Hoja kuu ya CCM ya kuwasemea wapinzani kuwa na 'vurugu' yaanza kupuuzwa na wapiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja kuu ya CCM ya kuwasemea wapinzani kuwa na 'vurugu' yaanza kupuuzwa na wapiga kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Oct 5, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Uchaguzi wa Igunga imedhihgbirisha bila shaka yoyote kwamba hoja kuu ya CCM katika kampeni zake za kukisemea chama kingine kuwa ni cha “vurugu” inaanza kupitwa na wakati na polepole inatokomea mbali.

  Pamoja na kupandikiziwa kuwa CDM ni chama cha vurugu, wananchi wasikichague, bado CCM ndiyo ikajikuta inapoteza kura (ingawa si jimbo) na CDM kujilimbikizia kura.


  Ni kawaida kwa chama kinachopoteza mvuto kukazania hoja ya ‘vurugu’ baada ya kushindwa kuwaelezea wapiga kura kipi kimekuwa kinawafanyia, na mara moja hukimbilia wamekuwa wanasimamia ‘amani’ utadhani ‘amani’ inaweza ikafanywa kuwa ni sera ya chama fulani.

  Nani asiyetaka amanai? Na amani haiimbwi majukwaani, hujengwa kwa misingi imara ya haki na utawala bora, vitu ambavyo kwa CCM vimetoweka.

  Kwa hiyo ni bora CCM wakaachana na hoja yao hii ya jutaja “vurugu” kuwaponda wapinzani wake, imeanza kutokuwa na mshiko wowote, maana wananchi sasa wameanza kun’amua vurugu zinaanza vipi.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Yote hayo ni kuanza kuishiwa sera wanakimbilia 'vurugu.' Polepole hoja hiyo inaanza kuwa siyo tena dili kwao na sijui sasa watatafuta nini mbadala. La mwisho watakalofanya nadhani litakuwa lile la Kivuitu - kutumia ubabe kubadilisaha matokeo na potelea mbali nendeni mkauane huko mitaani.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu umenena, hata zile hoja za ukabila na udini naona zime bounce tena kwa kishindo, wananchi zaidi ya 23,000 walioipigia kura chadema pale igunga imeonyesha kwamba CDM inakubalika na yanayosemwa na sisiem ni fitina tupu
   
 4. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba Meli nyingine ipinduke kule Zanzibar itoweke na Wabunge kama watatu hivi wa kuchaguliwa ili tuanze mtanange mwingine huko Zenji, ndo watajua CDM ni chama cha kitaifa au la.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Samahani Ndugu - post yako ina mahusiano gani na mada? Bora ungeanzisha mada hiyo ya utaifa wa vyama ili ijadiliwe.
   
Loading...