Zitto, Mnyika watikisa Korogwe |
Monday, 20 February 2012 07:27 |
Boniface Meena, Korogwe WABUNGE wa Chadema, Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini na John Mnyika wa Ubungo, wametikisa wilayani Korogwe baada ya wananchi kuwataka wawe mstari wa mbele kupigania hasa zao la mkonge, ambalo wabunge wao wanalisaliti. Pia, wananchi hao walimtaka Zitto kuhakikisha anarudisha hoja binafsi ya kutaka zao la mkonge liwe zao la mwaka 2012 kwa sababu mbunge wao, Yusuf Nassir, amewasaliti kwa kushawishi Spika wa Bunge kuzuia hoja hiyo. Wakizungumza kwa hasira mbele ya wabunge hao wa mkutano wa hadhara, wananchi hao waliwataka wawe watetezi wao kutokana na unyanyasaji wanaopata kutoka kwa wabunge wa CCM. Walimshtaki mbunge wao kwa Zitto wakitaka akamshughulikie ipasavyo kwa kuwa, anawasaliti wananchi wa Korogwe kwa kushindwa kutetea mkonge huku akijua ndiyo kazi yao kubwa. Katibu wa Wakulima Wadogo wa Shamba la Mwelya/Usambara, Ernest Mbezi, aliwaeleza Zitto na Mnyika kuwa wanashangaa mbunge wao na wengine wa Tanga kushindwa kuwatetea katika zao la mkonge. Akijibu hoja hizo, Zitto alisema atahakikisha anawasaidia wananchi hao kutetea hoja zao ili waweze kunufaika na mkonge, ambao ni zao linalowasaidia kwa maendeleo. Tunataka kila mkulima amiliki shamba lake la mkonge na aweze kufaidika na kilimo cha zao hilo, ili maendeleo na uchumi wa Tanga uweze kukua, alisema Zitto. Kabla ya mkutano huo, wabunge hawa walitembelea shamba la mkonge Mwalya/Usambara kujionea jinsi kilimo hicho kinavyofanyika na baadhi ya wakulima walisema kama wasipopigania zao hilo uchumi waoutaendelea kudidimia. Kwa upande wake, Mnyika alisema Serikali ya CCM na wabunge wake wamekuwa wakiwadanganya wananchi kuhusu mambo mbalimbali, ikiwamo suala la zao la mkonge ambalo linahitaji kusaidiwa. Mnyika alisema hali ya Serikali ya CCM sasa ni mbaya, imefanya uchumi wa nchi kuyumba kitendo ambacho kinafanya maisha ya wananchi kudidimia. Updates kutoka ukurasa wa Twitter wa Mh. Zitto 21/2/2012 - Ziara ya Tanga Jana tumemaliza Muheza.Tumekwenda kata ya Zirai-ambapo shule yao ya kata kati ya wahitimu 63 (form4),61 wamepata sifuri na wawili darajala 4. Tumehutubia Muheza mjini.Ujumbe wetu jana ni 'ukosefu wa ajira na ufisadi waweza kuangamiza Taifa iwapo hatua hazitochukuliwa. Sisi tunaelekeza nguvu kuisukuma Serikali kuweka fursa za uwekezaji kwenye Kilimo na viwanda vya Kilimo(uchumi wa vijijini) ili kukuza Ajira. Katika kupiga vita ufisadi, tutaendelea kuibua kashfa za ubadhirifu wa Mali za umma Kama njia ya kuzuia (deterrent). #ZiarayaTanga |
Hivi watu wa Tanga wanajua tofauti kati ya siasa na dini?
kila mwaka wanaipigia ccm kura hawa
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!
Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...

Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali! Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
Siamini kuwa Mh. Zito alivamia ajenda kama ulivyoandika ila nadhani lengo lake lilikuwa ku-speedup process ambayo ilikuwepo. Kuhusu kulifanyia siasa sidhani kwani hata wananchi wanaonekana wangependa ajenda ile ijadiliwe mapema, hata hivo maamuzi ya bunge yalikuwa sahihi pia kwani ni vema ukafanyika kwanza upembuzi yakinifu kabla ya kutekeleza.Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!
Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
........Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!
hio ajira itatoka wapi? na.. ni ya aina gani kwani mipango yote ya mwanzo imekufa kabisaaaa nikianza na ndege treni .meli . viwanda ndio kabisaa serikali yetu ya ccm yako imeuwa kwa makusudi viwanda vyote mmeviuza chuma chakavu
kuhusu bunge ndio wala hakuna tegemeo kwani mara nyingi nimeona ukikalishwa chini kwenye hoja zako hakuna anaezijali mpaka ccm ife ndio bunge litakuwa na maana sio hili mmejadili jairo na wenzake hakuna lolote mmefaidika binafsi kula posho kodi zetu
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!
Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...
HKigwangalla,
Ajira kwa vijana ni suala nyeti sana. Na suluhu yake ni mtambuka hivyo lazima kila sekta ibainishe wazi mikakati yake jinsi ya kuzalisha na kuzilinda ajira kwa vijana. Iwapo utapenda kuwashirikisha watu wengi zaidi nje ya "Vijana Wabunge", basi nami nitakuwa tayari kukushirikisha nilichojifunza toka BEE Policy ya Afrika Kusini, jinsi ilivyoingizwa karibu katika kila sera ya uzalishaji na huduma za jamii, inavyotekelezwa na vyombo mbalimbali vya serikali na sekta binafsi na mafanikio na mapungufu yake. Naamini BEE Policy ina mengi ya kuchangia kuboresha hoja ya Ajira kwa Vijana.