Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Uchaguzi wa Igunga imedhihgbirisha bila shaka yoyote kwamba hoja kuu ya CCM katika kampeni zake za kukisemea chama kingine kuwa ni cha vurugu inaanza kupitwa na wakati na polepole inatokomea mbali.
Pamoja na kupandikiziwa kuwa CDM ni chama cha vurugu, wananchi wasikichague, bado CCM ndiyo ikajikuta inapoteza kura (ingawa si jimbo) na CDM kujilimbikizia kura.
Ni kawaida kwa chama kinachopoteza mvuto kukazania hoja ya vurugu baada ya kushindwa kuwaelezea wapiga kura kipi kimekuwa kinawafanyia, na mara moja hukimbilia wamekuwa wanasimamia amani utadhani amani inaweza ikafanywa kuwa ni sera ya chama fulani.
Nani asiyetaka amanai? Na amani haiimbwi majukwaani, hujengwa kwa misingi imara ya haki na utawala bora, vitu ambavyo kwa CCM vimetoweka.
Kwa hiyo ni bora CCM wakaachana na hoja yao hii ya jutaja vurugu kuwaponda wapinzani wake, imeanza kutokuwa na mshiko wowote, maana wananchi sasa wameanza kunamua vurugu zinaanza vipi.