Sayansi ndio iliyoelezea habari za mfumo wa cells na mwili wa mtu kwa upana wake
Sayansi hiyo hiyo ambayo umetumia maneno yake kama reference kwasababu unaikubali kuwa ipo sahihi, kumbuka ndio sayansi hiyo hiyo iliyopinga habari za uwepo wa Mungu.
Ebu jaribu kufikiria kidogo, pamoja na vitu vyote hivyo vinavyozungumzia mfumo wa binadamu wa ndani mpaka nje ambavyo kwako vinaonekana ni very complex lakini bado sayansi hiyo hai-link swala hilo na habari za Mungu.
Pengine tungeitegemea kuiona Sayansi inakuwa ya kwanza kututangazia habari za Mungu kutokana na kile ilichoweza kukibaini kupitia tafiti zake zinazo shangaza, lakini haijawa hivyo.
Au kama Sayansi ilikuwa imejipanga tangu mwanzo kutokubali uwepo wa Mungu basi ingetuepushia mbali na hizi siri zilizopo ndani ya mwili wa binadamu ambazo watu wakianza kufikiria uchakataji wake wa kazi ulivyo wa ajabu wanaweza kufikia jibu la Mungu. Lakini kwanini ikaendelea kuweka vitu wazi?
Sasa hapo una machaguo mawili
- Ni eidha ukubali kuwa sayansi sio ya kweli (ambapo itakuwa ni pamoja na zile habari za cells ulizozichukua kama hoja za kweli)
- Au ukubali kuwa sayansi ni ya kweli kwasababu inatoa maelezo ya kweli na kwakua Sayansi hiyo hiyo imepinga uwepo wa Mungu basi jambo hilo lazima liwe kweli (kitu ambacho huwezi ukakubali)
Nikijiweka katika nafasi yako kiukweli naona upo umuhimu wa kuwa na machaguo mengi zaidi ya mawili
Kwa bahati mbaya ni kwamba unavyozidi kuongeza machaguo unazidi kulazimisha majibu yale unayoyataka wewe, majibu uayoyataka wewe ni pamoja na yale yasio sahihi.
Utachagua hizo option mbili ambapo kati yao kuna jibu sahihi au utavuruga mtririko wa hoja kwa kujiongezea options nyingine zaidi ili kuruhusu majibu yanayo kuridhisha? (yasio sahihi)
Uchaguzi ni wako