Wakati Mataifa Yaliyoendelea yakiwa kwenye mchakato wa kupunguza viwanda nchini mwao Kutokana na Madhara yatokanayo kuwa makubwa!
Sisi Tanzania ndio kwanza tunaongeza sera kuwa na utitiri wa viwanda kila kona nchini pasipo kuzingatia athari!
Watanzania wengi hatupendi kuchunguza athari katika kuliletea taifa maendeleo!
Ukiuliza "Serikali ya viwanda inafaida gani kwa inchi na wananchi?
Utajibiwa majibu mepesi tu kwamba " Watanzania tupende vya kwetu"
Nchi zilizoendelea ikiwemo marekani Wanahaha kupunguza Idadi ya viwanda angalau kwa 80% ili kuondoa athari ya uchafuzi wa mazingira jambo ambalo linachukua bajeti kubwa kupambana nalo!
Je; Kuna faida ya kuwa na Viwanda Tanzania?
Uanzishwaji wa viwanda hapa kwetu umejaa utapeli, hauna tija kwa wananchi wala kwa nchi?
Mfano;
Kiwanda cha TAILIZI (Malumalu) cha chalinze kinauza Tailz bei kubwa kuliko kununua za South Afrika au Thailand
JE; Hiyo sera ya viwanda yanini sasa kama mwananchi hafaidiki?
SI BORA TUNGEWEKEZA KWENYE ELIMU NA KATIBA MPYA BASI?
Mataifa makubwa yenyewe sahivi yanavidampo viwanda Afrika kutokana na uchafuzi wa mazingira kwao;
Sisi tunataka kila uchochoro kuwe na kiwanda, tena viwanda vyetu ni sawa na viwanda Bubu!
TUTACHELEWA SANA

- Bidhaa nyingi zitokanazo na viwanda vyetu hapa bongo Zinauzwa bei juu sana kuliko hata kuagizia Malaysia ...Je faida ya kuwa na kiwanda iko wapi?
- Wananchi wanaoajiliwa kwenye viwanda bongo wengi wao huchukuliwa vibarua na mwisho wao hudhulumiwa.. hapo faida iko wapi?
- Bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vyetu nyingi zimechakachuliwa i.e kama ni nondo unene na urefu ni pungufu, bomba ni pungufu,misumari ni laini yaani kila kitu kimechakachuliwa
- Viwanda vyetu kwa wingi havijulikani hata majina, Zunguka maeneo mengi ya viwanda vingi havina hata mabango kuonesha vinazalisha nini, Lakini pamoja na hayo utaduaa zaidi kiwanda kama hiko unaambiwa kilifunguliwa na mbio za mwenge au kiongozi
- Viwanda vingi bongo Vinasajiliwa kwa kutengeneza Bidhaa flani, Lakini humo humo wanazalisha Bidhaa mbalimbali na TBS wanaidhinisha!
- Kutokana na uchafuzi wa mazingira, Sera za mwalimu nyerere walishauri Angalau kiwanda kiwe na eneo kubwa lenye uoto wa asili (pori) lisilopungua 5 heka hii yote ilikuwa lengo ni kulinda mazingira yasiathiliwe na utitiri wa viwanda
- Mfano; Mkoa wa pwani unasakiwa kuwa na viwanda zaidi ya 300, kwa DSM kinondoni viwanda ni karibu 200, Ilala viwanda kibao, temeke chungu mzima, Kigamboni plan inadaiwa kuwa na viwanda zaidi ya 200 Lakini Je, Kuna Hatua gani za kunusuru mazingira kwa faida ya wananchi? JIBU NI HAKUNA!
Kiwanda cha TAILIZI (Malumalu) cha chalinze kinauza Tailz bei kubwa kuliko kununua za South Afrika au Thailand
JE; Hiyo sera ya viwanda yanini sasa kama mwananchi hafaidiki?
- Hiyo Sera ya viwanda yanini kwasasa kama kuna ukwepaji kulipa kodi kwa viwanda?
- Hiyo Sera ya viwanda yanini kuwekeza viwanda karibu na makazi ya watu?
- Hiyo Sera ya viwanda yanini kama hakuna Umeme wa kutosha?
- Hiyo Sera ya viwanda yanini kama haitoi ajira kwa wananchi?