Hoja ya msingi ya spika haijajibiwa na serikali kupita waziri wa elimu

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Hoja ya msingi ya spika iliyokuwa inataka majibu ya serikali ni hii hapa:

Vyuo vyote vinadai malipo mengine kabla ya kusajiliwa na ambayo hayapo kwenye boom. Malipo haya ambayo ni lazima mwanafunzi alipe ndiyo asajiliwe hata kama amepewa mkopo maana hayapo kwenye mkopo. Malipo haya huitwa administrative fees au other fees au other direct costs to the university!

Spika alikuwa anahoji uhalali wa malipo hayo kudaiwa kwa mwanafunzi ambaye amethibitika kuwa hana uwezo na kupewa mkopo na bodi.

Tulitegemea waziri aidha ayatetee malipo haya au ayapinge! Lakini hakuyasemea kabisa. Kama kuna ulazima wa malipo haya basi yangeingizwa kama kipengele mojawapo kwenye mkopo ili mwanafunzi asisumbuliwe! Kiasi kinachotozwa kinatofautiana kati ya Chuo na Chuo.

Vingine hutoza mpaka zaidi ya laki tatu! Matokeo yake mwanafunzi hutumia boom kuyalipia halafu akabaki hana hela za chakula na akabaki akiteseka!
Napendekeza spika akomae zaidi mpaka serikali ije na kauli inayoeleweka kuhusu hili!
 
Back
Top Bottom