Hoja ya uhifadhi Loliondo hata wamasai wanaielewa

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
Kwa mara kadhaa nilikuwa nikifuatilia mikutano ya PM na Jamii ya Wamasai, kwenye ule utaratibu wa kuishirikisha jamii ya Kimasai kwenye masuala ya uhifadhi, mara nyingi kauli zao ni kwamba wapo tayari kuwa wahifadhi wazuri ikiwemo eneo la pori tengefu la Loliondo

kuna baadhi ya masai kwenye ile mikutano walikiri kbs zipo changamoto za kuchanganya mifugo na wanyama hasa nyumbu, na hata mbwa mwitu, wanakiri kupoteza idadi kubwa ya mifugo inayotokana na kushambuliwa na simba, chui na hata mbwa mwitu.

Pengine walimpongeza sana PM na Serikali ya Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kutenga muda kuwasikiliza kuelekea mchakato wa kuweka beacons ili kulinda ecolojia iliyopo Loliondo.

Swali hapa ni lipi? imekuwaje hawa watu wamebadilika ghafla? nani yupo nyuma ya haya, kwanini hadi wakenya nao wanaingilia hili suala.

kwanini kumekuwa na usambazaji wa picha za uongo kwenye tukio hili lenye nia nzuri ya uhifadhi wa eneo la pori tengefu la Loliondo.

Kwanini hawa wanaojiita wanaharakati kwa kushirikiana na Raia wa nchi jirani wanapotosha Kauli ya Waziri Mkuu tena kwa makusudi?

Uwekaji wa beacons kwenye hifadhi na mapori tengefu mbona ni jambo la kawaida Ruaha, Kilomajaro, Serengeti, Mkomazi, Tarangire na maeneo Mengine mengi tu kote huku beacons zimewekwa na hapakuwahi kuwa na shida au hamkuwa na maslahi napo?

Wamasai wanapaswa kutambua wanatumiwa vibaya ili watu wengine waingize pesa kutoka kwa wafadhili, Wamasai wanapaswa kitambua rafiki yao namba 1 ni Serikali ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa pamoja kwa kuwapa huduma kibao za kijamii.

Ni majuzi tu PM alisema kuwa pamoja na kuweka beacons, Serikali inachimba visima vya maji loliondo ambapo pamoja na mambo mengine huku watawekewa Majosho na Mabakuli makubwa ya kisasa ya kunyweshea wanyama na akasisitiza wakandarasi wapo site. Wamasai wanapaswa kutambua Serikali inajali ustawi wa shughuli zao na hawana budi kuisikiliza na ndio maana Serikali ilisema haina nia ya kuwatoa Loliondo bali kuweka alama ili kuonyesha wanapaswa kulisha mpaka wapi ili kulinda eneo la pori tengefu.

inashangaza sana kuona watu wanapush fujo kwenye suala la uwekaji wa beacons tena eneo hili lina umbali wa kilomita 8 kutoka vijijini, inafikirisha sana kuona Mtanzania anachochea masuala haya tena kwa kushirikisha jamii za kimataifa bila kujali maslahi ya taifa. Kama nilivyosema awali Serikali imekuwa ikiwahudumia hawa ndugu zetu Maasai kwa miaka yote na hata siku moja haijawah kuchoka, bila hata msaada wa hao mnaowaita wafadhili wenu.

Wasalaam

Mussa Mtike
Mzalendo Halisi
 
Back
Top Bottom