HOJA KATIBA MPYA: Mwanasheria Mkuu Zanzibar ampinga Werema

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,136
Salim Said
MJADALA wa katiba sasa umeingia sura mpya baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Jaji Omar Makungu kutaka iundwe katiba mpya inayokidhi matakwa ya Watanzania, akipingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema anayetaka katiba iliyopo, iwekewe viraka. Jaji Makungu ni mteule wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein mara tu baada ya kuapishwa kuwa rais wa visiwa hivyo, kama ilivyo kwa Jaji Werema ambaye pia ni mteule wa kwanza wa Rais Jakaya Kikwete mara tu baada ya kuapishwa kuongoza nchi katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Jaji Makungu aliliambia gazeti hili jana kuwa katiba mpya ni muhimu kwa sasa kwa kuwa itasaidia kuweka misingi imara ya taifa, akipingana na Jaji Werema ambaye aliweka bayana kuwa "Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa,".

Lakini Jaji Makungu kwa upande wake alisema "Hoja ya katiba mpya ni nzuri na watanzania wanapaswa kukaa na kutafakari ili kuweka misingi imara ya nchi yao kwa sababu misingi ya nchi inapatikana katika katiba tu,". "Kwa nini kusiwe na umuhimu wa katiba mpya sasa? Nadhali wananchi wamesema na wameonyesha kuwa kuna mahitaji na umuhimu wa kuandikwa Katiba mpya.
Hilo hatuhitaji kujadili kwa sababu wao ndio wenye nchi," aliongeza Jaji Makungu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Alisisitiza, "Ni vizuri watu wakakaa, wakatafakari na kuandaa mapendekezo ya hoja zao kisha kuyawasilisha serikalini. Serikali nayo ni wanadamu, kukiwa na hoja ya msingi watabadilika. Tume itaundwa na mchakato wa kuandikwa katiba mpya utaanza."

Jaji Makungu alisema wazo la kuandikwa Katiba mpya ni jema lakini watu wanatakiwa kuwa makini katika kutoa mapendekezo yao, kwa sababu hapo ndio wanapoweza kuweka misingi ya taifa lao, watoto na wajukuu zao.

"Watu wafanye wasichoke, kama CUF walivyofanya wameandaa mapendekezo yao wamewasilisha serikali, Chadema nao wafanye, NCCR-Mageuzi na vyama vingine, wanaharakati na wadau wengine nao wafanye, serikali itabadilika tu," alisema Jaji Makungu.
Kwa kauli hiyo Makungu ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, anaungana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan kuunga mkono hoja ya kuundwa katiba mpya.

Madai ya Katiba mpya pia yamewahi kutolewa na Mamakamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuwa mabaya.

Wakati Jaji Makungu akisema hayo, baadhi ya Watanzania wanaoishi ughaibuni wamesema suala la kuandikwa kwa katiba mpya ya Muungano halitakiwi kucheleweshwa tena.
Kauli hiyo ilitolewa na Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nje kusema hatua ya Watanzania kudai katiba mpya kwa nguvu zote inathibitisha uelewa wao wa kiwango cha juu wa mapungufu yaliyomo katika Katiba iliyopo. Watanzania hao wanaoishi katika nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani pia wamekipongeza chama cha CUF kwa uthubutu wao wa kuandaa rasimu ya katiba na kulazimisha kuiwasilisha serikalini kwa maandamano ya amani.

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam jana na kusainiwa na Katibu wake Abdulla Abdulla, ilibainisha suala la katiba mpya ni jambo lisiloepukika kwa sasa.
"Kwanza tunawapa pole na kuwafariji wanachama wa CUF na wananchi wote waliojeruhiwa au kukamatwa katika maandamano ya kuwasilisha rasimu ya katiba mpya; lakini tunawapongeza sana viongozi na wananchi waliojitolea kushiriki katika maandamano hayo na kufanikiwa kuiwasilisha rasimu hiyo," alisema Abdulla.
Abdulla aliongeza, "Hatua hiyo waliyoichukua inathibitisha uelewa wao wa kiwango cha juu wa mapungufu yaliyomo katika Katiba iliyopo sasa ambayo haikidhi matakwa ya wananchi wengi wa Tanzania." "Tunaamini kuwa rasimu hiyo ni kielelezo halisi cha matakwa ya wananchi walio wengi na itakidhi kabisa hoja zote za kikatiba na kisheria ambazo kwa muda wote zimekuwa ni miongoni mwa matatizo ya msingi yanayoidhoofisha demokrasia nchini," alisema Abdulla.

Alisema wananataraji hatua iliyochukuliwa na wananchi itakuwa ni changamoto muhimu sana kwa viongozi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ngazi zote na kila mmoja wao ataikubali na kuitafsiri kuwa ni kichocheo cha kufungua kwa upana zaidi milango ya siasa za uwazi na dira kamili ya demokrasia iliyokamilika.
"Tunaziomba taasisi zote za kiserikali na zile ambazo si za kiserikali kuunga mkono rasimu hiyo ili nchi yetu iweze kupata katiba mpya na tuachane na tabia ya kutia viraka kwani kufanya hivyo ni kuongeza matatizo badala ya kuyatatua," alisema Abdulla.

SOURCE: MWANANCHI.

Mtazamo: Niliwaambia demokrasia Zanzibar imebadilika na kuna mabadiliko makubwa sasa hivi sijui huko baadae. sasa tunaanza kuona jinsi gani demokrasia inavyokomaa zanzibar. viongozi wake wanaongea kwa sauti ya wananchi na siyo chama kama waheshimiwa wetu wa bara. Mie sisupport hoja ya katiba mpya mpaka kuwapo na mdahalo baina ya wanaodai katiba mpya na wasiodai ili wapi yaonekane mapungufu ya katiba hii na je haya mapungufu kweli yana umuhimu wa kuandika katiba mpya au kuziba mashimo. Ila nampongeza sana huyu spika kwa kusema uwazi.
 
Hakuna haja ya viraka twataka katiba mpya!

Sikatai mkuu ila wasiwasi ni kwamba hiyo katiba mpya inaweza katiba mbovu kuliko ile katiba iliyopo sasa. KUMBUKA KUWA NA KATIBA MPYA SIO KUWA NA KATIBA INAYOKIDHI MAHITAJI. Hivyo basi kufanyike mchakato wapi ni muhimu.
 
Nikisema nikujibu kwa ufasaha ulichoandika hapa nina uhakika utasema nimekutukana au nimekuzaririsha, wacha tu nipite niangalie thread za watu wengine, maana shida kubwa hapa hatujuwani umri wala kiwango cha elimu.
 
Are mad? Just be fair and consult your decorum faculty of thinking and conscience!
 
Hakuna haja ya viraka twataka katiba mpya!

Kusema ukweli mkuu njowepo kama we ni mfuatiliaji mzuri wa sheria na historia kudai katiba mpya kabisa na kutupa iliyopo ni jambo gumu sana na wala sina uhakika kama wataalamu watakapotunga hiyo mpya kua ndo itakidhi mahitaji!!
Nchi nyingi duniani ikiwa ni pamoja na amerca ambao ni ma champion wa demokras hawajawahi kutengeneza katiba mpya ila katiba iliyopo hua inafanyiwa marekebisho ili kukidhi haja kulingana na mahitaji yanavyoongezeka.
Mi naona kama mtu akisema anataka katiba mpya kabisa na kutupa iliyopo ni kama anasema tz haijawahi kupata uhuru wala kujitawala yenyewe jambo ambalo lina mzalilisha mpaka baba yetu wa taifa.
Tunahitaji marekebisho makubwa kwenye vifungu vya katiba iliyopo na si katiba mpya
.
 
Watu wanadhani kutunga katiba mpya ni kitu rahisi na ndio maana wanafuata tu mkumbo katiba mpya katiba mpya tujadiliane waungwana faida na hasara ya katiba mpya na hii iliyopo otherwise tunaweza kutunga katiba mbovu tukakosa wa kumlaumu.
 
Nikisema nikujibu kwa ufasaha ulichoandika hapa nina uhakika utasema nimekutukana au nimekuzaririsha, wacha tu nipite niangalie thread za watu wengine, maana shida kubwa hapa hatujuwani umri wala kiwango cha elimu.

Naamini shida kubwa kwa wanaopinga katiba mpya ni hili neno MPYA ndilo lawatisha. Wanadhani wanaodai katiba mpya hawakubali ibara hata moja iliyoko katika katiba iliyopo. Poor!

Ukiwasikia wanasema iwekewe viraka, lakini viraka vinapozidi nguo hushindwa julikana rangi yake kutokana na viraka vingi vyenye rangi tofauti!

Lakini kikubwa, ni kwamba hivyo viraka wanavyodai kabla havijawekwa pamoja na mengine mengi ndiyo yanafanya katiba iliyopo kuwa dhaifu. Ninaamini viraka vinavyodaiwa sasa vitaonekana ktk katiba mpya vikiwa si VIRAKA tena, na baadhi ya ibara ambazo bado zinatufaa zitawekwa pia!

Anaeogopa/anaekataa katiba mpya lazima kuna benefits flani anazipata ama kwa kutumia mianya ya ubovu wa katiba iliyopo au kwa madaraka anayopewa na katiba iliyopo akijua kuwa katiba MPYA itaziba mianya hiyo. Watapoteza.

Katiba mpya ni lazima!
 
Mh kweli kazi tunayo hembu nikuulize unadhani ni vifungu gani unaviona havifai au vyote havifai?
 
Watu wanadhani kutunga katiba mpya ni kitu rahisi na ndio maana wanafuata tu mkumbo katiba mpya katiba mpya tujadiliane waungwana faida na hasara ya katiba mpya na hii iliyopo otherwise tunaweza kutunga katiba mbovu tukakosa wa kumlaumu.

katiba mpya ni lazima kutokana na mabadiliko mengi na makubwa ya kijamii,kisiasa,kiuchumi ambayo yametokea na yatakayotokea na tayari katiba iliyopo imekwisha kuonyesha udhaifu mkubwa hasa katika kukidhi mabadiliko ya kisiasa na kijamii na kiuchumi, na kuweza kukabiliana na changamoto za makundimbalimbali ya kijamii na pia utandawazi.
pia tutambue sisi kizazi chetu ndo kinawajibika kuwewawekekea misingi iliyobora na endelevu vizazi vyetu vijavyo ambao nao watawajibika kuifanyia marekebisho au hata kuiandika mpya ili kukidhi mabadiliko ya nyakati zao/hizo.

suala la kusema nani wa kulaumiwa si hoja maana sisi ndo tutakuwa ndo tuataiandika na si kwamba hii mpya itakuwa imeshushwa toka mbinguni au peponi kwa hiyo tujiamini na kupanua ushirikishwaji wakati wa mchakato wa kutoa maoni na pia tutoe maoni ambayo ni yatakidhi mahitaji yetu sasa na baadaye na pia endelevu,
Hivyo natoa mwito kuwa badala ya kulumbana tuanze kuleta maoni ya vipengele vipi vinahitajika kuendelezwa katika katiba ya sasa, vipengele zipi sifanyiwe marekebisho na kujumuishwa, na vipengele vipya kabisa za kuandikwa na vyote vikiunganishwa ndo tutakuwa na katiba mpya.

lakini napendekeza pia watu tukasome kama hatujaisoma katiba iliyopo ili tujue nini kipo na kina mapungufu gani na nini kinahitajika kukidhi mahitaji yetu.

shime tuanze kutoa maoni na mapendekezo na tuweze kuyajadili kwa kina katika jamvi hili na hatimaye tuyapeleke kwa wakusanyaji wa maoni
 
Tazama hii video kuanzia dakika ya 27

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom