Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Declaration of Interest, japo mimi Paskali, ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini hoja zangu zote hutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuzitoa truthfully, with objectivity, impartiality na balance bila bias ya ukada wangu, nimetoa angalizo hili kwa vile watu humu wana vyama vyao na viongozi wao ambao wengine wana waabudia, hivyo nakijua fika kinachomfika mtu atakayepandisha hoja
yoyote, kuwapinga waabudiwa hawa.
Wajemini haya ni maoni na mtazamo wangu tuu and not necessarily I must be right, hivyo Mhe. Tundu Lissu might be right and I might be wrong!.

Naomba nianze kwa kumpongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ile ile ya uropokaji, hivyo kuonekana kama mropokaji fufulani katika kufikisha ujumbe wake, na kweli ujumbe unafika.

Kwanza naomba kukiri kuwa mimi Paskali licha ya kuwa ni mwandishi wa habari, pia ni mwanasheria, ila sio wakili, Mhe. Tundu Lisu ni mwanasiasa, ni mwanasheria, na ni wakili, hivyo kwenye kuzungumzia hoja za kisheria, mimi siatahili hata kukaza tuu gidamu za viatu vyake, mimi kwake kama just a layman.

Japo Lissu nimesoma nae shule moja ya Ilboru, yeye alikuwa kwanza mwanasheria kisha ndipo akawa mwanasiasa, mtu kuwa mwanasheria hakukufanyi always kuwa right kwenye hoja zote za kisheria na mtu kuwa just a layman, anaweza kabisa kutofautiana na mwanasheria mbobezi na layman akawa right, mfano ni huu
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele! | Page ...

Katika jinsi ya kupinga udikiteta Tanzania, Tundu Lisu ametuasa tupaze sauti zetu kuupinga huu udikiteta kwa kupiga kelele ambako huku ni kuipinga kisiasa, wakati hoja halisi ya udikiteta, sio hoja ya kisiasa ni hoja ya kisheria. Hoja za kisiasa zishughulikiwe kisiasa, na hoja za kisheria, zishughulikiwe kisheria. Kushughulikia kisiasa kwa hoja za kisheria, ni kujifurahisha tuu, kamwe hakutaleta matokeo yoyote chanya, kwavile hoja ya udikiteta ni hoja ya kisheria na Tundu Lissu ni mwanasheria, ilitarajiwa hoja hii ya udikiteta aishughulikie kisheria na sio kisiasa.

Naomba kutofautina na Mhe. Tundu Lisu katika hili la udikiteta, kwa hoja kuwa udikiteta haupingwi kwa Press Conference, kwa maandamano, kwa mikutano ya hadhara, kwa kupaza sauti na kupiga kelele.

Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative Orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, jee kweli upo, zikishindikana ndipo sasa sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.

Udikiteta wa Magufuli Ulianza Lini?.
Kuna wengi humu wanaousikia udikiteta wa Magufuli wakidhani umeanza leo, no!, kuna aina mbili za vyanzo vya udikiteta na aina mbili za udikiteta.
Vyanzo vya udikiteta ni
1. Hulka ya Udikiteta nimeizungumza hapa -
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na ...

2. Mazingira ya Udikiteta nimeyazungumza hapa
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

Aina za udikiteta

1. Udikikiteta Katili nimeuzungumza hapa-
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...

2. Udikiteta Uzalendo nimeuzungumza hapa-
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

Jee ni Kweli Tanzania Tuna Udikiteta?.

Hili ndilo swali kuu la msingi la kujiuliza, jee ni kweli Tanzania tuna udikiteta?.
Hili nimelizungumzia hapa
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...

Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...

Udikiteta wa Vyama: CCM ni chama cha Kidikiteta, Ila pia Chadema ni Chama cha Kidikiteta.
Zaidi ya udikiteta wa mtu, pia kuna udikiteta wa vyama ni jinsi vyama vinavyoendesha mambo yake, haswa wakati wa uchaguzi wa viongozi wake, vyama karibu vyote vinahubiri demokrasia, lakini in reality vingi vinaendeshwa kidikiteta kwa a systematic fallacies zinazoitwa taratibu!.

Udikiteta wa CCM katika uchaguzi wa viongozi wake, nimeuzungumza hapa
Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC! | Page 9 ...

Kwenye hili la udikiteta, hata Chadema pia ni chama cha kidikiteta, ndani ya Chadema ndio hawana kabisa demokrasia, afadhali hata ya CCM. Hiyo demokrasia wanayoihubiri, kuanzia kwenye jina la chama chao, " Chama cha Demokrasia na Maendeleo", ni jina tuu!. Chadema kingekuwa ni chama kweli cha maendeleo, hayo maendeleo yangeonekana basi kwa kuanzia pale Mtaa wa Ufipa, walipo!.

Chadema kingekuwa ni kweli ni chama cha demokrasia, hiyo demokrasia tungeanza kuiona katika uchaguzi wa ndani wa Chadema, tena kuna hatari, hata kama ni Chadema wengeshinda uchaguzi wa 2015, wangeweza kuendesha nchi hii kwa udikiteta wa ajabu kuliko hata huu tunaoushuhudia sasa. Hili nililiona na nililizungumza hapa
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...

Chadema na Matumizi ya Busara: Chama Cha Kiharakati, Hakiwezi Kupewa Nchi Kutawala!.
Chadema kuna tatizo kubwa la matumizi ya busara katika kauli za baadhi ya viongozi wake. Unaweza kukosoa kwa lugha ya kistaarabu na kwa unyenyekevu ukafikisha ujumbe vizuri zaidi kuliko kutumia lugha kali, machukizo, matukano na lugha isiyo ya staha. Wakati tukielekea uchaguzi wa 2015, tulishauri humu, ili Chadema kiweze kuaminiwa na kukabidhiwa nchi, ni lazima kionyeshe ukomavu, maturity, kufuatia kwa muda mrefu Chadema kujitanabaisha kama ni chama cha kiharakati, tulishauri Chadema kujibadili kutoka chama cha kiharakati, kuwa chama tawala in waiting, chenye kuonyesha uwezo wa kuongoza nchi.
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...

Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...

Hata walipounda UKUTA, akina sisi tuliwashauri humu
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane ...

A Way Forward Kuelekea 2020, Kwa Kwa Udikiteta Huu Uliopo, na Siasa Hizi za Chadema, Do They Stand A Chance?.
Chadema haiwezi kupasua na kuja kutawala nchi hii isipofanya mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa siasa zake, kutoka kwenye chama cha kiharakati kinachoendesha politics of populism and politics of confrontation into smart politics!.

Aina Tatu Za Kupiga Siasa
Kuna aina tatu, za kupiga Siasa, ya how to play the game of politics, hizi ni siasa za maendeleo, (developmental politics), siasa za kujifurahisha (politics of politiking), na kuna siasa za migogoro, (politics of confrontation).

1. Siasa za Maendeleo.
Hizi ni siasa zenye malengo ya kuleta mabadiliko chanya, changing for the better. Kila political move unayofanya, ina malengo chanya ya kuleta mabadiliko, siasa hizi zimefundishwa sana na Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha Binadamu na Maendeleo. Siasa hizi ni siasa zenye sera, ilani, malengo, mikakati na time frame, hizi mimi naziita SMART Politics, ni siasa zenye
S - specific, significant, stretching
M - measurable, meaningful, motivational
A - agreed upon, attainable, achievable, acceptable, action-oriented
R - realistic, relevant, reasonable, rewarding, results-oriented
T - time-based, time-bound, timely, tangible, trackable

2. Siasa za Kujifurahisha.
Hizi ni kauli za kisiasa kwa ajili ya kujifurahisha tuu to gain political mileage lakini hakuna chochote kinachofanyika, hizi zinajumlisha ahadi zisizotekeleka, hizi ni politiking, mtu unazungumza ili tuu uonekane na wewe upo upo. Kwenye kundi hili, zile siasa za bendera fuata upepo pia zimo kwenye kundi hili. Hizi ni siasa ambazo hazina maana yoyote kwa maendeleo!, huku ndiko siasa za fitna, majungu, uongo, zengwe etc, etc.

3. Siasa na Migogoro
Hizi naziita ni siasa za attention seeking, yaani kupinga tuu kila kitu ili tuu kuonekana na kutafuta public sympathy, lakini hizo moves hazina faida yoyote wala manufaa yoyote ya maana!. Hapa ndio pale watu wanapinga kila kitu hata kile chenye manufaa kwao kwa lengo la kutafuta tuu umaarugu, una buni mgogoro kupata the much needed attention. Siasa hizi hufanywa sana kwa mikutano ya hadhara na maandamano ambayo mwisho wa siku ni kusumbua tuu watu, kuwapotezea muda wao, na hakuna manufaa yoyote yanayopatikana!.

Mfano hai ni hii kampeni ya kupaza sauti na kupiga kelele ambayo Tundu Lisu anaihamasisha, japo ni kweli, Rais Magufuli ni kama dikiteta fulani hivi kwa kufanya udikiteta fulani hivi kama vile amevunja katiba kwa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kinyume cha katiba!. ( nimesema kama amevunja katiba, kwasababu mamlaka pekee ya kuthibitisha katiba imevunjwa ni Mahakama Kuu ya Tanzania). Chadema wanahamasisha watu waandamane, wapige kelele tuu kwa lengo la kupinga udikiteta nchini!. Sasa kitakachofanyika kwenye kelele hizi ni mabango na kauli chonganishi kuupinga udikiteta ili wananchi waone Chadema inapinga udikiteta wa Magufuli!. Kupinga huku ni kwa kujifurahisha tuu, kwa sababu hakutabadilisha lolote wala chochote katika tuhuma za udikiteta wa Magufuli, sana sana kama rais Magufuli ni dikiteta kweli, atawatandika na kuwaadhibu waandamanaji hao kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa katiba watu wakaishia kuumia na kujuta kuzaliwa!.

Kunahitajika SMART strategies kwenye kuupinga tuhuma za udikiteta wa rais Magufuli, ni kwa kutumia katiba na sheria, imeeleza wazi nini kinachotakiwa kufanywa pale kiongozi aliyeapa kuilinda katiba, akawa ndie wa kwanza kuivunja hiyo katiba!. Kupaza sauti kuupinga udikiteta sio njia sahihi ya kudeal na udikiteta wa mkuu wa nchi, haswa ukizingatia dikiteta mwenyewe, ni dikiteta mzalendo!, hicho anachofanya rais Magufuli, ndicho wananchi Watanzania wa leo wanachotaka na ndicho kinachoweza kufanyika kututoa Tanzania ya leo, hapa tulipo, kwenye nchi masikini yenye umasikini uliotopea, na kutufikisha kule tunakotaka kwenda, kujenga Tanzania ya viwanda kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi kufikia kuwa ni nchi nchi tajiri, a donor country!. Hivyo Watanzania wanaopenda maendeleo ya kweli, kama gharama ya maendeleo hayo ni pamoja na rais Magufuli kuwa dikiteta, then huu ni udikiteta mzuri, a benevolent dictatorship, Inakubalika duniani kote, hivyo rais Magufuli aendelee kukaza uzi kunyoosha nchi iliyopinda na kuchezewa kwa miaka mingi hadi kuitwa ni shamba la bibi.

Kama ulifuatilia ule mkutano wa Chadema wa Mwembe Yanga, ulioitangaza the list of shame, ni Tundu Lissu huyu huyu na viongozi wote wa Chadema walikuwa wakali sana kuhusu rushwa na ufisadi, huku wakiendesha siasa za uanaharakati. Miongoni mwa sala za wanaharakati hawa akiwemo Tundu Lisu ni kumuomba Mungu, atupatie rais dikiteta mwenye uwezo wa kudeal na rushwa na ufisadi uliotamalaki Tanzania kwa miongo kadhaa. Mungu katusikia sala zetu, katupatia rais benevolent dikiteta kweli, Dr. John Pombe Joseph Magufuli!, sasa wale wale waliokuwa wakipinga rushwa na ufisadi, sasa ndio hawa wamewakumbatia waliokuwa mafisadi wale wale wa kwenye the list of shame na sasa ndio wanaopiga kelele kulaani rais Magufuli ni dikiteta!.
Ukweli Mchungu wa 2020.
Hakuna kitu kigumu kukizungumza humu jf kama ukweli mchungu!, wengi wetu humu wataanza kuizungumzia 2020 on 2019, by that time it will be too little too late!, sisi waona mbali, tunaizungumzia 2020 sasa, ili kutoa muda wa gestation period ya kujipanga and to do something worthwhile before its too late.
CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...

Kwa siasa hizi Chadema inazokwenda nazo, kwenye mazingira ya tuhuma hizi za udikiteta huu uliopo, kama hawatabadilika, I'm very sorry to say....
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani ...

In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa ...

Paskali
Rejea Kuhusu Udikiteta.
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ..

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

Rejea Kumhusu Tundu Lisu
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni ...
Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza ...
Usiyoyajua Kuhusu Nyerere: Shuleni Alikuwa Toto Tundu!, Almanusura ...
Kazi nzuri Tundu Lissu Antipas! | Page 10 | JamiiForums | The Home ...
Swali la Kizushi: Kwa Nini Job Ndugai Anamuogopa Tundu Antipasi ...
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau ...
 
Wanabodi,

Kwanza nampongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ya uropokaji hivyo kuonekana kama insane fulani, lakini ujumbe umefika.

Kwa vile Mhe. Tundu Lisu kwanza mwanasheria kisha ndio mwanasiasa, ametuasa tupaze sauti zetu kuupinga huu udikiteta kwa kupiga kelele. Naomba kutofautina na Mhe. Tundu Lisu katika hili la udikiteta, kuwa udikiteta haupingwi kwa Press Conference, kwa maandamano, kwa mikutano ya hadhara, kwa kupaza sauti na kupiga kelele.

Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3. (
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, zikishindikana ndipo sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.

No matter how good someone is, it's not necessarily he/she will always right, na kwa jinsi nilivyomsikia Lisu akimzungumzia rais Magufuli, kama Chadema ndio kinawategemea watu kama hawa kuuingiza ikulu, kiukweli Lisu atawaingiza chaka Chadema kama alivyowaingiza kwenye chaka la katiba.

Tundu Lisu is good in his own way ila sio mtu very dependable yanapokuja masuala nyeti yenye kuhitaji vichwa vilivyotulia. Aendelee kutumika kwenye amsha amsha lakini kwenye very serious issues zinazohitaji busara, Lisu anahitaji usaidizi wa wenye busara.

Chadema kuna tatizo kubwa la matumizi ya busara katika kauli za baadhi ya viongozi wake. Unaweza kukosoa kwa lugha ya kistaarabu na kwa unyenyekevu ukafikisha ujumbe vizuri zaidi kuliko kutumia lugha kali, machukizo, matukano na lugha isiyo ya staha.

Naomba kuwasilisha.

Paskali
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ..

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa

Pole Paskali more often than not unawaya waya tu, kama mtu usiyejua unachokitaka ama unachokisimamia, poor you! You are no credible analyst, rather simply a world class opportunist kama mtu fulani kafiwa na mwenza hapa Uhengani! Bs
 
Ndugu yangu Mayalla, Prelogative Orders hazitafutwi au kuombwa mahakamani kama maombi mengine yanavyoombwa. Prelogative orders hazitolewi kwa sababu tu nchi inaendeshwa kidikteta. Nchi inaweza kuendeshwa kidikteta lakini kukawa hakuna misingi ya kudai Prelogative orders. Orders hizi zina misingi yake na miiko yake ya kipekee kabisa iliyopo kisheria, na wala haziwezi kutolewa katika misingi ya kisiasa.
 
Acha kuwa mnafiki.We mwenyewe nini kinakushinda kwenda mahakamani wakati huwa unamponda kwa udikteta?
.
JF imekupa hadhi na heshims kubwa ya mada zako kutounganishwa lakini hiyo hadhi sometimes bora wangepewa wengine
Huyu ni mnafiki wa siku nyingi sana!!! Mwanzoni alisifia sana serikali, akawa anatafuta tonge! Alipoona hakuna dalili za tonge( yaani kupewa ka cheo kokote ndani ya serikali), akaanza kuchafua hali ya hewa! So, huyu jamaa ni ndumila kuwili design Fulani..!!! Huyu huku kwetu musoma simtofautishi na kitu kinaitwa "msimbe" yaani mwanamke unaeweza kumchukua ilimradi uwe na pesa..!!!
 
Paskali my brother nakuunga mkono kwa ulicho kisema japo sio mbobezi wa sheria je pale unapoona mahakama hazitendi haki(kuna mifano kadha wa kadha wa mahakama kuingiliwa na kupewa order na mamlaka au taasisi ya uraisi kwa baadhi ya kesi za kisiasa)je huoni huu uropokaji wa Tundu Lissu unakwenda much wider kushinda hizo charges kama sio tafsiri za kisheria unazo shauri zifuatwe?
 
Mayala kwa kisukuma maana yake njaa!

Kabla ya kutoa opinion ni bora ukawa unajiumiza kidogo kufanya utafiti na kujua nature ya suala ndugu Mayala,Ukiudisect ushauri wako, utaona kwamba ushauri wako ni one dimensional kwa issue complex ambazo kiuchache dimensions zake ni Legal-Social-Political!

Sasa, huwezi kuja na jibu jepesi kama hilo ulilolisema ndugu Mayala katika issue yenye dimensions nyingi!

Halafu unatumia Logical Fallacy ya Ad-hominem attack kwenye hoja yako ( yaani unashambulia personality ya mtu), kwa mfano maneno kama vile " anaropoka" hayaifanyi hoja yako iwe na nguvu!

Je wewe ndugu Mayala umeshafungua kesi mahali popote?, au unamsubiri Lissu afungue ili uje tena hapa uanzishe thread akishindwa mahakamani?.

Ndugu Mayala if you think you are right then lead the way!!
 
Wanabodi,

Kwanza nampongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ya uropokaji hivyo kuonekana kama insane fulani, lakini ujumbe umefika.

Kwa vile Mhe. Tundu Lisu kwanza mwanasheria kisha ndio mwanasiasa, ametuasa tupaze sauti zetu kuupinga huu udikiteta kwa kupiga kelele. Naomba kutofautina na Mhe. Tundu Lisu katika hili la udikiteta, kuwa udikiteta haupingwi kwa Press Conference, kwa maandamano, kwa mikutano ya hadhara, kwa kupaza sauti na kupiga kelele.

Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3. (
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, zikishindikana ndipo sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.

No matter how good someone is, it's not necessarily he/she will always right, na kwa jinsi nilivyomsikia Lisu akimzungumzia rais Magufuli, kama Chadema ndio kinawategemea watu kama hawa kuuingiza ikulu, kiukweli Lisu atawaingiza chaka Chadema kama alivyowaingiza kwenye chaka la katiba.

Tundu Lisu is good in his own way ila sio mtu very dependable yanapokuja masuala nyeti yenye kuhitaji vichwa vilivyotulia. Aendelee kutumika kwenye amsha amsha lakini kwenye very serious issues zinazohitaji busara, Lisu anahitaji usaidizi wa wenye busara.

Chadema kuna tatizo kubwa la matumizi ya busara katika kauli za baadhi ya viongozi wake. Unaweza kukosoa kwa lugha ya kistaarabu na kwa unyenyekevu ukafikisha ujumbe vizuri zaidi kuliko kutumia lugha kali, machukizo, matukano na lugha isiyo ya staha.

Naomba kuwasilisha.

Paskali
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ..

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa

Pascal you can not eat the cake and still have it...
 
Kwa sasa mahakama kuu ya Tanzania sio Taasisi huru,majaji wanaingiliwa kwenye shughuli zao mpaka wanaamua kujiuzuru,

Na kama mahakama inaingiliwa kwenye kutenda haki,haki zetu tuzitafutie wapi?je kuna haja ya kupeleka kesi mahakamani katika hali hii au tuangalie namna nyingine? Kama unazizuia mahakama zisitupe haki,na sisi kama nchi tunataka haki na tumekubaliana kikatiba tutaipata mahakamani,na wewe umezizuia mahakama zisitoe haki,nchi nzima ikiamua kutafuta mbadala wa mahakama nchi hii itakalika?

Wabunge bungeni mnawafukuza na kuwatisha,mnataka taifa lisemee wapi? Bunge ni mahala pa mijadala ya taifa,wakianza kujadili mnawafukuza na kuwatisha

Serikali nayo ikisikia watu wanatumia Uhuru wao kujadili,wanatuma polisi kuwakamata

Kuna kihadithi fulani kinasema kwamba hata umuwekeee vifaranga mia,ukimuachia tu,mwewe atapaa na kuondoka,Uhuru ni kitu cha asili cha binadamu,

Mkoloni na mabomu yote na mabunduki,hakufanikiwa kumnyamazisha Nyerere,kenyata,Mandela,Mugabe,

Leo karne ya 21 unawaza kuzuia watu wasiongee?

Wapinzani waliongea tena kwa ruksa na kukingiwa kifua na Nyerere baada ya tume ya Nyalali,

Leo wewe ni nani wa kumshinda Nyerere busara? Wewe unaweza kumshinda baba wa taifa kwa maono? Ccm walikataa vyama vingi,Nyerere akawaambia acheni ujinga,na wakati Mkapa anaomba urais,nyerere hakuzuia wapinzani wasipige kampeni,alisema muacheni Lyatonga mashabiki wake wamsukume gari lake,mrema yuko mwanza kwenye kampeni ,nyerere yuko mbeya,hakuamuru lyatonga akamatwe

Mtoto wa Nyerere alikuwa NCCR,Nyerere wala hakuumia kichwa... Leo hii unataka kufukia jalalani busara za Nyerere? Kwa ugwiji upi wa kisiasa ulio nao?

Mwinyi alitaka kuleta Tanganyika,Nyerere akamwambia ilani tuliyokupa haina hiyo hoja,umeitolea wapi? Leo ilani INA hoja ya mimba za wasichana,unaikataa,kwa hiyo kwenye kampeni mlikuwa mnawadanganya watu? Ccm itwambie kwamba ilani yao iko kichwani kwako au wana kitabu maalum cha ilani kinachoongoza mambo mbalimbali ikiwemo Uhuru wa mahakama
 
Wanabodi,

Kwanza nampongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ya uropokaji hivyo kuonekana kama insane fulani, lakini ujumbe umefika.

Kwa vile Mhe. Tundu Lisu kwanza mwanasheria kisha ndio mwanasiasa, ametuasa tupaze sauti zetu kuupinga huu udikiteta kwa kupiga kelele. Naomba kutofautina na Mhe. Tundu Lisu katika hili la udikiteta, kuwa udikiteta haupingwi kwa Press Conference, kwa maandamano, kwa mikutano ya hadhara, kwa kupaza sauti na kupiga kelele.

Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3. (
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;

me huwa nakuelewaga mkuu Pascali na mada zako,mfano hii lengo si kumponda mh Lissu bali nikuwafanya wanaJF na watz kote tuone na kusikia alichokiongea mh rais Lissu,unasaidia kusambaza taarifa,asante
 
Ahsante sana Mkuu kwa kuweza kuona unafiki na undumilakuwili wa huyu mkolomije.

Huyu ni mnafiki wa siku nyingi sana!!! Mwanzoni alisifia sana serikali, akawa anatafuta tonge! Alipoona hakuna dalili za tonge( yaani kupewa ka cheo kokote ndani ya serikali), akaanza kuchafua hali ya hewa! So, huyu jamaa ni ndumila kuwili design Fulani..!!! Huyu huku kwetu musoma simtofautishi na kitu kinaitwa "msimbe" yaani mwanamke unaeweza kumchukua ilimradi uwe na pesa..!!!
 
e82babc4965584a84c625487cdd455b9.jpg
 
Back
Top Bottom