Hoja ni msongamano au aina ya msongamano?

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Asalam-aleikoum Wana-JF!

Swali hili linahusu tangazo la serikali kuhusu tangazo la Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kupiga marufuku biashara barabarani ambazo ni kinyume na kanuni za town planning.

Tangazo la serikali linajaribu 'kufafanua' amri ya Mkurugenzi kwa wahusika ambao inaonekana kwamba wamepatwa na taharuki na sintofahamu ya maisha yao wakiondolewa kwenye maeneo hayo.

Lakini tangazo la pili linalo 'trend' redioni sasa kwamba vibanda vya kudumu haviruhusiwi ila vijimeza vinavyohamishika ndiyo vinaruhusiwa; kimsingi linaongeza mkanganyiko badala ya kutatua tatizo la MSONGAMANO.

1. Kwanza kutokana na tangazo la kwanza na la pili la ufafanuzi; utekelezaji wa yote haya mawili haupunguzi idadi ya wafanyabiashara kwenye maeneo hayo bali unawataka kujipanga upya tu. Kwahiyo kama watu ni walewale na eneo ni lilelie misongamano utapunguaje?

2. Kubadili 'umbo' toka vibanda vya kudumu kwenda vijimeza vinavyohamishika kunatatuaje tatizo la MSONGAMANO?
3. Kimsingi maagizo yote mawili yanaweza kuongeza msongamano badala ya kupunguza. Kwasababu:

A. Tatizo la MSONGAMANO wa wafanyabiashara mijini ni la kitaifa. Kwahiyo haliwezi kuondolewa kwa amri ya Mkurugenzi wa mji mmoja nchini au kwa agizo la waziri au mamlaka yoyote ya dola bila kusababisha mgogoro mkubwa katika jamii nzima ya Watanzania.

B. Tatizo la MSONGAMANO wa wafanyabiashara ni la kisiasa.

Kitambulisho cha mfanyabiashara au mjasiriamali kina hadhi kubwa kuliko passport hapa nchini kwasababu kiliasisiwa na Mkuu wa Nchi ambaye alimpa mhusika ruksa ya kufanya biashara "POPOTE" nchini!

Tukumbuke kwamba tamko la rais ni sheria. Kwahiyo hili neno 'POPOTE' halifutiki kwa agizo au tangazo la kiongozi au mamlaka chini ya rais. Na ndilo limekuwa mkuki kwa yeyote atakayewagusa watu hawa ambao idadi yao ni kubwa na inaongezeka kila siku.

C. Ingawa wakubwa hawatakubali kwamba "ufunguo wa tatizo" hili sio jawabu, kama 2+2=4; bali utatokana na mchakato na hatua kadhaa katika vyombo/taasisi mbalimbali husika. Wataalamu wa town planning na wa fani nyingine watanielewa.

Nimeshasema mahali pengine humu na narudia hapa tena:

Hili ni zimwi lillilopaswa kufungiwa kwenye chupa na kutupwa baharini. CCM wakalifungulia kwa madhumuni ya kisiasa. Lakini JPM akaenda mbali zaidi akalitoa ndani ya chupa na kuliweka 'SEBULENI' kwao.

Na hili ni moja ya mambo kadhaa yanayolikabili taifa letu awamu hii, yanayohitaji ufumbuzi. Tukiendelea na MFUMO TULIONAO wa kisiasa na utawala, hakika tutazidi kutopea kwenye vurugu.
 
Roho mbaya za chadema zishindwe na kulegea
20210514_130602.jpg
 
Back
Top Bottom