Hoja nyepesi za mgombea wangu wa chama changu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja nyepesi za mgombea wangu wa chama changu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kabewa, Aug 28, 2010.

 1. Kabewa

  Kabewa Member

  #1
  Aug 28, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Kwa bahati mbaya chama changu kimekuja na hoja nyepesi sana hoja ambazo hazipo kwenye ilani bali zinatoka kwenye vichwa vya wagombea wa chama changu kiasi ambacho naamini baada ya kutoka kumwaga sera hizo huwa wanasahau walichokiahidi mahali hapo.nashidwa kuamnini kwamba baada ya mgombea wangu kumwaga sera hizo ataweza kuzitekeleza kwa kipindi cha miaka hii mitano iwapo atashinda nadiriki kusema ni kampeni ahadi.naamini tena baada ya kuisha kwa miaka mitano atasema niliahidi sikumaliza tupeni tena miaka 5 tumalizie yale tuliyoahidi. Hizi propaganda nazikataa naomba mambo anayoahidi mgombea wangu yawe yale yaliyoko kwenye ilani na ataoe ahadi atakazo zitimiza kwa muda huo wa miaka mitano kama atachaguliwa.na atoe na ufafanuzi endapo litatokea tatizo litakalo sababisha kukwama kwa sera zake atalikabili vipi kwa kipindi hicho ili kuepuka kutotimiza ahadi zake . I mean aweke ulizi wa hoja ya ahadi zake ili azitimize.sio anaahidi huku akisema marekani watanisaidia ? Wakigoma si ndo umetuuza ??????? Maana kuomba kuna kupata na kukosa
   
Loading...