Hoja kuu mbili kuhusu taarifa iliyosambazwa na ubalozi wa Marekani, Tanzania

Na, Ibrahim Haroub Geveva

Nikiwa katika shughuli za kikazi za Umoja wa Mataifa hapa Geneva, nimefadhaishwa na namna Ubalozi wa Marekani Tanzania ulivyotoa taarifa ya UZUSHI huko Tanzania.

Mwaka 1998, hao ndugu walipigwa na hawakutoa tahadhari yoyote Dar es Salaam wala Nairobi. Nakumbuka nilikuwa Sudan wakati huo katika shughuli za Kanda ya Mashariki ya UN.

Hakukuwa na taarifa zozote za tahadhari kama huu uzushi. Jiulize kwa nini leo wametoa, tena siku ya Bajeti ya Nchi inapojadiliwa, Siku ambazo Watalii wengi wanakwenda kwa makundi makubwa Tanzania, Kuna nini hapo kimefichika?

Nimemuuliza Mtoto wa Shemeji yangu anayefanya kazi Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, amethibitisha hata Ubalozi wenyewe umeshangazwa na aliyechapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii bila kujiridhisha.

Wanahojiana, hivi walishindwa hata kuwapatia Polisi Oysterbay wachunguze? Au hata wale walinzi wa pale FFU au G4S ambao wanalinda Ubalozi wao?

Walishindwa kuwapa JWTZ? Walishindwa kuwapa Usalama wa Taifa waseme wanayojua? Je huu sio ujasusi uliopindukia katika nchi za wenzao?

Hayo maswali lazima yawasukume Wamarekani kuwaomba radhi washirika wao katika masuala ya Kiusalama. Kuna Mikataba ya Kimataifa inayowataka kushirikiana na vyombo vya ndani ya nchi husika wanapofuatilia mambo yanayohusu masuala ya ndani ya nchi.

Wamarekani hadi wanatoa kauli, walituma wachunguzi wao Masaki?Je, waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania au hata Umoja wa Mataifa? Wanatumia njia gani kuchunguza mambo nchini Tanzania hadi kutoa kauli ya namna hiyo?

Nani amewathibitishia huko mitaani hizo taarifa hadi kuchapisha katika tovuti yao? Tujiulize sote haya maswali.

Hivi Balozi wa Tanzania nchini Marekani hata akiwa na taarifa yoyote ya nchi hiyo ndio atoke kwa umma pale Washington DC kutangaza anachojua kuhusu Marekani? Sisi watu wa Diplomasia tunahoji, hiyo ni diplomasia ya wapi?

Basi ukiona hivi kuna jambo wanatengeneza kwa makusudi, si vinginevyo. Watanzania AMKENI.

Marekani, waombeni RADHI Watanzania na lazima mjenge tabia ya kufanya kazi na vyombo vya dola vya Tanzania katika kazi zenu. Umoja wa Mataifa unafuatilia jambo hili kwa karibu

NINAKUBALIANA NA HOJA KWA ASILIMIA ZOTE. KIMSINGI HIZI NI HUJUMA DHIDI YA TANZANIA, KWA SABABU WANAZOZIJUA WAO, NA PIA KWA MASLAHI YAO.

SASA KATIKA MAZINGIRA YA JINSI HII, JE MAMLAKA YA
NCHI YETU INASEMAJE JUU YA UZUSHI HUU?? ; JE MAREKANI INAPATA WAPI UHALALI WA KUTOA TAARIFA NZITO KAMA HIZO BILA YA KUZIJULISHA MAMLAKA ZETU?; JE NININI KIFANYIKE DHIDI YAO??
 
Marekani wapo sahihi kutoa taarifa kama hii.Na sijaona nukuu yako ya msingi uliyoitoa.
Kosa si kosa bali kurudia kosa ni kosa.Kama hawakutoa taarifa mwaka 1998 inaweza kuwa ndio fundisho la la wao hadi wametoa sasa hivi.
Tukiacha ushabiki wa kipuuzi ukweli ni kwamba vyombo vyetu vya ulinzi ni dhaifu sana hasa katika swala la intelejensia.
Vyombo vyetu vimejikita kwenye kulinda utawala uliopo madarakani na si suala la usalama wa raia.

Ni mpuuzi pekee anaweza kuwaamini vyombo vyetu vya ulinzi hasa baada ya kutokea matukio ya hovyo ya hivi karibuni.

Vyombo vya ulinzi vikianza kuingilia Mambo ya siasa mara nyingi vinapoyeza sita na heshima kwa wananchi.

Ukiondoa tahadhari za kipuuzi wanazotoa kwenye kukataza mikutano ya kisiasa ya wapinzani ni lini walishawahi kutoa hivyo kwenye swala la usalama wa raia?

Dr Mwele malecela alitoa tahadhari ya ugonjwa wa Dengue kuwepo nchini mwishoni walimfanya nini?Na leo tunateseka kwa ugonjwa gani?

Vyombo vya ulinzi hasa intelejensia vinapaswa kurudi kwenye misingi ya uanzishwaji wake.

Pia tishio limeonekana linaweza kutokea maeneo ambayo wanapenda kutembelea watalii sehemu ambazo raia wao huwa wanatembelea kwa hivyo wapo sahihi kwa kigezo cha kulinda raia wao.

Kazi mojawapo ya balozi yeyote ile ni kulinda usalama na haki za raia wake waliopo mchini humo
 
TUJIKUMBUSHE ILIVYOKUWA KENYA, JAMAA WALITOA ONYO HIVI HIVI SERIKALI YA KENYA IKADHARAU THEN JAMAA WAKAPIGA WASTGATE JAMANI TUWE MAKINI INTELLIGENCIA YA MAREKENI NI KUBWA SANA ILA NINAVYOJUA MIMI WAMETOA ONYO KWA RAIA WAO WAISHIO TANZANIA KITU AMBACHO NI WAJIBU WAO
 
Kabla ya mashirikiano ya Afrika na mabara mengine kabla ya miaka ya nyuma mambo yalikuwa shwari,tukasema ngoja tuungane labda tunaweza pata nafuu sasa hali ndo imezidi kuwa mbaya zaidi.Wazungu ni wauni sana wanajifanya watabili wa matatizo kumbe wao ndo watengeneza matatizo
 
NINAKUBALIANA NA HOJA KWA ASILIMIA ZOTE. KIMSINGI HIZI NI HUJUMA DHIDI YA TANZANIA, KWA SABABU WANAZOZIJUA WAO, NA PIA KWA MASLAHI YAO.

SASA KATIKA MAZINGIRA YA JINSI HII, JE MAMLAKA YA
NCHI YETU INASEMAJE JUU YA UZUSHI HUU?? ; JE MAREKANI INAPATA WAPI UHALALI WA KUTOA TAARIFA NZITO KAMA HIZO BILA YA KUZIJULISHA MAMLAKA ZETU?; JE NININI KIFANYIKE DHIDI YAO??
WANAHAKI YA KUWAFANYA HIVYO KWA RAIA WAO SEHEMU YEYOTE ILE NENDA KASOME VIENA CONVENTION KUHUSU MAMBO YA DIPLOMATIC RELATIONS
NGOJA TUPIGWE NDIO TUJE HAPA KULALAMIKA KWAMBA UBALOZI WA MAREKANI WALITOA ANGALIZO
 
Mleta mada umefikaje fikaje huko UN kwa uelewa wako huu .
Wamarekani wamechapisha hizi taarifa kwa ajili ya wananchi wao na kwenye website yao.

Mambo sasa o wenu kasema alikuwa anazifahamu ila alikaa kimya, anasubiri watu wafe ndio waanze kutafuta mchawi.

Sasa wewe mzee wa UN geneva hapo unacholalamika ni nini?
 
Kosa walilofanya ni kitowataarifu vyombo vya usalama
Ila hizi siyo za kudharau hata kidogo

Kabla ya lile shambulio la mwisho kenya hawa jamaa walitoa tahadhari na watu walibeza humu
Lakini matokeo mliyaona

Hoja ya kwamba mwaka 98 wao walivamiwa haina maana
Kwa kuwa unaongelea zaidi ya miaka 20 iliyopita mambo yamebadilika sana Leo teknolojia imeshatembea sana
Huwenda wavamiaji wa kipindi hicho hawakutumia mtandao kwa kuwa haukuwa active kama Leo
Appointment zilifanyika face to face labda na mipango kufanyika mwisho wa siku tukio
Leo utaepuka vp mtandao?
 
Mkuu Rukia Mbonde,
Asante huu ndio uzalendo, pia asante kwa mzalendo Ibrahim Haroub wa Geveva
P
MKUU ACHA KUPOTOSHA HUO SIO UZALENDO NYIE NDIO MNAOPOTOSHA MAANA YA NENO UZALENDO.
HIVI IKITOKEA TUKIPIGWA KWELI KAMA ILIVVYOTOKEA WASTEGATE KENYA AMBAPO UBALOZI WA MAREKANI KENYA ULITOA ONYO NA LIKAPUZWA UTAKUJA KUSEMAJE.
SIONI MANTIKI YEYOTE YA KUSEMA ETI HUYO MTOA HOJA NI MZALENDO
KIMSINGI TUWE MAKINI ONYO LA UBALOZI WA MAREKANI TULICHUKULIE SERIOUS
 
Mleta mada umefikaje fikaje huko UN kwa uelewa wako huu .
Wamarekani wamechapisha hizi taarifa kwa ajili ya wananchi wao na kwenye website yao.

Siro wenu kasema alikuwa anazifahamu ila alikaa kimya, anasubiri watu wafe ndio waanze kutafuta mchawi.

Sasa wewe mzee wa UN geneva hapo unacholalamika ni nini?
YAANI HUYO JAMAA ANAYESEMA SIJUI YUPO GENEVA NI MSENGE NA **** SANA WATU WANATOA TAHADHARI KWA RAIA WAO AMBAO WAPO TANZANIA MANAKE STILL HATA KAMA WAPO TANZANIA WANAJUKUMU LA KUWAHUDUMIA RAIA WAO KAMA MOJA YA MAJUKUMU YA UBALOZI.
SISI KAMA NCHI INABIDI TUJIONGEZE TUKIKUMBUKA KILICHOTOKEA WASTGATE KENYA KABLA YA SHAMBULIO HILO UBALOZI WA MAREKANI KENYA WALITOA ONYO LA NAMNA HII NA SERIKALI YA KENYA ILIWAPUUDHA
 
Mleta mada mbona imekuumiza as if wewe ni mmojawapo wa walipuaji? tahadhari ni tahadhari tusianze kujadili kwa nini marekani watume bali tuchukue tahadhari hilo ndilo kubwa.
 
Kuna kitu kimoja muhimu sana hapa.

Hizi taarifa zilikuwa na msingi wa ukweli au hazikuwa na msingi huo?

Kama zina msingi wa ukweli, Wamarekani wana wajibu wa kuwataarifu angalau raia wao.

Wamarekani waliingia matatani Kenya kwa kuwaonya raia wao tu kabla ya mashambulizi ya kigaidi Nairobi.

Sasa hapa wametaarifu umma napo wanalaumiwa.

Mmakonde anakwambia "ukichimama nchale, ukikimbia nchale".
Tahadhari ya kimbunga 'keneth' ilipotolewa na mamlaka za halia ya hewa duniani tuliziamini na kuchukua tahadhari japo kimbunga kilibadili mwelekeo na kutuacha salama, sasa kuna ubaya gani kwa tahadhari hii ambayo msingi mkuu ni kutupa msukumo wa kujiweka tayari kabla ya hatari?
Hakika nchi imeharibika.
 
Hahaah wivu utakuua mkuu,, sema watu walikua wanatamani kuona vita kwa sababu wamechoka kuhadithiwa vita vya zamani wakatamani kuona vita.

Ila ni sawa utabaki na uelewa wako ila uelewe tu kwamba kama ni shambulio la kigaidi au ambalo linahatarisha maisha yao, likiingia tu kwenye utandawazi kwa mana ya simu, computer, au njia yoyote ya mawasiliano ya kisasa basi wanaweza kupata taarifs yote kwa kina.

Na hawawezi kusema kwamba tumefuatilia sms au mawasiliano ya watu kwa sababu hiyo ni invasion of privacy kwa hiyo watakuzuga tuu kua hawana uhakika ila ujiongeze.

Ni kweli inaweza ikawa ni nchi ya kijinga ila naamini wametuzidi kiintelijensia na wanaona na kusikia mbali kuliko sisi. Kwa hiyo basi mpaka pale tutakapokua na intelijensia kali kama ile ya Mwalimu Nyerere na ikawa inatumia mbinu na vyombo vya kisasa zaidi, hatuna budi kuwasikiliza na kuheshimu maangalizo waliyotoa.

Kumbuka likitokea jambo halafu waje waseme kua tulifahamu lakini tukakaa nalo nadhani tutawachukia zaidi. Heri nusu shari... Kama ni muhenga utakua umeelewa. Sema inaonesha una chuki fulani na hao jamaa
Wala haina intelligensia ya maana sana ndio maana alishindwa kuvamia North Korea. Ni nchi yenye uchumi mzuri japo China itaipita kiuchumi. Ni nchi yenye madeni makubwa ikidaiwa Federal Reserve Bank benki ambayo iko owned na watu Roth family ni nchi ya kijinga sana ukii zoom.

Unaruhusiwa kutukana ili usife kwa pressure
 
Eti na Bashite naye anajitokeza kabana pua "mkoa wangu uko salama mbona hawakuniomba kibali cha kutangaza" !
Huu ujinga sijui unatoka wapi? Tahadhari ikitolewa watu wana jipanga Mara moja sio kuleta siasa.
Mlitaka US wawaarifu polisi wetu ambao siku kumi wanashindwa kumpata MO ndani ya Dar akiwa ametekwa? Acheni upumbavu chukueni tahadhari haraka mkiwashirikisha ubalozi wa US.
 
Na, Ibrahim Haroub Geveva

Nikiwa katika shughuli za kikazi za Umoja wa Mataifa hapa Geneva, nimefadhaishwa na namna Ubalozi wa Marekani Tanzania ulivyotoa taarifa ya UZUSHI huko Tanzania.

Mwaka 1998, hao ndugu walipigwa na hawakutoa tahadhari yoyote Dar es Salaam wala Nairobi. Nakumbuka nilikuwa Sudan wakati huo katika shughuli za Kanda ya Mashariki ya UN.

Hakukuwa na taarifa zozote za tahadhari kama huu uzushi. Jiulize kwa nini leo wametoa, tena siku ya Bajeti ya Nchi inapojadiliwa, Siku ambazo Watalii wengi wanakwenda kwa makundi makubwa Tanzania, Kuna nini hapo kimefichika?

Nimemuuliza Mtoto wa Shemeji yangu anayefanya kazi Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, amethibitisha hata Ubalozi wenyewe umeshangazwa na aliyechapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii bila kujiridhisha.

Wanahojiana, hivi walishindwa hata kuwapatia Polisi Oysterbay wachunguze? Au hata wale walinzi wa pale FFU au G4S ambao wanalinda Ubalozi wao?

Walishindwa kuwapa JWTZ? Walishindwa kuwapa Usalama wa Taifa waseme wanayojua? Je huu sio ujasusi uliopindukia katika nchi za wenzao?

Hayo maswali lazima yawasukume Wamarekani kuwaomba radhi washirika wao katika masuala ya Kiusalama. Kuna Mikataba ya Kimataifa inayowataka kushirikiana na vyombo vya ndani ya nchi husika wanapofuatilia mambo yanayohusu masuala ya ndani ya nchi.

Wamarekani hadi wanatoa kauli, walituma wachunguzi wao Masaki?Je, waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania au hata Umoja wa Mataifa? Wanatumia njia gani kuchunguza mambo nchini Tanzania hadi kutoa kauli ya namna hiyo?

Nani amewathibitishia huko mitaani hizo taarifa hadi kuchapisha katika tovuti yao? Tujiulize sote haya maswali.

Hivi Balozi wa Tanzania nchini Marekani hata akiwa na taarifa yoyote ya nchi hiyo ndio atoke kwa umma pale Washington DC kutangaza anachojua kuhusu Marekani? Sisi watu wa Diplomasia tunahoji, hiyo ni diplomasia ya wapi?

Basi ukiona hivi kuna jambo wanatengeneza kwa makusudi, si vinginevyo. Watanzania AMKENI.

Marekani, waombeni RADHI Watanzania na lazima mjenge tabia ya kufanya kazi na vyombo vya dola vya Tanzania katika kazi zenu. Umoja wa Mataifa unafuatilia jambo hili kwa karibu
Huyu ni fala tu...akawaambie wapumbavu wenzie personally nawaamini wamarekani
 
Mkuu wametoa kwenye ubao wao wa ubalozi kwa kupitia mitandao ya kijamii. Inatakiwa uelewe kua mitandao ile unaifatilia kwa hiari,, na hata wao walitegemea raia wa marekani ndio wafikiwe na huo ujumbe ila kama kuna sisi waswahili tunafatilia pia kurasa zao hizo ndio tumeipata pia.

Hawajachapisha kwenye gazeti na sio lazima kufatilia taarifa au kurasa zao kama hupendi wanachosema.

Mlaumu huyo alietoa huko na kuileta kwa watanzania wote.
I don't think walichofanya ni sahihi. Walitakiwa kuongea na vyombo vya dola.
Usalama sio kitu cha masihala....na Tanzania wanajitahidi mno kuhakikisha matatizo kama hayo hayatokei
 
Juni 19, 2019.
Kwa uzoefu wangu wa ufuatiliaji wa masuala ya kidiplomasia na siasa za kimataifa, kilichofanywa na Ubalozi wa Marekani katika Tahadhari yao iliyotolewa saa 1:19 Jioni tarehe 19 Juni, 2019 kuwa kuna minong’ono ya kutokea mashambulizi katika maeneo ya Masaki hususani katika hoteli na migahawa inayotumiwa mara nyingi na watalii na pia maeneo ya Slipway Msasani ni Mikakati ya makusudi isiyoitakia heri Tanzania.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa kupitia akaunti rasmi ya Twitter ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Marekani imekiri kuwa haina ushahidi wa kuwepo kwa tishio hilo na muda ambao mashambulizi yatafanyika na inawataka wananchi kuchukua tahadhari.

Kwa tabia za Marekani hasa pale wanapokuwa hawakubaliana na baadhi ya mambo kwa Taifa fulani hii ni mbinu ambayo huitumia ili kudhohofisha Serikali kwa kuwatisha Watalii, wawekezaji, Wafanyabiashara na hata wananchi wenyewe. Yapo maeneo ambayo hufikia hata hatua ya kutekeleza mashambulizi yenyewe ili mradi ionekane nchi hiyo sio salama na Serikali inashindwa kusimamia usalama wa nchi yake.

Huu ni ukoloni wa kupigiwa mfano na haukubaliki hata kidogo.

Zipo hoja kadhaa za kujiuliza kwenye tahadhari hii ya Marekani

1. Mkataba wa Vienna unaosimamia masuala ya Ubalozi na mashirika ya kimataifa katika nchi nyingine unaelekeza pamoja na mambo mengine, ni makosa kuingilia mambo ya ndani ya nchi ambayo Ubalozi upo. Mkataba huu unaelekeza kuwa kama kuna jambo lolote basi Ubalozi ama Shirika husika liwasiliane na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje. Kwenye jambo hili Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umekiuka kwa makusudi kwa sababu ni mpango mahususi wa kuichafua nchi.

2. Ubalozi wa Marekani unatoa taarifa nyeti kama hiyo kwenye jamii bila kuwa na uhakika na jambo lenyewe. Tena unakiri kuwa hauna ushahidi. Hili ni jambo la ajabu na hatari sana hasa linapotolewa na Ubalozi wa nchi yenye hadhi kama Marekani. Maana ya hili ni moja tu kufanikisha mpango wake wa kuichafua nchi baada ya kuona njia zote zingine haziwezekani. Kulikuwa kuna ulazima gani kwa Ubalozi wa Marekai kutangaza kupitia Twitter kwa jambo ambalo hawana uhakika nalo tena bila hata kuvijulisha vyombo vya ulinzi na usalama na Wizara ya Mambo ya nje ya nchi?

3. Kilichofanywa na Ubalozi wa Marekani ni kama kujivika usemaji wa masuala ya usalama kwa Tanzania, nchi ambayo ni Huru na ina uhuru wa kufanya mambo yake yenyewe. Ni vizuri Watanzania wakajiuliza hivi leo Balozi wa Tanzania nchi Marekani Mhe. Wilson Masilingi atoe taarifa kwa vyombo vya habari kuwa kuna minong’ono imeenea kuwa maeneo fulani ya Jiji la New York ama Washington DC yatashambuliwa na anatoa tahadhari kwa wananchi huku akikiri kuwa hana uhakika na minong’ono hiyo, PATAKALIKA?

4. Kama kweli kuna hiyo hatari isingekuwa busara kwa Marekani kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kupanga namna ya kukabiliana na mashambulizi hayo badala ya kukimbili kutangaza kwenye mitandao ya kijamii. Ama kuvijulisha vyombo vya ulinzi na usalama ili vyenyewe ndivyo vichukue hatua ya kutangaza na kuweka tahadhari?

Lakini pia ni vizuri Watanzania tujiulize kwa nini mambo yafanyike leo siku ambayo Jarida la Forbes limeitangaza Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa Amani katika Afrika Mashariki?

Kwa nini yatangazwe leo wakati ambapo Tanzania inaendelea kung’ara kila mahali kwa msimamo wa Rais wake Dk. John Magufuli ambaye ameamua kupigania maslahi ya Watanzania dhidi ya unyonyaji uliofanywa na watu na makampuni mbalimbali yakiwemo ya Kimarekani kama vile Symbion, kampuni iliyoleta vichwa vya Treni bila kuzingatia utaratibu na mengine mengi yaliyojiandaa kutupiga katika gesi, madini na mikataba ya kinyonyaji?

Mchezo kama huu umeshafanywa na Marekani katika maeneo mengi baadhi yake ni Korea Kaskazini ambako sote tunajua mzozo uliopo kati ya nchi hiyo na Marekani, Canada na Uganda kwa kutaja machache.

Najua wapo wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania ambao kwa umbumbu na ubinafsi wao watashangilia na kuunga mkono kinachofanywa na Marekani lakini Watanzania ni lazima tuwe macho na jambo hili.

Wamarekani ni wazuri sana kwenye kuharibu amani na uchumi wa nchi ambazo wanalazimisha maslahi yao. Na hutumia mbinu hii hii ya kuwatumia watu wa ndani na hapa kwetu wanatumiwa wanasiasa wa vyama vya upinzani. Walifanya hivyo Libya yanayowakuta Libya leo kila mtu anayaona, wamefanya Tunisia na kwingineko.

Watanzania tuvisikilize vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, na bahati nzuri tayari vimeshazungumza kuhusu jambo hili. Tuwaambie wawekezaji, wafanyabiashara na watalii ambao wanakuja kwetu Tanzania kuwa nchi yetu ipo salama na vyombo vya ulinzi na usalama vipo na vinaendelea na majukumu yake ya kila siku ya kulinda usalama wa nchi na watu wake. Hata siku moja jukumu la ulinzi wa nchi yetu halijawahi kuwa mikononi mwa Wamarekani na nchi yetu ina historia ya kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Kwao Marekani kila uchao watu wanauawa kwa kupigwa risasi, tena ni nchi ambayo silaha za moto zinauzwa kama saa ya mkononi. Silaha zimezagaa kila mahali na mauaji ya kutumia silaha yametamalaki lakini hata siku moja Balozi wa Tanzania hajawahi kutangaza hali ya hatari katika Marekani.

Huu ni uhuni.

Wasituvuruge.
Mlichopanga kufanya bila shaka kimebuma...Wapi wameingilia maswala ya ndani ya nchi. Hivi wapi mkataba wa Vienna unasema nchi isiwape taadhali wananchi wake walioko mataifa ya kigeni. Ebu kuweni wakweli katika ili..kama mipango imebuma basi sisi tunafurai sana.
 
Back
Top Bottom