HOJA HII DHIDI YA SHAKA NI UPUUZI
Na Bollen Ngetti
RAIS SSH katika kukwamua uchumi uliodorora kufuatia janga la Covid-19 na matumizi ya hovyo ya Fedha za umma ametafuta na kupata 1.3 Trilioni kutoka IMF.
Fedha ambayo ameelekeza kutumika hapa hapa nchini kwenye miradi ya maendeleo na hivyo pesa yote hii itazunguka humu humu nchini. Lakini akasema, "wengi wanajua mimi ni mweupe hapana, ukitaka kujua rangi yangu halisi wewe dokoe fedha hizi". Hii ni salaam.
Lakini, haikuishia hapo. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Ndugu Shaka Hamidu Shaka naye akapigilia msumari wa moto, "ole wake atakayejaribu kudokoa fedha hizi kinyume na maelekezo ya matumizi yake, atakutana na rungu la usoni". Kwamba Shaka anasisitiza alichokisema Iron Lady, Samia.
Sasa, kuna hoja ya kipuuzi inaundwa na lile kundi lililoweka masharti ya kipuuzi ya kukutana na Msajili wa Vyama likidai, "Kwani ni kazi ya Shaka kuwaonya watendaji wa Serikali au kazi yake ni kueneza Itikadi ya chama?" Kwamba Shaka hana hayo Mamlaka.
Hoja dhaifu na ya kipuuzi sana. Iko hivi watani na wazoefu wa Mahakama, Serikali ya Samia ilipewa ridhaa na wananchi walioamua kuipa ushindi CCM. Kwamba, CCM ndiye mwenye duka na Serikali ni mwajiriwa tu.
Ni CCM ilimadi ilani yake 2020 na wananchi wakaikubali na kukichagua na hivyo kukipa ridhaa ya kuunda Serikali. CCM ni bosi wa Rais SSH.
Ifikapo 2025 Serikali ikiboronga umma utawauliza CCM na si Serikali. Hivyo CCM lazima ihakikishe Serikali yao inatekeleza walichoahidi wasije kukosa majibu 2025.
Shaka ni Msemaji wa chama. Kauli yake ina baraka zote za chama. Kwa mantiki hiyo anapoongea Shaka ni CCM wenye dhamana wameongea. Ndio maana anao uwezo wa kukagua miradi ya maendeleo yote ni kuhakikisha Serikali inatekeleza ilani yao.
Kazi ya Uenezi si kutangaza chama tu. By the way, nchi ni wapi CCM hakijulikani hadi ukakitangaze? CCM si chama chenye ngome upande fulani wa nchi kama kilivyo kile saccos ya babamke. Hapana.
Hizi 1.3 Trilioni zitanufaisha wananchi wote. Hakuna atakayebanwa mbavu kwa Covid-19 akanyimwa mtungi wa oksijeni kisha yeye ni Ufipani, hapana. Kwa hiyo sote tuunge mkono kauli ya Shaka, ina tija kwetu.
#MguseMamaNinuke