Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Kwa sasa Tanzania tunashuhudia tabia ya ajabu ya madiwani na Wabunge kujiuzulu na kuhamia chama kingine kwa kisingizio cha kuunga mkono upande wa vyama wanavyohamia. Tunajenga nyumba moja ni upuuzi kudai kuwa ukihamia upande wa chama A utajenga vizuri zaidi kuliko upande wa chama B. Ijulikane kwamba mawazo, sera au ilani ya CHAMA A inaweza ikachangia kuleta maendeleo bora zaidi kuliko hata chama B.
Ukisikiliza sababu zinazotolewa na Wabunge au Madiwani hazina msingi, mashiko wala uzito unaostahili. Ni upuuzi kujiuzulu Udiwani na Ubunge na kuhamia chama kingine kwa kuunga mkono chama kilichopo madarakani au pinzani kwasababu yoyote ile.
Kulingana na Katiba ya JMT wakti wa Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani Watanzania huwa hawachagui mtu baali wanachagua Ilani au Sera za Chama kitakachoshika dola kwa miaka 5 ijayo. Kwa kuwa Diwani au Mbunge anayeshinda kwenye eneo husika huwa Watanzania wamechagua Ilani au Sera za chama na siyo mtu basi kujiuzulu kwa Diwani au Mbunge kusiruhusiwe kuwarudisha Watz nyuma kuingia kwenye Uchaguzi mpya kwa namna yoyote ile.
Uchaguzi huu huwa una ligharimu Taifa mabilioni ya Fedha ili kutekeleza haki ya Kidemokrasia kwa Watanzania. Ni upuuzi kuanza kurudia chaguzi za Udiwani na Ubunge ndani ya kipindi cha mwaka au miaka kadhaa kabla ya kipindi cha miaka 5 kwasababu ya mtu kujiuzulu na kuhamia chama kingine isipokuwa iwe ni kifo.
Kutokana na maelezo hayo naomba sasa Bunge litunge sheria kali za kuzuia Madiwani na Wabunge kuhama toka chama kimoja kwenda kingine kwasababu za kishabiki isipokuwa kifo kama ifuatavyo:

- Diwani au Mbunge anayejiuzulu na kujivua uanachama asiruhusiwe kugombea tena Udiwani au Ubunge mpaka kipindi cha miaka 5 aliyokuwa amechaguliwa iwe imepita.
- Kwa kuwa Watanzania walichagua sera au ilani ya chama husika wakati wa Uchaguzi Mkuu,nafasi inayoachwa wazi ipewe chama kilekile cha aliyejiuzulu kutokana na washindi wa 2 waliopatikana wakti wa mchakato wa kupata wagombea.
- nafasi ya Udiwani au Ubunge iliyobaki wazi baada ya mhusika kujiuzulu ijazwe na Wanachama wa chama kilekile kilichoshinda Ubunge au Udiwani kwa waliokuwa washindi wa 2 kwenye mchakato wa kutafuta wagombea au kura za maoni.
- Nafasi ya Udiwani au Ubunge iliyobaki wazi baada ya mhusika kujiuzulu ijazwe na Wanachama wa chama kilekile kilichoshinda Ubunge au Udiwani kwa waliokuwa washindi wa 2 kwenye mchakato wa kutafuta wagombea au kura za maoni.
- Kunapotokea kwamba Mbunge au Diwani amefariki dunia basi mchakato wa kupata Mbunge au Diwani utokane na chama kilekile cha Mbunge au Diwani aliyefariki kwa kuangalia matokeo ya washindi wa 2 wakti wa mchakato wa kupata wagombea.
- Iwe ni marufuku kurudia Uchaguzi wa Madiwani au Wabunge kwa sababu za kujiuzulu kwa vile Uchaguzi ni kuwabebesha Watanzania gharama zisizo za lazima.