Mjenda Chilo
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 1,472
- 527
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"
CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.
Ni kweli?
Komba for president!! LoL
This might be out of topic ila hapo kwenye red umeongea kinyume chake...Mzee Mwanakijiji,
Sintopendekeza mtu isipokuwa kwa manufaa ya taifa na japokuwa Membe ni kichwa, muweza ukiachana na habari za Ufisadi wake maana huko CCM hakuna msafi kihivyo. Wayahudi walilaaniwa tena na Mungu mwenyewe lakini bado wanaitawala dunia.
Hivyo pamoja na utetezi wako bado nakuhakikishia kwamba CCM wataweza tu kushindana ikiwa watamsimamisha Asha Rose Migiro na hii itatokana na WANAWAKE kutumia kauli mbiu ya TUKIWEZESHWA TUNAWEZA. Itakuwa sio swala la chama bali wanawake against the rest...Na amini maneno yangu watu hawatatazama tena nyuma wala kutazama uwezo wa AshaRose isipokuwa ni mageuzi ambayo kwao yatawalemaza akili..
Kwa upande wa ushindani na hasa Chadema wanatakiwa kuanza mapema sana kumtafuta na kumwandaa mgombea japo kwa siri lakini nawatahadharisha mapema - KAZI IPO 2015 wajipange mapema na vizuri sana laa sivyo itakuwa aibu maana elimu ya Uraia haijazama vichwani mwa wananchi hivyo SHIDA na MATATIZO yanatangulia Mapenzi yao..
duuuh mkuu nahisi umekosa topic ya kupost kumsimamisha membe itakuwa bora hata arudi white hair
NI vizuri watu wakasoma actually nimeandika nini... maana wengine wanachangia wakidhania kuwa nimeandika nini.
NI vizuri watu wakasoma actually nimeandika nini... maana wengine wanachangia wakidhania kuwa nimeandika nini.
ulichokiandika ndicho kinachochangiwa acha kuikana post yako,,,,,,
Kaka mara hii umeishakachuliwa hadi kuwa kuwadi wa mafisadi kama si nepi yao? Huyo Membe amekupa nini hadi umzimie na kumuabudia hivyo ndugu yangu? Kweli adui yako muombee njaa na penye udhia penyeza rupia. Yaani mihemko yako yote ya miaka yote umeishia hapo? Kwanini siku hizi watu wanashabikia uchanguuu hadi kwenye mawazo yarabi? Heri ungenyamaza kuliko kuvua nguo mtoni usijue kuna watu. Heri kuamini kwenye unachohubiri hata watu wakakucheka kuliko kuramba matapishi yako. Pole sana bwana mdogo. Je huduma yako unauza bei gani?
Ushahidi gani unataka wakati yeye mwenyewe yupo?. He is who he is!unamaanisha nini kuwa KICHWA,,,,,
USHAHIDI????
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa sasa kukubali ukweli halisi kuwa determinant factor ya ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, lies with mgombea wa CCM na ndio maana mimi siku zote nimempigania EL!, na nikasema wazi, kama sio yeye then ni Membe!.Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"
CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.
Ni kweli?
Mkuu wangu katika hili kusema kweli nitatofautiana na wewe..Nitarudia kusema kwamba Wadanganyika bado kabisa hawajaelimika ktk elimu ya Uraia na siku zinakwisha..Na uloyasema hapo juu kwao ni miujiza ya Mussa kwa sababu wana njaa, wana shida na meli yetu inazama hivyo kila mtu leo yupo ktk kupoteza maisha kama asipopata boya ya kuelea. Hivyo sii rahisi kuupata UMOJA ktk hali hii na pengine sii rahisi pia kumpata rais unayemzungumzia..Sidhani kuwa CCM inachukiwa kwasababu ya Rais fulani, kinyume chake Rais amebaki kuwa anapendwa na CCM inachukiwa.Chuki dhidi ya CCM si kutokana na watu au haiba zao, si kutokana na sera, ni kutokana na mfumo uliokiuka maana nzima ya chama, kanuni, taratibu na sheria n.k.
Chuki dhidi ya CCM ni kutokana na chama kupoteza umiliki wa wananchi kwa kundi dogo lenye nia tofauti na ile ya CCM.
Uchaguzi wa 2015 hautaongozwa na sura au kashfa za mtu mmoja mmoja. Utaongozwa na dira ya kitaifa na mtazamo.
Kikubwa zaidi ni kuchoshwa kwa wananchi na kundi teule kuiweka nchi ilipo kwa miaka 50.
Hakuna kiongozi aliye ndani ya CCM au serikali yake anayeweza kuja na hadithi tofauti.
Membe kama walivyo wengine hajaweza kusimama katika masilahi ya taifa.
Hajakwepa kashfa kwasababu anaposhindwa kuueleza umma nini kimetokea kwa kujificha nyuma ya bunge na serikali hana maadili, uthubutu au utashi wa kisiasa.
Lakini hatuhitaji kiongozi wa uchumi na siasa tu, tunahitaji kiongozi atakayewaunganisha Watanzania na kurudisha Tanzania isiyo na makundi ya kikabila au kidini. Membe ameshindwa mtihani huo kwa kuanzia.
Naamini kuwa ili CCM ijirudishie hadhi ni lazima mgombea wa 2015 atoke nje ya 'system' iliyopo.
Na sidhani kuwa ni suala la nani atakuwa rais, bali chama gani kinaweza kututoa hapa tulipo!