Na, Ibrahim Haroub Geveva
Nikiwa katika shughuli za kikazi za Umoja wa Mataifa hapa Geneva, nimefadhaishwa na namna Ubalozi wa Marekani Tanzania ulivyotoa taarifa ya UZUSHI huko Tanzania.
Mwaka 1998, hao ndugu walipigwa na hawakutoa tahadhari yoyote Dar es Salaam wala Nairobi. Nakumbuka nilikuwa Sudan wakati huo katika shughuli za Kanda ya Mashariki ya UN.
Hakukuwa na taarifa zozote za tahadhari kama huu uzushi. Jiulize kwa nini leo wametoa, tena siku ya Bajeti ya Nchi inapojadiliwa, Siku ambazo Watalii wengi wanakwenda kwa makundi makubwa Tanzania, Kuna nini hapo kimefichika?
Nimemuuliza Mtoto wa Shemeji yangu anayefanya kazi Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, amethibitisha hata Ubalozi wenyewe umeshangazwa na aliyechapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii bila kujiridhisha.
Wanahojiana, hivi walishindwa hata kuwapatia Polisi Oysterbay wachunguze? Au hata wale walinzi wa pale FFU au G4S ambao wanalinda Ubalozi wao?
Walishindwa kuwapa JWTZ? Walishindwa kuwapa Usalama wa Taifa waseme wanayojua? Je huu sio ujasusi uliopindukia katika nchi za wenzao?
Hayo maswali lazima yawasukume Wamarekani kuwaomba radhi washirika wao katika masuala ya Kiusalama. Kuna Mikataba ya Kimataifa inayowataka kushirikiana na vyombo vya ndani ya nchi husika wanapofuatilia mambo yanayohusu masuala ya ndani ya nchi.
Wamarekani hadi wanatoa kauli, walituma wachunguzi wao Masaki?Je, waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania au hata Umoja wa Mataifa? Wanatumia njia gani kuchunguza mambo nchini Tanzania hadi kutoa kauli ya namna hiyo?
Nani amewathibitishia huko mitaani hizo taarifa hadi kuchapisha katika tovuti yao? Tujiulize sote haya maswali.
Hivi Balozi wa Tanzania nchini Marekani hata akiwa na taarifa yoyote ya nchi hiyo ndio atoke kwa umma pale Washington DC kutangaza anachojua kuhusu Marekani? Sisi watu wa Diplomasia tunahoji, hiyo ni diplomasia ya wapi?
Basi ukiona hivi kuna jambo wanatengeneza kwa makusudi, si vinginevyo. Watanzania AMKENI.
Marekani, waombeni RADHI Watanzania na lazima mjenge tabia ya kufanya kazi na vyombo vya dola vya Tanzania katika kazi zenu. Umoja wa Mataifa unafuatilia jambo hili kwa karibu