Hoja binafi:- bila kujiunga na ccm........ Sidhani........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja binafi:- bila kujiunga na ccm........ Sidhani........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wakuziba, Jul 1, 2012.

 1. w

  wakuziba Senior Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huenda kichwa cha habari kikamfanya msomaji adhani kuwa mimi ni mfuasi wa ccm. la hasha! mimi ni mzalendo nilie na uchungu na nchi yangu. nchi kwanza vyama baadaye.

  baada ya tafakuri ya kina, naomba tujadili suala la demokrasia ya vyama vingi. kitu kikuu ambacho raia wanakitegemea na kukihitaji kutoka katika serikali yao ni KUWALETEA MAENDELEO. maendeleo ambayo yanaleta maisha bora kwa raia wote. tuna mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992 (1995). demokrasia inakua taratibu! si haba!


  HULKA YA MTANZANIA IKOJE

  Mtanzania ana tabia ya uhafidhina. siyo mwepesi kubadilika. mifano ipo mingi lkn niende kwenye soka. tuna timu kubwa za simba na yanga. miaka nenda miaka rudi ni simba na yanga. azam, mtibwa, coastal, majimaji, jkt, kagera, toto nk... wamekua wasindikizaji kwa muda mrefu. nchi zilizotuzunguka, wana kawaida ya kuwa na mabadiliko kila mwaka kwenye uongozi wa ligi. kenya kulikua na gormahia na afc leopards kwenye chati, uganda kulikuwa na kcc, villa na express, malawi kulikua na bata bullets na zambia kulikuwa na nkana red devils. hizi timu zilitamba miaka ya nyuma. raia wa nchi nilizotaja, wamekua wakishabikia timu inayofanya vizuri. hawana uhafidhina. HAPA KWETU HATA TIMU IKIFANYA VIZURI MADHALI SIYO SIMBA AU YANGA, watanzania hawana habari nayo. HII NI ISHARA YA UHAFIDHINA WA WABONGO. kumhamisha mtanzania na kubadili mtazamo na fikra zake ni kazi kubwa sana! kwa upande wa siasa, kuna watanzania ambao huwaambii kuitu kuhusu CCM. siyo mijini wala vijijini. wana imani kubwa sn na ccm. HII NI ISHARA NYENGINE YA UHAFIDHINA WA WABONGO.


  HALI YA VYAMA VYETU IKOJE
  chama cha ccm
  ni chama kikongwe. kina makada wazoefu wa siasa za kila aina. siasa baridi, siasa safi na siasa chafu. kina mabingwa wa propaganda. pana uwezekano, kina mamluki ktk KILA chama cha siasa. ccm kina sifa moja kuu: kimeunganisha watanzania kutoka ktk kila kanda, dini, rangi na kabila. hali hii imetokana na kuwa chama pekee kwa miaka mingi hadi mwaka 1992. watanzania wote ilibidi wajiunge ccm. hawakua na mbadala. huwezi kusema ni cha wakristo au waislamu. wote ni chama chao. kasoro yake kuu ni moja: kinasuasua ktk kuwaadhibu wanachama wake wanaotajwa ktk kashfa mbalimbali za rushwa. kukumbatia wala rushwa ni ishara ya kwamba rushwa ipo na imeshamiri. hali hii inatusababishia maendeleo duni. wapinzani wametafsiri ccm kuwa ni chukua chako mapema kama kiashirio cha wanaccm kuiba mali ya umma.ccm wana hali ngumu kuhusu mgombea urais 2015 lkn wana sifa moja. wanaweza kuingia chimwaga / kizota wakiwa na tofauti. la ajabu wanatoka wakiwa kitu kimoja na wagombea wanapeana mikono. sijui huwa wanafanyaje!!!!!!!!!!!!!


  chama cha chadema ni chama ambacho kimefanya vizuri sana ktk uchaguzi wa mwaka 2010. idadi ya wabunge wake imeongezeka sana na ndiyo chama kikuu cha upinzani kwa sasa. kina viongozi jasiri ambao niwabunifu na hawana uwoga ktk kueleza na kutetea ukweli. kina kasoro kadhaa zifuatazo:-
  a). viongozi wake wakuu wana ushindani wa kisiasa, sifa na umaarufu. hili ni tatizo kuu chdm. kushindana huku kumewafanya waogopane na kuoneana wivu. wanaweza kuonekana wana safu moja lkn ukiangalia kwa jicho la kiuchambuzi utagundua kuwa slaa, mbowe, zitto , lissu, mnyika nk...... wana matabaka ya ndani kwa ndani. kila mmoja anataka atangulize kitu bungeni kwa kujijengea umaarufu yeye sio chdm.

  b). chama chochote lazima kianzie ktk eneo mojawapo ktk nchi yetu. chdm kilianzishwa na mtanzania kutoka kasikazini. bila shaka mizizi yake ilianza kuimarika kaskazini. ccm wakatumiya mwanya huu kukipaka matope kuwa ni chama cha kikanda na kikabila hadi wakatafsiri chadema kuwa ni chagga development manifesto (ilani au mradi wa kuwaendeleza wachagga). hali hii imefanya watanzania wengine waogope kujiunga na chama cha chdm.

  c). ccm wamepakaza kuwa chdm ni chama cha wakristo. wakawa wanatoa mfano wa viongozi wake wakuu. wakasema dk. kabourou alipokua katibu mkuu, alipigwa vita kwa kuwa ni muislamu. kutodhihirika kwa majina ya kiislamu ya marehemu bob makani na zitto kabwe, kulifanya watu waamini kuwa viongozi wote wa chdm ni wakristo. chdm hawakujitahidi kuweka wazi kuwa bob makani, zitto kabwe na mzee arfi ni waislamu. japo mzee arfi anajulikana lkn amekua hapewi nafasi ktk majukwaa ya chdm licha ya kuwa ni makamu mwenyekiti.

  d). chdm kimeridhika kwa kuwa na mashabiki na siyo wanachama wakereketwa. kimesahau kuwa kasoro ya ccm ktk kura za maoni mwaka 2010, ndizo zilizochangia ama chdm kupata wabunge waliohama ccm au wanaccm kukikomoa chama chao kwa kukipa chdm kura. huu ndiyo ukweli kuhusu mwaka 2010. pana uwezekano mkubwa kuwa iwapo ccm itacheza karata vizuri, itarudisha sehemu kubwa ya viti vyake mwaka 2015. ufunguzi wa matawi ya chdm unafanywa sn vyuoni na nje ya nchi kuliko vijijini. hii ni kasoro.

  e). kinyang'anyiro cha kumtafuta mwenyekiti wa chama na mgombea urais mwaka 2015 nalo ni tatizo chdm. mbowe, zitto na slaa wote nadhani wana nia ya kugombea urais. slaa alifanya vizuri 2015 lkn wengine wanamuona kama mzee ambae huenda asiwe na mvuto 2015. mbowe ana sifa lkn ile propaganda ya ccm kuwa chama kina wenyewe, inamgharimu kwa kufanya wanachdm kutoka mikoa mingine wasimkubali. baadhi wanadai kuwa ni dikteta vikaoni.

  f). wanachama wa chdm wanatumia sn jazba wanapowaelimisha wapinzani wao. wako radhi wamtukane mtu badala ya kumvuta taratibu kwa kumuelimisha. msomi anaweza kuguswa na wizi unaofanywa serikalini. mama muuza vitumbua hahitaji matusi anaposema yeye ni mwana ccm. anahitaji kuelimishwa kuwa wizi wa viongozi ndiyo umemfanya awe maskini nk..... hii ni kasoro kubwa ya wafuasi wa chdm. mambo ya tahriir square kwa tanzania bado sn. nani amejitokeza ktk sakta hili la dk ulimboka kuandamana! hawa ndiyo watanzania.


  chama cha wananchi cuf hakikufanya vizuri mwaka 2010 tofauti na chaguzi zilizotangulia. ni chama ambacho kina kasoro zifuatazo;
  a). uongozi wa juu wa chama haubadiliki. japo lipumba na seif wamejaribu kufafanua kuwa wao ni wapiganaji ambao wako vitani na makamanda huwa hawabadilishwi kama nguo ili huzuia malengo yasipotee, lkn watu bado hawajaelewa hoja yao vizuri. kutobadili viongozi wa juu kumetumiwa na ccm pamoja na chdm kuisulubu cuf.

  b). ccm ilianzisha propaganda kuwa cuf ni chama cha waislamu. kama ilivyo chdm, cuf nayo ilianzia sehemu mojawapo ya jamhuri yetu. wakazi wa eneo la visiwani wengiwao ni waislamu. cuf ikawa na wanachama wengi wa mwanzo wakiwa waislamu. hali hiyo ikatumiwa kisiasa na ccm kuwa cuf ni chama cha kidini na wakristo jambo hilo likawatia hofu kujiunga cuf! baadhi wanasema jina cuf lina asili ktk qur'an.

  c). licha ya profesa lipumba kuwa msomi lkn ameshindwa kuwavuta wasomi wenzake kujiunga na cuf. chdm kimefanikiwa kuwavuta wasomi wengi tu! kosa hili la lipumba limekiathiri sn chama.

  d). safari za mara kwa mara za lipumba nje ya nchi zinachangia kudumaza chama.

  e). hakuna asiejua hali na mpasuko wa kisiasa ulivyokua visiwani kati ya ccm na cuf. ilifikia waamue kuungana ili kusitisha tofauti zinazo irudisha nyuma znz. ni jambo zuri lkn chdm wamelitumia kwa kuisulubu cuf. wanaiita ccm B. si kweli kuwa cuf ni ccm b lkn kisiasa chdm wanahaki ya kusema hivyo ili waidhoofishe cuf. cuf wanadai kuwa vile wamo serikalini, 2015 watachukua serikali ya znz. hawatoibiwa kura tena. yetu macho!


  vyama vya nccr, tlp, udp nk....... havifanyi vizuri sn. inasemekana kuwa ushindi wa nccr kigoma ni kutokana na mgombea wao urais wa 2010, mzee hashim rungwe kuwa mwenyeji wa kigoma. walimpa kura za "tusimuangushe mtoto wetu...". mrema kwishnei, cheyo yupoyupo........


  KWELI CCM ITANG'OKA 2015?
  jibu la haraka ni kuwa HAPANA. pana uwezekano mkubwa wa ccm kushinda. kwa nn nasema hivi?

  1- ccm wanauzoefu wa kumpitisha mgombea na tofauti zikaisha. rasharasha huwepo lkn huwa chache sn. huu mtikisiko wa mgombea unaosubiriwa kwa hamu na wapinzani kuigawa ccm, sidhani kama utakuepo. akina mwakyembe na sitta wanaiponda sn chdm bungeni. wanakula kuku kwa mrija.
  2- vijijini bado wana imani kubwa na ccm na hata baadhi ya miji.
  3- tofauti za safu ya juu ya chdm zinaweza kukipa zilzala kipindi cha uchaguzi wa mwenyekiti na mgombea urais. kinaweza meguka. zitto anaweza hamia nccr. ana mvuto na wafuasi wengi.
  4- propaganda za ukanda na udini zimekua mwiba kooni mwa chadema. hakikubaliki sn kwa waislamu. anae bisha apitie matokeo ya uchaguzi wa 2010 ktk tovuti ya NEC. ataona jinsi chadema ilivyofanya ktk maeneo yenye waislamu wengi.
  5- cuf imekuwa ikiiharibia chadema. uwepo wa cuf ni kihunzi kwa chadema. na sasa uadui bungeni wa cuf na chdm ni mkubwa. hii inaashiria kuwa vyama vya upinzania haviwezi kumpitisha mgombea mmoja 2015. ni faida kwa ccm.
  6- ili ccm ifanye vizuri, pana uwezekano ikakubaliana kuwapa cuf znz ili wanacuf wa bara wote waipigie ccm. ieleweke kuwa mwana cuf yuradhi kuipigia ccm au nccr kuliko kuipa kura chdm
  7- siyo siri uchaguzi wa 2010 ulitawaliwa na udini (anaekataa hili atakua na matatizo). ccm ilikua na mgombea muislamu. cuf ilikua na mgombea muislamu. chdm ilikua na mgombea mkristo. wakristo wengi walipeleka kura zao chdm. kura za waislamu wengi zilikwenda ccm na cuf. mwaka 2015, pana uwezekano mkubwa ccm watampitisha mkristo. hali hii itapunguza kura za chadema. maaskofu ambao walikuwa upande wa chdm, wakiona mgombea mkristo ccm, watahama na wafuasi wao kwenda ccm. hali hii itaigharimu sn chdm 2015.
  8- uhafidhina wa watanznaia kuikumbatia ccm utaendelea kuisaidia. watu wako radhi kuipa kura ccm hata kama uchaguzi unafanyika kipindi ambacho umeme ni wa mgao nk........


  NINI KIFANYIKE?

  kuna usemi wa kiingerza usemao "IF YOU CAN'T DEFEAT THEM, JOIN THEM" kama unaona huwezi kumshinda adui yako, jiunge nae. ni bora wapinzani wakajiunge ccm tujenge nchi yetu. uwezekano wa kuwaondoa waovu ktk ccm utakua mwepesi makamanda wote wakiwa ndani ya ccm. jambo hili linaweza kutafsiriwa kuwa naipigia debe ccm lkn sivyo. kwani tatizo ni jina ccm au ni vitendo vya viongozi wa ccm? nje ya ccm itakua kazi kuking'oa hiki chama. tujiunge ccm. multipartism has many disadvantages than single party system!


  TANBIHI
  - makala yangu ili ieleweke kwa baadhi ya wasomaji, inabidi kupumzisha akili yko ili uazime uzalendo kwanza ndiyo uisome.
  - nimesukumwa na uzalendo kuandika makala hii na siyo utashi wa kisiasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  - japo nimefupisha ripoti ya utafiti wangu, naomba vyama viangalie kasoro zao ili vijirekebishe.
  - huu ni utafiti, nategemea constructive criticisms siyo matusi!

  wakatabahu: wakuziba (mzee wa ukweli unaochoma)
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  KANU ilipigwa chini kenya ndio itakua ccm
   
 3. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Somebody please read and summarise for me..
   
 4. w

  wakuziba Senior Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  siyo kwamba naiunga mkono ccm lkn kanu haikuwa na nguvu kama ccm. kwanza ukabila ni mkubwa kenya. muasisi wa kanu ni jomo kenyatta na wenzake. moi alikua kadu. alikuja kujiunga kanu baadaye. inasemekana japo alipata urais kupitia kanu, hakuwa na mapenzia na chama hicho ndiyo sbb alimfanya odinga kuwa katibu mkuu ili aisambaratishe kanu. alimpitisha uhuru kuwa mgombea urais wa kanu licha ya kukataliwa na wakenya wengi. inaelekea utangulizi wangu kuhusu hali ya wabongo kutobadilika haraka kuhuuelewa.


  nakupa ushauri wa bure: usiwe mvivu wa kusoma. pili chunguza siasa za kimataifa kabla ya kuchangia. hiki siyo kijiwe cha kahawa
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  habari yako ni nzuri ..ngoja nikae tena chini niisome maana naona mengi ni ya ukweli na mengine nahisi nahitaji kufanya some refferences
   
 6. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hapo penye ....wapinzani wajiunge na CCM ndipo palipoharibu kila kitu Mods unajua watu wengine wanatulazimisha tutukane naone tuwe na jukwaa la kutukanana kuliko ban huyu ananilazimisha nipate ban
   
 7. w

  wakuziba Senior Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi sioni sababu ya kunitukana. nimechambua kutokana na jinsi ninavyo fuatilia siasa hapa nchini. hilo ni wazo la kutaka watu wajiunge ccm ili wafanye mageuzi na mapinduzi wakiwa ndani ya ccm. ni mtazamo. kama ww unaona upinzani unaweza kuchukua nchi 2015 au 2020, una uhuru wa kukataa hoja yangu na kueleza sababu. nimesema ktk sababu za chdm na cuf kufanya vibaya ni WAFUASI WAKE KUPENDA MATUSI. ILE LUGHA YA KUMVUTA MWANA CCM HAIPO. ndugu yangu nachukua masters ya siasa. makala hii nimeitafiti. mimi siyo mkamilifu naweza kuwa nmekosea, jiepushe na kutukana. umesoma tanbihi yangu mwishoni mwa makala yangu?
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Duh!
  Naona wamekudharau!
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kama hao ccm wana uelewa mkubwa hivyo mbona kila kitu kinawashinda?hata kuwaua akina mwakyembe, mwandosya,uli, hata kufanya jema moja mbele ya macho ya wananchi?

  God yupo na sasa anafanya kazi kuliko ?Hata cdm wakifa, hata akina anilea nkya, na Bisimba.Mungu atawaondoa ktk Dittoo.Kufuru imefika mbali sana.kilio cha albino, hela ya desi, kilio cha watesekao ktk nchi, mahusiani na nchi haramu hatopona muovu
   
 10. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Umejitahidi kuchambua vizuri,lakini suala la wapinzani kuhamia ccm siyo busara hata kidogo. Bila shaka kuna falsafa hujaisoma,ni kwamba huwezi kuuzima moto uliokolea ungali bado uko ndani ya nyumba ambako kama utakuwa na maji mengi basi ni lita mia tu. Kama viongozi wakongwe kina Sitta wameshindwa kuleta mabadiliko ndani ya chama itakuwa sembuse wapinzani-wahamiaji. Pia watanzania wahafidhina wengi wao ni wazee,na kuna dalili kubwa za vijana kupenda mabadiliko.Kwa hiyo kama ambayo waswahili wanasema HAKUNA BINGWA MILELE,vyama vya upinzani bado vina fursa ya kufanya mabadiliko katika siasa zao kuliko kuvunja vyama na kuhamia ccm. Kama ulivyosema ni vema kufuatilia siasa za kimataifa: basi utakubaliana nami kwamba nchi nyingi duniani zinatoka kwenye monopartism kwenda multipartism kwa hiyo kwa maoni yako tutakuwa tunapishana na wakati. N.B-Mpunga umechukuliwa,pumba zimeachwa!
   
Loading...