Hoja ya bibi imenimaliza, haijibiki

Hoja ya bibi imenimaliza, haijibiki

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,966
WanaJF, mwaka huu nimedhamilia kuweka kitu ndani, majiko ya kuazima yamenichosha, katika kampeni zangu za mwaka huu nimeamua kuanza kuwaandaa ndugu zangu juu ya ujio wa jiko la kisasa, jiko la mjeremani, siyo haya ya mchina. Kampeni yangu imeanzia kwa Bibi yangu ambaye kwa kweli ni moja ya watu muhimu kabisa katika maisha yangu na mtu aliyekata tamaa juu ya hatima yangu ya kuoa, nilipoonana naye nikamweleza kisha nikamwaga sifa juu ya hili jiko jipya la mjeremani, alichoniuliza ni hiki, umewahi kuniletea wengine ukawamwagia sifa lakini baadae ukaja kusema siyo, huyu naye si yatakuwa hayo hayo? Niliinamisha kichwa tu nisipate cha kujibu, kwa kuchechemea sana nikajibu, kwa kulinganisha na hao wa nyuma huyu naona ni bora zaidi.
 
Hakikisha una gas/mafuta ya kutosha ili hilo jiko liwe linawaka.
 
Jiko la mje remain n zuri sana, tatizo maintainance fee yake n kubwa sana, mwambie bb yako , utajitahidi kadr ya uwezo wako kulitunza ili liweze kupika chakula kitamu like Siku mpaka na watoto wako wane walitumie na wakiwa wanajua ubora wake.

All the best
 
ah...angalia mengine yana ripuka hovyo....
 
Ana maanisha mke kama nimemuelewa vzur hahha

kwani unadhani hajaelewa? au na wewe hujamwelewa majiko ya mlimani city anayoyaongelea? tembelea samaki samaki utayaona.
 
Jiko la mje remain n zuri sana, tatizo maintainance fee yake n kubwa sana, mwambie bb yako , utajitahidi kadr ya uwezo wako kulitunza ili liweze kupika chakula kitamu like Siku mpaka na watoto wako wane walitumie na wakiwa wanajua ubora wake.

All the best

asante mkuu, ila hata hayana maintanace fee kubwa, yapo imara sana, ni kuchochea mkaa, gas au mafuta tu.
 
lisije tu likakuunguza[/QUOTE\]
jiko lolote linaunguza mkuu usipokuwa makini, bora uunguzwe na jiko la mjeremani si la mchina maana la mchina laweza kukulipukia hata usoni.
 
best wishes jiko ni jiko tu wewe na utunzaji wako na matumiz yako.....

bibi kagundua kitu usipokuwa makin hta hilo la mjeru litakushinda
 
lisije tu likakuunguza[/QUOTE\]
jiko lolote linaunguza mkuu usipokuwa makini, bora uunguzwe na jiko la mjeremani si la mchina maana la mchina laweza kukulipukia hata usoni.

mimi namshauri atafute na mchina wa kupiga support pembeni akiwekeza sana kwenye jiko la mjeremani atakuja kulia
 
Kuna uwezekano wewe si mpishi mzuri ndio maana bibi JEKI kawa na wasiwasi kidogo...

Jiko lafaa nini kama mpishi hana mapenzi na upishi au kujipikilisha!!!
 
Last edited by a moderator:
best wishes jiko ni jiko tu wewe na utunzaji wako na matumiz yako.....

bibi kagundua kitu usipokuwa makin hta hilo la mjeru litakushinda

Nitajitahidi dada yangu, ila uangalifu katika kuchagua jiko ni muhimu, haya ya mchina kila mara yanahitaji kupigwa JEKI.
 
Back
Top Bottom