Hoja binafsi ya Mh. Kafulila imedhaminiwa na waathirika wa DOWANS

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Wadadisi wa mambo wanabainisha kuwa mkakati kujisafisha uliobuniwa na waathirika wakuu wa sakata la Richmond/Dowans unavyo vipengere vinne;

kipengere cha kwanza kilikuwa cha kumpata spika anayeunga mkono kundi hilo;
kipengere cha pili ni kupata njia ya kuwasilisha tena hoja hiyo bungeni baada ya kuhitimishwa rasmi katika bunge lililopita,hii ndiyo kazi inayotarajiwa kutekelezwa na mh Kafulila, pengine baada ya kuandaliwa na Zitto;
kipengere cha tatu tatu ni kupata idadi ya kutosha ya wabunge watakao azimia kufanyia suala hilo uchunguzi mpya pinde suala hilo litakapo wasilishwa bungeni, inasemekana idadi hiyo ilkwisha patikana;
kipengere cha nne ni kuteka hisia za watu ili wafikirie kwamba serikali hatua ya kufanyia uchunguzi tena suala hilo imetokana na kubanwa kwa serikali, hiyo ndiyo kazi inayofanywa sasa na UVCCM
 
NI ngumu sana kuamini vitu vilivyofichika ndani yetu ila unapoanza kuangalia kumbo la watu wa CCM kwa 2015 hili nalo linawezekana.

Sasa wanapishana kama magari kwenye highway....kila mtu akitafuta mtoko wake

Wataalam wanasema "Maamuzi ya kikao huvunjwa kwa kikao" ninaamini wanataka kutumia hili kujengea ya kwao "Findings za Committee huvunjwa na Findings za Committee Nyingine".

Let wait and see lakini hizi ni chenga za kisiasa za mwaka 47 ambazo wanasiasa wa leo wakizitumia ni ishara tosha ya kuwa wamefilisika na hawawezi kuongoza tena mustakabali wa taifa. Ni kuwapiga chini tu sasa
 
hao wadadisi wa mambo wanaoongelewa hapa ni kina nani?. . . imekaa kama hisia za mtoa mada zaidi kuliko habari za kidadisi, sentesi zinagongana zenyewe kwa zenyewe
 
Kujaribu kufanya hivyo ni dhahiri kuliaaibisha bunge lililopita,kamati ya bunge iliyofikia maamuzi yale, na hasa Mzee six, Mwakyembe, mm Kilango nk.

Foolhardy indeed. Kundi hilo ni moto halitakubali kudhalilishwa. Lakini pia kumbuka sasa hivi ngome ya opposition ni kubwa ikiongozwa na vijana tena wazungumzaji mno.Wanauwezomkubwa wa kupanga na kupambanua hoja. Waache wakaaibishwe zaidi na hasa wanataka kile kilichofichwa kwa kuinusuru aibu serikali kuwekwa nje.

SUBIRINI WAYASHIKE MAKAAYA MOTO,ni kutoka kikaangoni hadi motoni.
 
tarita, husisaau karibu asilimia 60 ya wabunge wa ccm ni wapya, na kesho wanaanza kuwapiga msasa na uende bahasha pia zikatembea. Aidha wapinzani hivi sasa hawako kundi moja; kwa mtazamo wa vyama vingine vya upinzani ni afadhali ccm kuliko chadema.
 
Back
Top Bottom