Hoja marudio ya kufungia mwaka kwenu makamanda

Hoja marudio ya kufungia mwaka kwenu makamanda

images.jpeg-1.jpg
 
Basi huelewi ulichokiandika.

Au Masha kavunja sheria gani??

Sent using Jamii Forums mobile app

Teh teh teh

Wewe ndo huelewi unachokisoma.

Hakuna mahala nimesema Masha kavunja sheria.

Lakini, kama papo, niwekee nukuu yake hapa.

Sawa? Umeelewa hiki nilichokiandika hapa?

Teh teh teh...umenifanya nicheke kwa sauti aisee.
 
Nyani ngabu anatafuta u dc, eeh jiwe la chato mhurumie muhitaji ngabu,
Lumumba wote semeni ameeen😁😁😁
 
Chama tawala kinaweza kuwa na mapungufu yake mengi tu, lakini nadiriki kusema bado hatujawa na mbadala. Tuache mihemko na ushabiki usio na tija. Ni kweli sifurahishwi na baadhi ya mambo yanayoendelea japo mengi yanaenda vizuri isipokua kuna marekebisho machache yanahitajika.

Tulipofikia, tulihitaji mtu wa kaliba ya JPM kushtua na kurudisha heshima ya serikali. Niliwahi kusema awali tunahitaji aina flani ya udikteta, sitatengua hiyo kauli kwa sababu nilimaanisha.

Upinzani kuna wakati unajenga hoja kizembe na kwenye vitu visivyo na msingi kiasi cha kutilia shaka kama kweli nia na adhma yao ni kushika dola siku moja.

Kuna kipindi nashawishika kusema kuendelea kuwa upinzani kuna watu wanafaidika Zaidi kuliko hata wakishika mamlaka.
 
Teh teh teh

Wewe ndo huelewi unachokisoma.

Hakuna mahala nimesema Masha kavunja sheria.

Lakini, kama papo, niwekee nukuu yake hapa.

Sawa? Umeelewa hiki nilichokiandika hapa?

Teh teh teh...umenifanya nicheke kwa sauti aisee.

Sasa kwanini umeunganisha Masha na wavunja sheria unasema Mzee baba anawashughulikia??

Kama Masha Hana kosa kwanini fastjet ihujumiwe?? Huoni Kama Lisu alisema kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee hiyo picha imenichekesha saaaana!
Tungekuwa na vyombo vya habari vya kipelelezi nadhani ingekuwa vizuri vikawatafuta kwa sasa na kuwauliza maoni yao baada ya miaka mitatu kuhusiana na kitendo walichokifanya!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni asubuhi nyingine tena pande hizi. Wengi wetu tumelala salama na kuamka salama. Natumai hii siku ya mkesha wa 2019 itawaendea vizuri ili muweze kuukaribisha mwaka mpya inavyostahili.

Sasa bana, hii hoja nilishawahi kuizungumzia huko nyuma. Ila kwa takriban wiki mbili au tatu hizi zilizopita, naona maudhui yake yanajirudia rudia hususan kwenye lile sakata la kufungiwa kwa muda kampuni ya usafiri wa ndege ya Fastjet.

Kwa sasa inasemekana yule waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Masha, ndiye mwenye wingi wa hisa kwenye umiliki wa hiyo kampuni.

Inajulikana wazi kuwa jamaa ni mwanaCCM licha ya kuchepuka kidogo hapo katikati na kwenda kuchezea mchanga kwa wale wachezea mchanga wa CHADEMA kule Ufipa.

Baadaye aliamua kurudi nyumbani CCM.

Sasa hii majuzi baada ya hiyo kampuni yake kuzuiwa kufanya shughuli zake na serikali, CHADEMA wakaanza tena kuirudia ‘talking point’ yao.

‘Talking point’ yenyewe nadhani ilitoka kwa kamanda wao Tundu Lisu hapo kipindi cha nyuma ambapo alisema kwamba Rais Magufuli atapomaliza kuwashughulikia wapinzani, atahamia kwa hao hao CCM wenzake.

Hiyo ni kauli ya kipumbavu kabisa.

Kwa nini ni ya kipumbavu? Kwa sababu, kama lijitu linavunja sheria, linakiuka taratibu na masharti, hao CHADEMA sijui wangependa kuona halichukuliwi hatua kisa tu na lenyewe ni liCCm?

Hawa makamanda sijui walitaka hizo ndege za Fastjet ziendelee tu kufanya shughuli zake hata kama zimekiuka masharti na taratibu kisa tu mwenye hisa nyingi kwenye hiyo kampuni ni mwanaCCM?
Wao badala ya kupongeza hilo jambo, eti wao wanaligeuza na kuwa suala la ‘see, we told you so’.

Kwa maana nyingine ni kwamba, hawa makamanda wao wanataka mtu akiwa ni wa CCM, kama kavunja sheria, basi asiadhibiwe na mwanaCCM mwenzake kwa sababu wote ni wa chama kimoja!

Sawa, nakubali kuwa kuna nyakati haki huwa haitendeki kwa usawa ambao tungependa kuuona. Lakini, inapotokea haki imetendeka bila kuangalia wala kuzingatia rangi za mtu za chama, sote twapaswa kutoa pongezi maana hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa. Siyo kuanza kuponda na kupiga siasa za majitaka na za bei rahisi.

Mpaka wakati mwingine najiuliza; ina maana hawa makamanda wao wakishika dola, kamanda mwenzao akiharibu, hawatomshughulikia kwa vile tu ni kamanda mwenzao??

Makamanda mnakera sana. Na nashukuru mko huko beach kidimbwi mnachezea mchanga. Bakini huko huko. Ikulu panawapwaya.

Heri ya mwaka mpya,

[emoji1536]
Inagawa ubajitahidi kuandika hoja zako zinanishawishi kuwa shule yako ni ndogo sana

Hoja ya lisshu iljikita kwenye kuminya haki za watu na kuonea
 
Kuna kipindi nashawishika kusema kuendelea kuwa upinzani kuna watu wanafaidika Zaidi kuliko hata wakishika mamlaka.
Naomba nichangie kuhusiana na hii paragraph ya hoja yako
"Kuna kipindi nashawishika kusema kuendelea kuwa upinzani kuna watu wanafaidika Zaidi kuliko hata wakishika mamlaka."

Sio kwamba wanafaidika tu bali pia wanajua kuwa hawana uwezo wa kupata ridhaa ya kupewa Ikulu.

Nguvu zao zote zinaishia kwenye ubunge. Kwao kupewa Ikulu
Ni kama bonuses za kisiasa.
 
Inagawa ubajitahidi kuandika hoja zako zinanishawishi kuwa shule yako ni ndogo sana

Hoja ya lisshu iljikita kwenye kuminya haki za watu na kuonea

Ni kweli. Shule yangu ni ndogo sana. Kwa hilo hujakosea.
 
Kwa sasa wamesahau kuwa walituambia Edward Lowassa ni Rais wa mioyo yao.

Wiki mbili zilizopita walihamia kwa Membe na kuanza kusema ni Rais wao ajaye.

Juzi wamehamia kwa Lissu baada ya kusahau walichosema kuhusu Membe.

Ndio maana nimesema akili yao ni sawa na random access memory (RAM)
Nyie mlipongeza Sheria, kanuni ya kikotoo, juzi mpepongeza raisi wenu kuifuta kanani ya sheria
 
Back
Top Bottom