye itikadi, mrengo, madhumuni na msimamo wa chama

Na mbona alisema ni kuwapata nafasi watumishi madaraka, kuwapa wanachi mamlaka ya kuenjoy nchi yao
 
Kwa hiyo hoja za Slaa ni guta science siyo?

Noted.
 
Ni kweli wao ni kutaja kasoro za watu lakini sijasikia ahadi yeyote ya kuondoa kero za watanzania kama ni jinsi gani elimu itaboreshwa, kuondoa kero ya foleni ambayo inaligharimu taifa hili kuliko kawaida. Nataka kusikia kuimarishwa miundombinu hasa reli na bandari. Uchumi wa nchi, Maisha na kipato cha mtanzania wa kawaida kitaboreshwa vip kwa kutumia rasilimali zetu za ndani( kwani wenzetu Rwanda na Kenya wameweza). Ndio ninataka kusikia sio huyu kazaa na fulani, huyu kaiba je tuna uhakika gani wewe hutaiba? Tunataka mtuambie kwa kweli nchi hii iko hoi sana

Hivi huwa unafatilia kweli anayoyaongea Dr Slaa na upinzani kwa ujumla?au unajitoa akili mkuu?
 
Tangu nimeanza kufuatilia Upinzani Tanzania hasa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kupitia nyota wao Bw.Slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na CCM zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi WatanZania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (Watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila Mtz analijua hili?
Hata mtoto wa Shule ya msingi anajua kwamba kuna Watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (CHADEMA) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza Shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara Hospitali hakuna Dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua Sayari mpya na sasa anatuarifu...

Kwa ufupi wewe ni product ya shule za kata 100%!! Kitu gani huelewi hapo? Unataka kuwa spoonfed Kama mtoto Wa kindergarten halafu unajaribu kutumia neno Kama "rocket science" ili tudanganyike kwamba wewe ni sophiscated intellectual kumbe ni Hot Air! Bs
 
Tusubiri muda ufike wa kampeini ndo tutaweza vizuri kuchambua. Lakini ninacho kijua wapinzani hawana jipya...ila ingekuwa vizuri wakawa wengi bungeni hats 45% ili tubalance pande zote
 
wewe ni mbea tu hujamsikiliza vema drvslaa alishasema mengi sana ila kwa umbea wako unagusia vitu vidogo vidogo
 
Kwa ufupi wewe ni product ya shule za kata 100%!! Kitu gani huelewi hapo? Unataka kuwa spoonfed Kama mtoto Wa kindergarten halafu unajaribu kutumia neno Kama "rocket science" ili tudanganyike kwamba wewe ni sophiscated intellectual kumbe ni Hot Air! Bs

Duh! Kwa hiyo kutumia neno ,,rocket science" ndiyo inamaanisha mtu ni intelectual? Halafu isitoshe kuna tatizo gani kusoma Shule ya Kata? Nimeshaelezea kitu nisichokielewa sasa sijui ni kwanini unaniuliza tena!
 
Hawajajiandaa kuwakomboa watanzania,angalia mfumo wao,je unawapa ahueni watendaji wao km makatibu wa wilaya na mikoa kulipwa mishahara mizuri.Tazama viongozi wa Taifa wanalipwa mishahara,posho za safari wakiwa mikoani ila watendaji wa mikoani hawalipwi na km wanalipwa ni kiduchu.Hivi kweli wanaweza kuwaletea wa TZ maisha bora wakati wao wenyewe hawapeani maisha bora!
 
Km ulimsikia akisema hayo,ina maana aliposema muda wa kampeni bado ukifika atashusha nondo zake,uliziba masikio!!?? Hata hivyo aligusia mambo machache,alitolea mfano wa train kwa nchi km yetu yenye rasirimali kedekede ni aibu kusafiri kwa train siku 3 wakati kuna train zenye kasi ya km-300 kwa saa!!. Sijui nini ambacho hujaelewa hapo..!

Bullet train.Ila mgombea urais CCM mwaka 2010 alisema atajenga standard gauge mpya from dar to kigoma sasa sijui inahamishiwa kwa muuza nyumba za serikali au.
 
The main function of the opposing party is to oppose each and every things,and propose nothing.
 
Duh! Kwa hiyo kutumia neno ,,rocket science" ndiyo inamaanisha mtu ni intelectual? Halafu isitoshe kuna tatizo gani kusoma Shule ya Kata? Nimeshaelezea kitu nisichokielewa sasa sijui ni kwanini unaniuliza tena!

Shule za kata is synonymous with low quality education which produces "educated illiterates" upo hapo!! or people who attended in the four walls of a classroom but never got educated an iota!
 
Sasa hapo kosa langu liko wapi mimi kusoma Shule unazoziita za Kata, si ndiyo shule ambazo nchi yangu imezijenga na ndio Elimu ambayo nchi yangu inatoa? Ulitaka nisome wapi ndio nifit kwenye hiyo standard yako?
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Tangu nimeanza kufuatilia Upinzani Tanzania hasa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kupitia nyota wao Bw.Slaa sijawahi kusikia hata siku moja akisema atafanya nini tofauti na CCM zaidi ya kukosoa tu!

Kwa mfano hapa juzi nilimsikia akisema siku hizi WatanZania hawali nyama, mara akasema wengi wetu (Watz) hatunywi chai asubuhi kwa sababu hatuwezi kununua chai jambo ambalo ni kweli lkn mbona kila Mtz analijua hili?
Hata mtoto wa Shule ya msingi anajua kwamba kuna Watz wengi hawawezi kununua nyama, kitu ambacho nimekikosa kwake ni kwamba suluhisho lake ni lipi? Yaani yeye (CHADEMA) watatua vipi hilo tatizo?

Utasikia mtoto anamaliza Shule ya msingi hajui kusoma wala kuandika mara Hospitali hakuna Dawa sijui tunapoteza masaa matatu barabarani kwenye foleni anaongea kana kwamba amegundua Sayari mpya na sasa anatuarifu...

Nilishamsikia Dr Slaa akisema:
1. Kupunguza matumizi ya serikali na kuelekeza nguvu zaidi kwenye maendeleo.
2. Kupunguza baraza la mawaziri kufikia 21 (kama sikosei).
3. Elimu bure hadi form 6 (kama sikosei).
4. Kupunguza gharama kwenye vifaa vya ujenzi ili Watanzania wengi waweze kuwa na makazi bora.
5. nk.
 
Back
Top Bottom