HOJA YA KATIBA: JK amvuruga Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA YA KATIBA: JK amvuruga Mnyika

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  HOJA YA KATIBA:JK amvuruga Mnyika
  Sunday, 02 January 2011 21:10

  [​IMG]Mussa Mkama

  KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kwamba anaanza mchakato wa kuandikwa upya Katiba ya Tanzania, imefilisi hoja binafsi ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye jana alitoa tamko rasmi kueleza kuwa amesitisha kwa muda mpango wa kuiwasilisha hoja hiyo bungeni, mwezi Februari mwaka huu.

  Katika tamko hilo lenye kurasa sita na kichwa cha habari "Kauli yangu juu ya tamko la Rais Kikwete kuhusu Katiba Mpya" Mnyika alisema kwa mazingira yaliyopo, anasubiri utekelezaji wa serikali katika suala hilo.

  "...Katika mazingira hayo, nasubiri kwanza ufafanuzi wa serikali kuhusu mchakato huu ikiwemo kujua kwa kina muundo wa tume, hadidu za rejea na kama serikali itapeleka bungeni mapendekezo kuhusu mchakato, kabla ya kutoa kauli kuhusu hatma ya hoja binafsi ambayo nilitoa taarifa kuwa nitaiwasilisha bungeni katika mkutano wa mwezi Februari,"alisema Mnyika na kuendelea:

"na katika kipindi ambacho nasubiri ufafanuzi wa serikali ambao inapaswa kuuweka hadharani, nitaendelea na hatua ambazo nilizitangaza nilipokwenda kuwasilisha taarifa ya hoja tarehe 27 Desemba 2010.

  "

Mnyika ameendelea kueleza katika tamko hilo kuwa " kutokana na kauli ya Rais Kikwete na hatua za ziada ambazo natarajia kutoka kwa serikali, nitatumia wiki ya kwanza ya mwezi Januari kukutana ana kwa ana na baadhi ya viongozi wa asasi za kiraia, taasisi za dini na vyama vya siasa ikiwemo Chadema, kuweza kushauriana hatua za ziada za kuchukua."

  Aidha alisema "natambua kuwa kauli ya Rais Kikwete kukubali kuandikwa kwa katiba mpya, inaashiria mabadiliko ya kimtazamo kwa upande wake pia ukilinganisha na kauli zake mbalimbali katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka 2010 kuhusu suala la mabadiliko ya mfumo wa utawala katika taifa, hali inayoashiria kwamba ametambua kuwa umuhimu wa katiba mpya ni wa Watanzania waliowengi."

  
Hata hivyo alieleza kuwa pamoja na rais kukubali kuandikwa kwa katiba mpya, bado Watanzania wanahitaji kujadili kwa kina na kwa haraka kuhusu mchakato uliopendekezwa ili taifa liende katika mkondo sahihi wa kuanza kutoa maoni.

  
"Suala hili ni la msingi kwa kuwa Historia ya Taifa letu inaonyesha kwamba Tume zilizoundwa na Marais na kushughulika na masuala yanayogusa Katiba hazikuweza kukidhi matakwa ya wananchi kwa sababu mbalimbali," alisema Mnyika na kuongeza:

"Mathalani, taifa linajadili sasa kuhusu mabadiliko ya katiba kutokana na kasoro katika hatua za awali za kuandikwa kwa Katiba ya Kudumu ya Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ndiyo tunayoitumia hivi sasa pamoja na marekebisho yake."

  
Aliendelea "Mchakato uliotumiwa na Rais wa wakati huo, Marehemu Julius Nyerere ndio ambao unajitokeza sasa kwenye hotuba ya Rais Kikwete kwa kueleza kwamba Rais anaunda tume na baadaye mapendekezo ya tume yanakwenda moja kwa moja kwenye vyombo vya kikatiba bila kwanza kuwa na matokeo ya utaratibu huu, ni wananchi kutoshirikishwa kwa ukamilifu wake katika maamuzi yanayohusu katiba."

  "Matokeo ya mfumo huo ni kuandikwa kwa katiba isiyokubalika na umma kwa uwingi wake na kusababisha mpaka sasa marekebisho (viraka) mara kumi na nne na bado kuna mapungufu mengi kwa kiwango cha sasa kukubaliana kuandika katiba mpya," alisema.

  "Katika mazingira hayo, ndipo panapojitokeza umuhimu wa kuwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa katiba kabla ya mapendekezo ya katiba kupelekwa kwenye mamlaka za kikatiba ambazo kwa mujibu wa katiba ya sasa ibara ya 98 ni Bunge pekee."

  Mnyika aliendelea kueleza kuwa kauli ya Rais Kikwete inaashiria kwamba wananchi hawatahusishwa moja kwa moja kwenye kuamua katiba, badala yake tume itachukua maoni yake na baadaye maamuzi yatafanywa na bunge kwa niaba yao kama ilivyo kwenye marekebisho ya kawaida ya katiba kwa mujibu wa ibara ya 98 ya katiba.


  Mbunge huyo kwa tiketi ya Chadema, aliwasilisha taarifa ya kutaka kupeleka bungeni hoja binafsi ya Katiba Mpya Desemba 19 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine alipinga pendekezo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda la kuunda tume ya kuangalia mchakato huo.

  "Ibara ya 8 kifungu cha kwanza cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mapungufu yake inaeleza wazi umuhimu wa wananchi kushirikishwa katika uundwaji wa katiba. Pia Ibara ya 63-(2) nayo inaeleza wazi," alisema Mnyika.


  Aliongeza kuwa kama mbunge ana haki ya kuwasilisha hoja binafsi kuhusu katiba mpya na kwamba ni vyema suala la uundwaji wa katiba likarejeshwa mikononi mwa Bunge kwa kuwa ni mhimili wa dola unaofanya kazi kwa niaba ya wananchi.

  "Ibara ya 98 ya katiba ndio sehemu pekee inayozungumzia marekebisho ya katiba hivyo ni wakati muafaka suala hili la katiba likapelekwa bungeni ili wananchi wawakilishwe," alifafanua Mnyika.

  "Unajua katiba ni sheria na kwa kuwa bungeni ndiko kunakotungwa sheria basi wanaopaswa kutoa mwelekeo wa katiba mpya ni Bunge," aliongeza.

  "Pia katiba ni mkataba kati ya wananchi na watawala... ikumbukwe kuwa anayeandika mkataba ni mwenye mali, na hapa mwenye mali ni mwananchi na Bunge lipo kwa ajili ya wananchi. Kutokana na hilo, ipo kila sababu ya suala hili kurudi bungeni."

  Msimamo wa Mnyika kupeleka hoja binafsi bungeni aliutoa siku mbili baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuamua kulibeba suala la madai ya katiba mpya, akisema kuwa atamshauri Rais Jakaya Kikwete kuunda timu ya kushughulikia suala hilo.

  Pinda alitangaza uamuzi huo Desemba 19 katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam katika kipindi ambacho kilio cha katiba mpya kinaongezeka kila kukicha.

  “Isije watu wakadhani serikali ina kigugumizi; hapana. Sasa mjadala umeiva na ni vizuri lizungumzwe kwa utaratibu. Nipo tayari kuzungumza na rais. Nitamshauri mzee (rais) na nitaweka nguvu zangu huko, hilo halitawezekana tusipoweka ‘initiative’ (juhudi),” alisema Pinda.

  "Watu wasifikiri wala kuona kuwa serikali haioni kama madai ya katiba mpya kuwa si ya msingi.
  “La pili, tunataka kuzungumza machache, lakini kubwa ni hili la katiba mpya. Kumekuwa na maelezo mengi, marefu, mjadala mkali;

  sasa hili nataka niseme tusione kama madai ya katiba si ya msingi sana; hapana. Ni ya msingi. Kwa serikali mabadiliko ya katiba ni utaratibu wa kawaida kwani ni jambo lililo ndani ya katiba,” alisema Pinda.

  “’All along’ Watanzania wameendelea kuibuka na kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Tulipofikia tunaulizana 'kuna ugumu gani kukaa na kuandika katiba mpya?"

  Aliongeza kusema: "Mimi binafsi sioni tatizo kwa hilo kufanyika, lakini kama serikali zipo namna mbili za kulishughulikia. Moja ni kutafuta utaratibu wa kumshauri rais aunde kamati ya watu wangalie maeneo gani ya kuingiza katika katiba hata ikibidi wananchi waulizwe yatoke ya kuwekwa mezani kwa kuhusisha vyama vya siasa na wanazuoni.”

  Pinda aliitaja njia ya pili kuwa ni rais kuunda timu yake ya kiserikali itakayoangalia mapendekezo ya tume zilizoundwa awalikuangalia marekebisho ya katiba na kuchukua mapendekezo yaliyojirudia yatakayoonekana kufaa kuingia katika katiba.

  Alisema kutokana na tume hizo yapo yaliyotekelezwa na yale ambayo yaliahirishwa akisema kuwa pengine ni kutokana na wakati. Hata hivyo alisema ni bora kuruhusu tume itakayokuwa pana na kuyatazama mapendekezo ya tume za awali, kuangalia na kushauri akisema kuwa huenda ikaona mambo mengine.

  “Ni bora kuruhusu tume pana ya kutazama, tushauri na kuangalia, pengine tukiyaona ya utawala si katiba mpya bali kitu kingine. Katika katiba yapo mema mengi tusiangalie ubaya tu, katiba hiyo ndiyo imetufikisha hapa taifa likiwa na sifa za utawala bora na mambo mengine,” alisema Pinda.

  Lakini Mnyika alipingana na Pinda kuhusu hoja ya kuundwa kwa timu ya kuchunguza madai hayo akisema "Sikubaliani na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu katiba.”

  “(Waziri Mkuu) Amesema atamshauri rais kuunda timu itakayoangalia mapendekezo ya tume zilizoundwa na pia kuanzisha utaratibu wa marekebisho ya katiba. Naona kauli yake haijalenga kuwepo kwa katiba mpya, bali inalenga zaidi marekebisho ya katiba."

  Hata hivyo mjadala huo wa katiba ulifungwa Desemba 31 mwaka jana baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuanza mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya.

  "Nimeamua kuunda tume maalumu ya Katiba, yaani Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakialisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano," alisema Rais Kikwete alipokuwa akitoa salamu zake za mwisho wa mwaka.

  Tangu kumalizika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, Chadema imewasha moto wa mabadiliko ya katiba na kufufua mjadala wa kutaka kuandikwa kwa katiba mpya kiasi cha Waziri Pinda kuamua kutoa tamko kuwa atamshauri Rais Jakaya Kikwete aunde tume kuchunguza madai hayo.

  

Miongoni mwa viongozi waliojiunga kwenye mjadala huo wa kutaka katiba mpya ni mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Sinde Warioba na Frederick Sumaye, Jaji Mkuu Agustino Ramadhan na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alitahadharisha kuwa bila ya katiba mpya nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Suala la katiba mpya, JK na serikali yake hawana mamlaka ya kutuburuza ili walichakachue nje ya Bunge.........................Ni Bunge tu ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria na kama halikuhusishwa tangu mwanzo na kuachwa mwishowe lije tu kubariki (rubber stamp) kazi ambayo tayari imekwisha kuvurugwa tutaendelea kudai katiba mpya............................

  JK anavyokuja anataka kuendeleza ubabe wa viongozi waliomtangulia wa kutuandikia katiba yao na kuivika joho la kuwa ni yetu kwa ushirikishwa wetu wa kijuu juu tu..........tunataka katiba mpya ambayo tutashiriki haswa katika kuiunda hiyo tume ambayo yapaswa kuwa ni mkutano wa kikatiba siyo mtu mmoja anaiunda atakavyo yeye kwa kujaza maswahiba wake ambao mwishoni wanasema yale mambo muhimu ya utawala bora siyo kilio cha watanzania............na hivyo wanayaondoa.......................................

  Wakifanya hivyo kilio chetu cha katiba mpya kitaendelea kuwa pale pale...................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Mnyika yasubiri tamko la serikali


  Na Grace Michael

  MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika amesema kuwa anasubiri ufafanuzi wa serikali kuhusu suala zima la katiba ikiwemo muundo wa tume, hadidu za rejea na kama serikali itapeleka bungeni mapendekezo kuhusu mchakato kabla
  ya kutoa kauli kuhusu hatma ya hoja yake binafsi ambayo alitarajia kuiwasilisha bungeni.

  Alisema kuwa wakati akisubiri ufafanuzi wa serikali ambao inapaswa kuuweka hadharani, ataendelea na hatua ambazo alizitangaza katika uwasilishaji wa taarifa ya hoja yake Desemba 27, mwaka jana.

  Taarifa iliyotolewa jana na mbunge huyo ilisema kuwa kutokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete, atatumia wiki ya kwanza ya Januari kukutana ana kwa ana na baadhi ya viongozi wa asasi za kiraia, taasisi za dini na vyama vya siasa ikiwemo CHADEMA ili kushauriana hatua za ziada za kuchukua.

  Kama nilivyoeleza awali, hoja hiyo pamoja na kuwa inaitwa hoja binafsi kwa kanuni za bunge na mimi ni mwakilishi, lakini ni ya umma kwa sababu katiba mpya ni hitaji la wananchi, hivyo maamuzi kuhusu hatma ya hoja husika yatafanywa kwa kushauriana na wananchi na wadau wengine baada ya kupata ufafanuzi wa serikali,� alisema Bw. Mnyika.

  Alisema kuwa kabla ya wananchi kuanza kutoa maoni kuhusu maudhui, alitoa mwito kwa wadau wote kujadili kwa kina mchakato wa katiba mpya kwa kuwa mchakato usipokuwa sahihi hata maoni mazuri yakitolewa yanaweza yasifikie hatua ya kufanyiwa kazi kwa ukamilifu na hatimaye kukosekana tija ambayo inakusudiwa kwa kuandikwa kwa katiba mpya miaka 50 baada ya uhuru.

  Bw. Mnyika alikumbusha kuwa mwaka 1991 chini ya uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi iliundwa tume ya kuhusu mfumo wa vyama Tanzania tume hiyo ilikuja na mapendekezo mengi ikiwemo la kutaka kuandikwa kwa katiba mpya, lakini serikali ilichukua machache ikiwemo la kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, hivyo mchakato unaotarajiwa kuanza sasa ungeshakamilika miaka mingi kama mapendekezo ya wakati ule yangetekelezwa kwa ukamilifu wake.

  Tukumbuke mwaka 1998 Rais Benjamin Mkapa aliunda Tume ya Marekebisho ya Katiba, hata hivyo sehemu kubwa ya mapendekezo ya Tume hayakutekelezwa. Na Rais wa wakati huo aliikataa hadharani sehemu kubwa ya taarifa yao na kutangaza kuwa tume imefanya kazi kinyume na hadidu rejea.

  "Wakati huo tume ilielezwa kuwa ilikwenda kinyume na maoni ya wananchi lakini kimsingi ni kwamba mapendekezo ya tume yalikwenda tofauti na misimamo ya serikali, hivyo ni lazima kujipanga katika kutekeleza suala hili, alisisitiza.

  Alisema kutokana na mazingira hayo ni muhimu kwa mchakato wa sasa kufanyika kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na kuwekewa utaratibu bayana ikiwemo kuitaka tume yoyote itayoundwa kutumia mfumo wa 'Green Paper' ili wananchi wenyewe kuanza kutoa maoni yao kuhusu masuala wanayoyaona kipaumbele badala ya kuathiriwa kimsimamo na serikali au tume yenyewe.

  Alisema kuwa pamoja na Rais Kikwete kuweka bayana kuwa tume anayoiunda itahusisha wadau, hata hivyo ni muhimu tume ikaundwa katika mfumo ambao ni shirikishi, sio tu wajumbe kuteuliwa kutoka sekta au kada fulani, bali pia kuwe na mashauriano kati ya kada au sekta husika kabla ya uteuzi ili kuwe na uwakilishi badala ya wahusika kujiwakilisha wenyewe au kumwakilisha aliyewateua.

  Bw. Mnyika alisema kuwa anatambua tofauti aliyoionesha Rais Kikwete kwenye jambo hili kwa kutambua haja ya katiba mpya kinyume na kauli za watendaji wake ndani ya serikali, zikiwemo za Waziri Celina Kombani, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadaye Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema ambao wote walitaka marekebisho ya katiba kwa kuwekwa viraka mbalimbali.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Mwanzo mzuri Mnyika.........endelea hivyo hivyo kuwa karibu na wananchi...usije ukawa kama CCM ambao walilibeza wazo la katiba mpya na hata hawakuliweka kwenye Ilani yao ya Uchaguzi na sasa wanajikuta..................they are out of touch and out of place....................Keep it up boy.....................................
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya tume mimi hata siyaamini,serikali zote zilizoshka madaraka hapa nchini ziliwah kuunda tume,lakini sijawai kuona matokeo chanya,hebu angalia kulikua na tume ya nyalali,tume ya jaji kisanga na miji2me mingne lukuki,TUMELISM ZMENICHOSHA,MZGO WA KATIBA WADONDOSHEWE WANANCH
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amefanya vema kusubiri kidogo. Retreating is not a surrender.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mnyika kume hata wewe ghiliba za Jk umeshindwa kuzing'amua.......................Hakuna tofauti yoyote kati ya JK na Werema au Kombani.........they are birds of a feather........................

  Werema na Kombani wanataka viraka kwenye katiba na JK ametekeleza azma hiyo kwa kujiundia katuem kake ambako katawajibika kwake mwenyewe na wala siyo kuajibika Bungeni...........................Na hii ndiyo kasoro kubwa ambayo Mnyika bado hajaiona.........................nayo ni tatizo kubwa la utawala bora nchini ni viongozi serikalini hawawajibiki Bungeni wala kwa wapigakura................Bunge wanalidhoofisha kwa kuliingilia majukumu yake kama haya ya kutunga sheria.....................na wanalipooza bunge kwa kuwapa baadhi ya wabunge vyeo serikalini..................i.e grand corruption........................

  Wapigakura hawasikilizwi matakwa yao kwa kuitumia NEC na TISS katika kuchakachua kura zao na mahakama pia hutumiwa kubeza hoja halali za wapigakurakama tulivyoona kwenye suala la mgombea binafsi...............................

  Ushauri wangu kwa Mnyika ni kuikataa Tume ya JK kwa sababu haina nguvu ya kisheria na kazi ya kutnga sheria ni ya Bunge na wala siyo ya Ikulu kama JK anavyojaribu kucheza rafu hizi za wazi wazi............................Bunge lisikubali kushushiwa hadhi yake kwa kunyanganywa majukumu yake haya ya kutunga sheria na katiba tena ndiyo sheria kuu..........................

  Bunge inabidi litunge sheria ya kuanzishwa mchakato wa kuitunga upya katiba yetu.........................

  1) Uwepo Mkutano wa kikatiba ambao utaratibiwa na Tume ya wataalamu ambao upatikanaji wake ni kupitia usaili wa wazi na utakaosimamaiwa na Kamati ya Bunge ya sheria na katiba.........Raisi kazi yake ni kuthibitisha tu majina hayo ambayo yatakuwa yamepata baraka zote za Bunge..................................

  2) Mapendekezo ya Mkutano wa kikatiba yapelekwe ndani ya mwaka mmoja kwa Mwanansheria MKuu ambaye atachapisjhwa muswada wa kupeleka Bungeni........................

  3) Baada ya Bunge kuupitisha....................wapigakura waote wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni....................Hii ina maanisha tunahitaji Bunge liunde sheria ya kura ya maoni ambayo serikali ya Muungano haina................................Tangu tupate Uhuru hatujawahi lupiga kura ya maoni......yaani hii ni aibu kwa taifa hili.........................

  4) Iwepo Tume ya kusimamia utekelezaji wa Katiba Mpya ambayo upatikanaji wake ni ule ule ambao Kamati ya wataalamu itakuwa ilipatikana......yaani uwepo uwazi siyo mtu mmoja anatuchaguliwa watu wake awatakao yeye kinyume na sheria ya ajira serikalini................
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani JMK alitangaza kuunda tume ya kuandika katiba? Wacha kuchakuwa!
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hako Ka Mnyika kalitaka umaarufu kupitia hiyo hoja? Hajui anapoamka yeye wenzake walilala zamaaani.

  Siasa si lelemama, ultimate ya siasa na satisfaction ni kufikia alipofikia JMK, nani juu yake Tanzania?

  Hapo ndipo utajuwa gap iko wapi! Haka ka-Mnyika haka!
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Out of touch? Out of place? Kwa ajili kanisa haliwataki au hujasikia ya Sumbawanga? Duhh! Wengine, wengi ya wa Tanzania ndio Rais wetu huyo na ndie tuliemchaguwa kwa kura nyingi kuliko alieshika hata namba mbili, alimuacha mbaaaaaali. Sasa, hamuitaki hiyo tume? Hamna sera? Au sera ni kupinga tu, hata jema kwenu si jema.

  Ahsante JMK kwa hotuba yako nzuri ya funga Mwaka na funga midomo.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe Kikwete kwa kujitokeza kwake kufanya kazi ambayo TANGU MIAKA YOTE HANA IMANI NAYO (Kuandikwa Upya kwa Katiba yetu) na kwamba wala hamna kikao chochote cha CCM kilichojadili na kumtuma akafanye kazi hiyo, mpaka hapo tu MPANGO HATARI WA ULAGHAI WAKE KWA UMMA WA TANZANIA tayari umechangia kufadhili na kuongezea ari zaidi ANZMA YA NGUVU YA UMMA kuhakikisha kwamba wanawapa MAELEKEZO MAALUM KILA MBUNGE wa taifa hili kuweka taifa mbele na KUAIBISHA MAFISADI kwa kupitisha kwa kauli moja Hoja Binafsi ya Mhe Mnyika kule Bungeni Dodoma kuanzisha mchakato kupitia vikao rasmi na wala si kupitia chumbani kwake Mhe Kikwete Ikulu.

  Kwa kweli inabidi kumpongeza Mhe Kikwete na ghiliba yake hatari kwa ustawi wa umoja wa kitaifa kwa jinsi ilivyosadia KUAMSHA ZAIDI SHAUKU YA WANANCHI KUTAKA KUJUA KILA MBUNGE JINSI atakavyoshiriki hoja ya Mnyika kama njia sahihi ya kuja KUTOA DIRA MBUNGE YUPI WA KUJA KURUDISHWA BUNGENI 2015 na yupi ni Mbunge wa MAFISADI wa kupiga chini wakati wa uchaguzi ujao.
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180


  Bwana Ruta, hapa umenielimisha sana na sasa nimejua haki yangu kitaalamu zaidi japo tangu siku JK alipotutolea wazo la kuunda tume, mimi binafsi nilikataa na niliwashawishi wenzangu wengi kwamba ni lazima watanzania tupinge kuburuzwa tena na huyu dikteta wa kikwere.


  Ametufanyia udikteta kwenye kura ZETU HALALI.kWA HILI TUSIKUBALI KAMA NI BARABARANI TUINGIE KWA AMANI.Ruta umenifungua macho hasa hapa:"Ushauri wangu kwa Mnyika ni kuikataa Tume ya JK kwa sababu haina nguvu ya kisheria na kazi ya kutnga sheria ni ya Bunge na wala siyo ya Ikulu kama JK anavyojaribu kucheza rafu hizi za wazi wazi............................Bunge lisikubali kushushiwa hadhi yake kwa kunyanganywa majukumu yake haya ya kutunga sheria na katiba tena ndiyo sheria kuu.............."

  WATANZANIA TUKATAE YA KIKWETE ENOUGH IS ENOUGH.

  MNYIKA zingatia ushaueri wa Ruta kwamba:Tume ya JK kwa sababu haina nguvu ya kisheria na kazi ya kutnga sheria ni ya Bunge na wala siyo ya Ikulu kama JK anavyojaribu kucheza rafu hizi za wazi wazi............................Bunge lisikubali kushushiwa hadhi yake kwa kunyanganywa majukumu yake haya ya kutunga sheria na katiba tena ndiyo sheria kuu..........................


  1. [*]

   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pumba zingine bwana!
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mh.Mnyika please come forward uteleze una msimamo gani baada ya kusoma maoni ya wadau hapa JF ninaamini utakuwa umepata jipya zaidi
   
 15. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hoja ya Mnyika haijavurugwa kwani sio sahihi Rais kuunda tume ya Katiba!
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Rais hajaunda tume ya kuunda katiba, au hamjasikia alichoongea?
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Jan 3, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..Spika Makinda, na wabunge wa CCM, wasingeruhusu hoja ya Mnyika ijadiliwe bungeni.

  ..nampongeza John Mnyika kwa kuona mbali.
   
 18. T

  Tom JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania hii tumeona tume nyingi zilizowahi undwa chini ya URAISI wa CCM na hakuna tume ilowahi fanya kazi kwa maslahi ya walalahoi.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nasi twayajua.
   
Loading...