Hoja binafsi kuhusu kujiuzulu kwa wabunge na madiwani na kuhamia chama kingine

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kwa sasa Tanzania tunashuhudia tabia ya ajabu ya madiwani na Wabunge kujiuzulu na kuhamia chama kingine kwa kisingizio cha kuunga mkono upande wa vyama wanavyohamia. Tunajenga nyumba moja ni upuuzi kudai kuwa ukihamia upande wa chama A utajenga vizuri zaidi kuliko upande wa chama B. Ijulikane kwamba mawazo, sera au ilani ya CHAMA A inaweza ikachangia kuleta maendeleo bora zaidi kuliko hata chama B.

Ukisikiliza sababu zinazotolewa na Wabunge au Madiwani hazina msingi, mashiko wala uzito unaostahili. Ni upuuzi kujiuzulu Udiwani na Ubunge na kuhamia chama kingine kwa kuunga mkono chama kilichopo madarakani au pinzani kwasababu yoyote ile.

Kulingana na Katiba ya JMT wakti wa Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani Watanzania huwa hawachagui mtu baali wanachagua Ilani au Sera za Chama kitakachoshika dola kwa miaka 5 ijayo. Kwa kuwa Diwani au Mbunge anayeshinda kwenye eneo husika huwa Watanzania wamechagua Ilani au Sera za chama na siyo mtu basi kujiuzulu kwa Diwani au Mbunge kusiruhusiwe kuwarudisha Watz nyuma kuingia kwenye Uchaguzi mpya kwa namna yoyote ile.

Uchaguzi huu huwa una ligharimu Taifa mabilioni ya Fedha ili kutekeleza haki ya Kidemokrasia kwa Watanzania. Ni upuuzi kuanza kurudia chaguzi za Udiwani na Ubunge ndani ya kipindi cha mwaka au miaka kadhaa kabla ya kipindi cha miaka 5 kwasababu ya mtu kujiuzulu na kuhamia chama kingine isipokuwa iwe ni kifo.

Kutokana na maelezo hayo naomba sasa Bunge litunge sheria kali za kuzuia Madiwani na Wabunge kuhama toka chama kimoja kwenda kingine kwasababu za kishabiki isipokuwa kifo kama ifuatavyo:

  1. Diwani au Mbunge anayejiuzulu na kujivua uanachama asiruhusiwe kugombea tena Udiwani au Ubunge mpaka kipindi cha miaka 5 aliyokuwa amechaguliwa iwe imepita.
  2. Kwa kuwa Watanzania walichagua sera au ilani ya chama husika wakati wa Uchaguzi Mkuu,nafasi inayoachwa wazi ipewe chama kilekile cha aliyejiuzulu kutokana na washindi wa 2 waliopatikana wakti wa mchakato wa kupata wagombea.
  3. nafasi ya Udiwani au Ubunge iliyobaki wazi baada ya mhusika kujiuzulu ijazwe na Wanachama wa chama kilekile kilichoshinda Ubunge au Udiwani kwa waliokuwa washindi wa 2 kwenye mchakato wa kutafuta wagombea au kura za maoni.
  4. Nafasi ya Udiwani au Ubunge iliyobaki wazi baada ya mhusika kujiuzulu ijazwe na Wanachama wa chama kilekile kilichoshinda Ubunge au Udiwani kwa waliokuwa washindi wa 2 kwenye mchakato wa kutafuta wagombea au kura za maoni.
  5. Kunapotokea kwamba Mbunge au Diwani amefariki dunia basi mchakato wa kupata Mbunge au Diwani utokane na chama kilekile cha Mbunge au Diwani aliyefariki kwa kuangalia matokeo ya washindi wa 2 wakti wa mchakato wa kupata wagombea.
  6. Iwe ni marufuku kurudia Uchaguzi wa Madiwani au Wabunge kwa sababu za kujiuzulu kwa vile Uchaguzi ni kuwabebesha Watanzania gharama zisizo za lazima.
Naomba kuwasilisha.
 
unachozungumza hapa ni nadharia tu,
wewe unafahamu wazi kabisa kwamba watanzania wengi huwa hawachagui ilani, bali wanachagua watu na chama.
pia unafahamu wazi kuna baadhi ya watu wamediriki kusema wapo tayari kuchagua hata jiwe eti kwa sababu wanataka chama flani.
lakini pia unafahamu kwamba chama kinaweza kuwa na sera na ilani nzuri lakini wasimamizi ktk utekelezaji wa hizo sera wakakosekana.
sasa basi, kwa nini mtu asitafute welekeo ambao anaamini/ ameona sera zilizopo zinatekelezwa kama yeye alivyotegemea? na tena anapata `pumzi' ya maamuzi kutokana na katiba iliyopo.
 
Huyu anaejiuzuru leo kw sbbu za hovyo km wewe unavyodai.na hawa waliowahi kutamka kuwa km ccm itasimama kwenye uchaguz na shetani wako tayari kumchagua shetani na kuiacha ccm.nani mjinga au mpumbavu kati ya hao wawili.
 
Ni haki yao kikatiba, waache wajiuzulu, mtu hawezi kulazimishwa kufanya kazi, au kuwa na imani fulani muda wote, imani ya mtu inaweza kubadilika hivyo ni haki yao, waache watumie haki yao kikatiba.
 
Wanajf
huu niushahidi mwingine ambapo mwl nyerere alisema tuna watu wanaopenda kutawala na sikusaidia wananchi.Najiuliza Dr,MOLELL kinachomrudisha ccm ni itikadi ya ccm au niuongozi wa magufuli ambaye baada ya muda yanapotea?
 
Pesa inayotumika kuwanunua Wapinzani ni pesa ya walipa kodi toka Hazina na walipa kodi wengi si wanachama wa CCM, hivyo CCM wanatumia pesa za Umma kwa kazi za hovyo hovyo, pesa ya kurudia uchaguzi ni pesa ya walipa kodi ni pesa ya Umma, pesa zinatumika sasa kudhoofisha upinzani ni pesa nyingi sana haijapata kutokea popote Duniani, ni pesa ambazo zingeweza kutumika kupeleka maendeleo jimboni wilayani mikoani na CCM wangevuna kura pasipo kufanya uchakachuaji na kuiba Kura,Hili Dili la 10% lililochongwa na Maliyamungu Bashite na Lipumba pamoja na le mutuz ni Ufisadi Hatari kuliko Ufisadi wowote Afrika, wao wanapata pesa lakini pesa za Umma zinapotea kwa kazi za hovyo hovyo.
 
Huyu anaejiuzuru leo kw sbbu za hovyo km wewe unavyodai.na hawa waliowahi kutamka kuwa km ccm itasimama kwenye uchaguz na shetani wako tayari kumchagua shetani na kuiacha ccm.nani mjinga au mpumbavu kati ya hao wawili.
Dili la Lipumba, Maliyamungu Bashite na le mutuz ndiyo limekuwa Sumu ya upinzani kwa sasa, wanapiga pesa nyingi kwa mgongo wa kuzitumia kudhoofisha upinzani.
 
Ni haki yao kikatiba, waache wajiuzulu, mtu hawezi kulazimishwa kufanya kazi, au kuwa na imani fulani muda wote, imani ya mtu inaweza kubadilika hivyo ni haki yao, waache watumie haki yao kikatiba.

Hatuwezi kuendelea na sheria za kipumbaf zinazo ligharimu Taifa mabilioni kwa kisingizio cha HAKI YA KIKATIBA! Huu ni uzezeta na Katiba siyo msahafu lazima ifumuliwe kuondoa huu ujinga unaowanufaisha wapuuzi fulani wa Chama Twawala...!! Kwa utawala huu wa CCM na mbinu zinazotumiwa na CCM kutaka kufuta upinzani surely there is no DEMOCRACY in Tanzania...!!!
 
Back
Top Bottom