Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,339
- 144,836
Ni asubuhi nyingine tena pande hizi. Wengi wetu tumelala salama na kuamka salama. Natumai hii siku ya mkesha wa 2019 itawaendea vizuri ili muweze kuukaribisha mwaka mpya inavyostahili.
Sasa bana, hii hoja nilishawahi kuizungumzia huko nyuma. Ila kwa takriban wiki mbili au tatu hizi zilizopita, naona maudhui yake yanajirudia rudia hususan kwenye lile sakata la kufungiwa kwa muda kampuni ya usafiri wa ndege ya Fastjet.
Kwa sasa inasemekana yule waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Masha, ndiye mwenye wingi wa hisa kwenye umiliki wa hiyo kampuni.
Inajulikana wazi kuwa jamaa ni mwanaCCM licha ya kuchepuka kidogo hapo katikati na kwenda kuchezea mchanga kwa wale wachezea mchanga wa CHADEMA kule Ufipa.
Baadaye aliamua kurudi nyumbani CCM.
Sasa hii majuzi baada ya hiyo kampuni yake kuzuiwa kufanya shughuli zake na serikali, CHADEMA wakaanza tena kuirudia ‘talking point’ yao.
‘Talking point’ yenyewe nadhani ilitoka kwa kamanda wao Tundu Lisu hapo kipindi cha nyuma ambapo alisema kwamba Rais Magufuli atapomaliza kuwashughulikia wapinzani, atahamia kwa hao hao CCM wenzake.
Hiyo ni kauli ya kipumbavu kabisa.
Kwa nini ni ya kipumbavu? Kwa sababu, kama lijitu linavunja sheria, linakiuka taratibu na masharti, hao CHADEMA sijui wangependa kuona halichukuliwi hatua kisa tu na lenyewe ni liCCm?
Hawa makamanda sijui walitaka hizo ndege za Fastjet ziendelee tu kufanya shughuli zake hata kama zimekiuka masharti na taratibu kisa tu mwenye hisa nyingi kwenye hiyo kampuni ni mwanaCCM?
Wao badala ya kupongeza hilo jambo, eti wao wanaligeuza na kuwa suala la ‘see, we told you so’.
Kwa maana nyingine ni kwamba, hawa makamanda wao wanataka mtu akiwa ni wa CCM, kama kavunja sheria, basi asiadhibiwe na mwanaCCM mwenzake kwa sababu wote ni wa chama kimoja!
Sawa, nakubali kuwa kuna nyakati haki huwa haitendeki kwa usawa ambao tungependa kuuona. Lakini, inapotokea haki imetendeka bila kuangalia wala kuzingatia rangi za mtu za chama, sote twapaswa kutoa pongezi maana hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa. Siyo kuanza kuponda na kupiga siasa za majitaka na za bei rahisi.
Mpaka wakati mwingine najiuliza; ina maana hawa makamanda wao wakishika dola, kamanda mwenzao akiharibu, hawatomshughulikia kwa vile tu ni kamanda mwenzao??
Makamanda mnakera sana. Na nashukuru mko huko beach kidimbwi mnachezea mchanga. Bakini huko huko. Ikulu panawapwaya.
Heri ya mwaka mpya,
[emoji1536]