Hoja 28 za Juma Duni Haji

Hoja 28 za Juma Duni Haji

Chama kilimpitisha kuwa mgombea ubunge huko unguja baada ya kukataa kuwa mgombea mwenza wa lipumba .Ila njaa na tamaa ikampeleka chadema kuwa mgombea mwenza wa lowasa.
Na hata mikutano yake ya mgombea mwenza alikuwa anazunguka na watu wa cuf ambao leo wanataka kuvuliwa uanachama akina mnyaa.
Na alizunguka nao mpaka ikafikia wakati anataka kususa sbb migogoro ya majimbo ilikuwa kila mahali.

kuna watu wanadhani mafanikio ya cuf au Cdm yalikuja miezi miwili ya mwisho , na si jitihada ya kila chama , mikutano waliofanya, na kuhamasisha watu kujiandikisha pamoja na Ccm kuchokwa hasa kwenye rushwa kila kona , serikali za mitaa mbona Cuf na Cdm walifanya vizuri tu chini ya viongozi wao wa asili
kulikuwa kuna haja gani lowasa kuletwa wakati wagombea walikuwepo wenye sifa, na je baada ya kusaini makubaliano je yaliheshimiwa hasa yale ya kuachiana majimbo je yaliheshimiwa? matatiro alikosa jimbo je mr. duni hilo halikuumizi kama kiongozi wa juu wa chama .
ni ujinga kwa mwanafunzi aliyejiandaa na mtihani kisawa sawa kwa bahati nzuri /mbaya mtihani ukavuja kapata alama 42 halafu akajisifia kuwa hayo ni mafanikio . kwangu mim naona CUF walitakiwa wafanye vizuri zaidi ya hapo kwa kuwa ccm ilikuwa taabani na wanapaswa wajilaum wenyewe kwa hilo
 
Aiseee sikuwahi kufikiri kama huyu mheshimiwa Babu Duni Hajji ana akili kubwa namna hii!
Baada ya Hashim Rungwe,Babu Duni anaingia ktk list ya wanasiasa walionifurahisha zaidi mwaka huu.
Ni makala ndefu lakini nimeisoma hatua kwa hatua,nukta kwa nukta.
Huyu Mzee alifaa kabisa kuwa makamu wetu wa Rais endapo haki ingetendeka.
Mungu akupe uhai Mzee wetu,2020 sio mbali.
 
Hapa ndio tofauti ya wazanzibar Na watanganyika inapoenekana. Wanzibar nje ya Zanziba wanakuwa pamoja.

Hoja za Duni zinawakuna waliojua Siasa baada ya Lowasa Na gia za angani. Babu Kama hajui Leo mchango wa Lipumba Na Slaa basi pasi nashaka Siasa Ni uongo Na ulaghai.
Babu duni akumbuke kauli zake mwenyewe Na serikali Yao ya kitaifa Na namna wananchi walivyochoka CCM kabla ya uchaguzi.
Lipumba wanamtumia Kama kafala Yao lakini Duni ndiye aliyevunja serikali ya kitaifa Zanzibar kwa kuwa kigeugeu Na haki ya mungu Kama Lipumba anatumika basi Na Babu duni anatumika the same way.
Babu duni alikimbilia Chadema kukidhi uroho wake wa kushika madaraka Na lazima wakubari watanzania giliba wameziona Na kukataa.
Waendelee kunyukana lakini wenyewe kwa hiyari zao wameamua kujipiga dole Na sasa wanataka kutushirikisha kujua linanukiaje.
 
Babu kashusha nondo. Na leo nimefahamu hazina ya wazee iliyopo upinzani. M
zee anajenga hoja huku akiongozwa na takwimu. Prof avuliwa nguo na kuinamishwa
Hana cha nondo wala nini! Tatizo ni ndumakuwili huyo Mzee. Sasa sijui yupo CUF au CDM?? Achana Kabisa na Profesa Lipumba!! CUF is finished under Seif Sharif Hamad. MTU gani wa kushindwa Urais Mara 5 !! Kila siku yeye tu hakuna wengine na safari hii alipoona hali mbaya akaamua kutunga matokeo na kujitangaza! Shame!!
 
Namba 22. "Akili za Watanganyika zimefinyangwa kwa miaka 50 kama unga wa chapati" hapa nakubaliana nae.
Kabisa
Nimesoma nikajisikia uchungu sana lakini haikunifanya nipingane na alichokisema.
Wazanzibar wametuzidi sana katika kujielewa.
Wana msimamo na umoja tofauti na sisi unafiki na uroho vimetuzidi.
 
Hapa ndio tofauti ya wazanzibar Na watanganyika inapoenekana. Wanzibar nje ya Zanziba wanakuwa pamoja.

Hoja za Duni zinawakuna waliojua Siasa baada ya Lowasa Na gia za angani. Babu Kama hajui Leo mchango wa Lipumba Na Slaa basi pasi nashaka Siasa Ni uongo Na ulaghai.
Babu duni akumbuke kauli zake mwenyewe Na serikali Yao ya kitaifa Na namna wananchi walivyochoka CCM kabla ya uchaguzi.
Lipumba wanamtumia Kama kafala Yao lakini Duni ndiye aliyevunja serikali ya kitaifa Zanzibar kwa kuwa kigeugeu Na haki ya mungu Kama Lipumba anatumika basi Na Babu duni anatumika the same way.
Babu duni alikimbilia Chadema kukidhi uroho wake wa kushika madaraka Na lazima wakubari watanzania giliba wameziona Na kukataa.
Waendelee kunyukana lakini wenyewe kwa hiyari zao wameamua kujipiga dole Na sasa wanataka kutushirikisha kujua linanukiaje.
Kama huelewi jambo ni bora kunyamaza na kujifunza. Duni hajaenda Chadema kwa uroho bali ni makubaliano ya vyama kukidhi matakwa ya sheria mbovu ya uchaguzi. Huyo Lipumba hata siwezi kumsema maana hata watoto wadogo wameshamuona ni babu jinga tuu. Ni mtu wa aina gani huyu ambaye anachafua CV yake ya kisiasa aliyoijenga miaka mingi kwa kukubali kutumika?
 
Hana cha nondo wala nini! Tatizo ni ndumakuwili huyo Mzee. Sasa sijui yupo CUF au CDM?? Achana Kabisa na Profesa Lipumba!! CUF is finished under Seif Sharif Hamad. MTU gani wa kushindwa Urais Mara 5 !! Kila siku yeye tu hakuna wengine na safari hii alipoona hali mbaya akaamua kutunga matokeo na kujitangaza! Shame!!
Lipumba ana lipi la kusea niachane nae kabisa? yeye kashindwa urais mara ngapi? Hoja ipi ya Juma Duni unaikataa? Tumia akili ktk kujadili hoja
 
kuna watu wanadhani mafanikio ya cuf au Cdm yalikuja miezi miwili ya mwisho , na si jitihada ya kila chama , mikutano waliofanya, na kuhamasisha watu kujiandikisha pamoja na Ccm kuchokwa hasa kwenye rushwa kila kona , serikali za mitaa mbona Cuf na Cdm walifanya vizuri tu chini ya viongozi wao wa asili
kulikuwa kuna haja gani lowasa kuletwa wakati wagombea walikuwepo wenye sifa, na je baada ya kusaini makubaliano je yaliheshimiwa hasa yale ya kuachiana majimbo je yaliheshimiwa? matatiro alikosa jimbo je mr. duni hilo halikuumizi kama kiongozi wa juu wa chama .
ni ujinga kwa mwanafunzi aliyejiandaa na mtihani kisawa sawa kwa bahati nzuri /mbaya mtihani ukavuja kapata alama 42 halafu akajisifia kuwa hayo ni mafanikio . kwangu mim naona CUF walitakiwa wafanye vizuri zaidi ya hapo kwa kuwa ccm ilikuwa taabani na wanapaswa wajilaum wenyewe kwa hilo

Kwa tume ipi ya UCHAGUZI!? Ilichukua wiki na zaidi kuyatangaza Matokeo ya mshindi wa ubunge kinondoni huku watu wakiwa taabani kwa virungu na mabomu ya machozi ya Polisi.

Jee umeyasahau ya mbagala na kwa kingwendu!!???

CUF na upinzani watafanya vizuri zaidi siku Tanzania itakapopata tume huru ya UCHAGUZI na katiba mpya.
 
Siku hizi sipendi kusikia wala kusoma habari ya Prof. Mapumba, maana amekuwa kielelezo cha UJINGA.
Asante Mzee Duni kwa hoja zako makini, iko siku ccm itakuja kufa tu! Innalilaah Maaswabirina!
 
be the first to replay..yani niko baa na pombe yote imekata kwa hizi nondo 28 takatifu kutoka kwa babu duni
Msiwe mnataja taja bar hapa.Ona sasa umenipa mzuka wa kupiga masanga.Ngoja niende zangu junction pale nikapige zangu mbili tatu..Dhambi hii ya kunywa pombe itakuwa juu yako
 
Mpaka Leo hatuna mshauri Wa uchumi anayewasaidia watu mbalimbali nchini,Lipumba angejenga consultancy kubwa ya kiuchumi ambayo ningekuwa inashauri Governmental na non Governmental na non Governmental organi za nje na ndani na nje ya nchi,achilia mbali watu binafsi,angekuwa anafanya seminar mbali mbali ndani na nje ya nchi,angekuwa pia anaandika vitabu na kuviuza kwa watu mbalimbalj,Lipumba angekuwa millionaire na angekuwa na repute kubwa,nadhani angekuwa kama Kiyosaki kwa bongo hii,siasa imepoteza hadhi na heshima ya Lipumba,Leo hii teja ana heshimika kuliko Lipumba amepoteza followers wengi Sana aliokuwa anawashawishi kwa elimu aliyonayo
 
IMG_4724.jpg


UTANGULIZI.

Na. Juma Haji (Juma Duni Haji)

Chama cha CUF kimeingizwa kwenye kile kinachoitwa mgogoro wa uongozi kwa kisingizio kwamba eti Maalim Seif anataka kukiuza chama hicho kwa chama cha CHADEMA. Profesa. Lipumba ni mtaalam wa uchumi na hesabu, na ndiyo silaha kubwa katika kufanya uchambuzi wa masuala ya kiuchumi. Kwa mtu kama mimi na wale tuliokwenda shule pamoja naye hapo chuo kiku cha Dar es salaam hatuwezi kukubali hoja kama hizi kutolewa na mtu anaeitwa Profesa wa uchumi.

Kwa kweli ni aibu. Sasa nimeelewa kwa nini yule babu wa Arusha aliweza kuwahadaa watanganyika wote wakiwemo viongozi wakuu wa serikali, kwa kusema amepata dawa ya kila maradhi kwa kuwanywesha maji ya mti wa ajabu. Sasa si shangai vipi wananchi wenye u-albino wamekua wakiuliwa, kwa baadhi ya wananchi kuamini kwamba wanaweza kupata utajiri, na mwisho sasa sishangai vipi baadhi ya wananchi walikua wanakamatwa na kuchunwa ngozi kwa kudhani tu kwamba ngozi hiyo ikifanyiwa matambiko unapata utajiri.

Inasikitisha sana kwamba baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru bado hatuko huru, hatuja zinduka na hatujaweza kujitambua na kujikomboa. Tujipime kwa kujiangalia tulivyofanikiwa kwenye chaguzi huko nyuma, tuone kwamba hoja hii ya kuuzwa chama cha CUF kwa chadema inasimama vipi.

1. Profesa akiwa ndiye Mgombea Urais wa chama cha CUF mwaka 2010, alipata kura za urais 695,667 sawa na asilimia 8.28% na Dr. Slaa wa Chadema alipata 2,271491 sawa na asilimia 27.05% . Mwaka huo hapakua na ukawa na wala hakukuwa na ushirikiano wa vyama.

2. Mwaka 1995 na 2000, Chadema hawakuweka Mgombea urais na kura tulizopata CUF ni, 418,973 1995 na mwaka 2000 tukapata kura 1,329,077, sawa na 6.43% na 16.5%. Miaka 10 hiyo tulikosa hoja ya msingi ili kupata kisingizio cha kuwalaumu wazanzibari au chadema. Muda wote kisingizio chetu ni dola ya CCM kutofanya uchaguzi huru na wa haki.

3. Uchaguzi wa 2005 tukapata kura 1,327,125 sawa na 11.68 % takriban sawa na zile za uchaguzi wa 2000. Katika uchaguzi wa 2010 tukafanya vibaya sana na kura zetu kushuka hadi 695,667 takribani sawa na zile za 1995.
4. Baada ya miaka 20 kushiriki uchaguzi chini ya uongozi wa miaka 15 ya Profesa. Lipumba na mara zote akiwa ni mgombea wetu wa urais tunapata kura chache. Uchaguzi huo wa 2010, pia hatukupata hoja ya kuwasingizia wazanzibari kukiuza chama kwa chadema.

5. Si mara moja wala mbili Profesa. amesikika akisema kwenye misikiti kwamba kwa makusudi waliamua kumuachia Mhe. Kikwete ili ashinde eti kwa sababu ni Muislam mwenziwawo wa Tanganyika. Mwisho wa mwezi wa Novemba 2016 Sheikh. Khalifa Khamis wa msikiti wa Mtoro amelalamika sana juu ya uonevu unaofanyiwa wa-Islam na jinsi walivyokua wameendelea kukibeba chama hicho (CCM) katika chaguzi zote. Alisema kwamba bila waislam wa CCM , chama hicho mwaka 2015 kilikua ICU, yaani chumba cha wagonjwa mahtuti. Kama si fyokofyoko za Lipumba si ajabu kingeondoka madarakani mwaka huu 2015.

6. Badala ya kuuweka wazi ukweli huo, Profesa. anasingizia ukawa ndio uliokikosesha ushindi chama cha CUF huku akijua kwamba yeye ndiye muanzilishi wa Ukawa na jina hilo limeasisiwa na yeye binafsi kwenye kikao cha umoja wa wabunge wa Bunge la Katiba hapo kwenye ukumbi wa Msekwa Dodoma. Ni Profesa akiwa mwenyekiti wa ushirikiano huo aliyeweka saini makubaliano ya pamoja juu ya kuweka mgombea mmoja wa Urais kwenye uchaguzi wa 2015. Ulipofika wakati wa mgombea mmoja awe siye yeye ndipo akaanza kusingizia nafsi kumsuta.

7. Katika hali ya kuonekana ni mwenye uchungu na hasira juu ya kuvurugwa kwa Bunge la katiba alitoa hotuba ya kuwashawishi wabunge wa upinzani wa bunge hilo kutoka kwenye bunge hilo kwa msingi kwamba tukishiriki, tutakua tunahalalisha katiba ya CCM chini ya kivuli cha Bunge la katiba. Hali ya mjadala wa bunge hilo ulivyotawaliwa na ubaguzi wa kidini na kikanda na asili za watu Profesa. alichukia na kuwaita CCM ni wabaguzi kama wale wa Ruwanda walioitwa Ntarahamwe. Hotuba zake hivi sasa ni tafauti kabisa ya zile za Bunge la katiba. Kumbe wakati akisema yale yeye mwenyewe ni mmoja ya CCM aliyevaa ngozi ya kondoo. Kutushawishi kututoa ilikua ni agizo la CCM ili CCM wapate nafasi kufanya watakavyo katika kupindua maoni ya wananchi ya Tume ya Mzee warioba. Hivyo yeye ni ntarahamwe kupita CCM. Kwa nini sasa anafanya hivi nitaeleza baadae.

8. Hoja ya kuuzwa chama anayoitumia kukiuwa chama hiki (CUF) ni ya kushangaza maana siku tulipokwenda kumuona nyumbani kwake kabla hajajiuzulu, mimi na Maalim Seif, yeye alikua mbioni anakimbilia kumfuata Mr. Mbatia ili kukamilisha mazungumzo ya kumleta Lowassa, kwenye upinzani na ni yeye aliependekeza kwetu kwamba Mzee Lowassa ajiunge na aidha NCCR au Chadema na kwamba CUF imuunge mkono. Sisi tulikubaliana nae baada ya kutushawishi kwa takwimu alizotueleza kwamba amepewa na wazee wa chadema kwamba akija Mzee Lowassa tutashinda kwa asilimia 60 au zaidi.

9. Ni vizuri kujiuliza kwa kigezo gani cha msingi au cha kitaalam cha Ukawa na au kuja kwa Lowassa alichonacho Profesa, kumlaumu Maalim kwamba ndiye kisirani wa kutaka kukiuza chama cha CUF kwa Chadema?

10. Chama cha CUF 2010 kiliweka wagombea katika majimbo 132 huko bara, ambayo yalikua na jumla ya kura 6,002,623. Katika majimbo hayo tulipata kura za wabunge 639,402 sawa na 10.65% ya kura hizo.

11. Mwaka 2015, tumeweka wabunge katika majimbo 86 tu, 2, ya zamani na 50, tuliyopewa na Ukawa. Ziada ya majimbo 34 ni yale tuliyoweka wenyewe, 25 katika hayo tulipambana na CCM bila chadema wala NCCR. Jumla ya kura za majimbo hayo 86 ni 4,398,666 , kati ya kura hizo, CUF tulizopata ni 1,112,246 sawa na 25.29%. Majimbo machache chini ya ushirikiano tumepata kura nyingi, kuliko majimbo mengine tulipokua peke yetu chini ya uongozi wa Profesa. Wingi huu wa kura kutoka 695,667 hadi 1,112,246 hakuwezi kabisa kutafsirika kwamba chama kimeuzwa , wingi huu umetuongezea ruzuku kwa zaidi ya shs. 11 milioni kuliko ile ya 2010 tulipokua peke yetu.

12. Siamini na nitakua nahitaji kikombe cha babu wa Lolipndo, kwamba kupata kura nyingi ni kukiuza chama. Hoja hii ni dhaifu maana kama chama ni kukiuza basi pale alipotuacha Profesa katikati ya maandalizi ya uchaguzi ilikua ni kukiuza chama au kukiuwa,? Na yeye akijua kwamba anakiuwa, lakini pamoja na wazee kumbembeleza alituacha tufe.

13. Vipi chama kinasemwa kimeuzwa wakati chini ya ukawa tumeongeza wabunge kutoka 2 Tanzania bara hadi 10, na kupata madiwani kutoka 152 tukiwa peke yetu hadi 285, tumepata Halmashauri 5, manaibu Meya 3, ushindi ambao hatujawahi kuupata kwa maisha yote ya chaguzi tulizoshiriki peke yetu chini ya uongozi wa Profesa.

14. Chini ya ukawa tumeshinda Urais wa Zanzibar, tumeongeza majimbo kisiwa cha unguja kutoka 2, hadi 10 na kuiweka CCM kukataa kutoa Serikali na hivyo kupindua ushindi wetu fawahisha.

15. Tungetegemea Profesa afurahie matunda haya hasa yale ya kushinda uchaguzi huo huko Zanzibar. Cha ajabu badala ya kushiriki kupambana tupewe serikali yetu ya CUF Zanziba yeye anapinga tusipewe na anakubali kumtambua Dr. Muhammed Shein eti kumkomoa Maalim Seif .

16. Suala ni Je, kweli Profesa alikua mwanachama wa kweli kwa miaka yote hii 16 ya uongozi wake au alikua ni pandikizi lililopewa kazi maalum kuhakikisha kwamba CUF haishindi na wala haipewi Serikali? Tulishindwa kumjua kwa sababu alikua hajapata majaribu katika uongozi wake. Pale maslahi yake yalipopata mtihani akajidhihirisha mwenyewe kwa kuchukua hasira za kujiuzulu, pamoja na kuombwa asifanye hivyo wakati huo wa uchaguzi.

17. Hulka ya binaadam ni kwamba unapompa uongozi ndipo hujidhihirisha alivyo, si kwamba hua amebadilika. Hivyo ndivyo alivyojidhihirisha Profesa Lipumba kwamba kumbe hakua mwenzetu zamani sana.

18. Profesa alipotuachia chama wakati wa maandalizi ya uchaguzi aliamini kabisa kwamba tutashindwa kusimama na hivyo kupata hoja ya kutusuta pale tungeshindwa vibaya katika uchaguzi huo. Muungu alitulinda kwa sababu nia zetu anazijua yeye.

19. Baada ya kuona chama hakikufa ndipo akatumwa tena kuja kukimaliza kiwe hakipo kabisa. Maana suala la kujiuliza ni tangu lini Profesa awe rafiki na Polisi. Tangu lini Profesa atumie uchochezi wa lugha za CCM katika kugombanisha wafuasi wake wa CUF kwa kutegemea eti ndo anarudi kukijenga? Utakujaje kujenga chama kwa kukigawa pande mbili. Kwa nini utumie nguvu za dola ambayo ndiyo adui wetu mkubwa kutaka kurudi kwenye uongozi wa chama ulioukataa mwenye? Wapi duniani penye mfano wa kiongozi mnafiki kama huyu, kuacha uongozi kwa hiari yake na akaondoka kwenye kiti chake hicho kwa mwaka mzima na hapo tena akazinduka kwamba anafuta uamuzi huo. Haijapata kutokea labda uwe umekunywa kikombe cha babu wa Loliondo.

20. Katika uachaji wake wa uongozi hivyo tulitakiwa tusubiri muda gani mpaka tukubali kwamba sasa Profesa hayupo kwenye kiti chake hicho. Je, tulikua tungojee miaka minne au mitatu au hadi mwaka mmoja kabla uchaguzi mkuu wa 2020 ndipo tuamini kwamba sasa Profesa hayupo tena kwenye kiti chake.

21. Ni aibu, na ndiyo maana nikasema tunahitaji kikombe cha babu, maana ilivyotarajiwa hivi sasa tuwe tunaimarisha chama chetu kujiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Badala yake leo CUF chama chenye nguvu, tupo mahakamani tunagombanishwa wenyewe kwa wenyewe huku CCM imekaa pembeni inachochea na kutucheka.

22. Katika hali hii watanganyika mujitambue kwamba munasafari ndefu sana ya kujikomboa, maana akili zenu zimefinyangwa kwa miaka 50 kama unga wa chapatti, hadi kuamini kwamba shida zenu ndiyo raha ya maisha yenu. Na ufakhari wa kijana wa Tanganyika ni ubabe na matusi, kama vile walivyo viongozi wa CCM na vijana wao. Badala ya kuona aibu kwa tabia hizo Profesa mzima nae anaona hiyo ni sifa. Ninasema haya kwa ushahidi wa Takwimu.

23. Nimepitia matokeo ya chaguzi za Jamhuri ya Muungano tangu hapo 1995 na kuangalia vipi vyama vya upinzani kwa jumla vilivyofanikiwa. Katika kipindi chote hicho ushindi wa vyama vya upinzani wakiwa mmoja mmoja na kwa pamoja hauja fikia asilimia 30 (30%) ya ushindi wa chama cha CCM.

24. Uchaguzi wa 2015 tulipojiunga vyama vine katika mazingira magumu ya mfumo uliopo tumeweza kupata asilimi 40, (40%) ya kura za Rais ambazo ni sawa na asilimi 68.3% ya kura za urais za CCM. Hii ni dalili njema. Pia vyama viwili hivi vimeweza kupata asilimia 44. 5 (44.5%) ya viti vya CCM.

25. Takwimu hizi zinatuambia kwamba kama lengo ni kuiondoa CCM madarakani basi tukiungana pamoja wapinzani, CCM inaondoka 2020 , hata kama itatumia nguvu za dola.

26. Hii ndiyo moja ya sababu kubwa za kutumiwa Profesa kuuwa CUF ili kuuwa ukawa. Hivyo Profesa hakuja kujenga chama cha CUF ametumwa kukamilisha kazi kabla 2020. Mialiko ya kuitwa Ikulu mara baada ya uchaguzi na kesi zake kufutwa ghafla ni sehemu ya utamu wa kutiwa bei.

27. Hivyo asitafutwe mchawi na kupakana matope yasiyo mvua, Profesa tangu awali alikuja CUF kama afisa mwenye kazi maalum, kutumung’unya ndani kwa ndani kama dumuzi la gunia la mahindi, maana muda wote dalili zikionesha kwa wepesi wake ndani ya chama.

28. Wakati ulipofika amejidhihirisha mwenyewe kwa kupoteza imani ya wanachama. Imani ikishapotea hairudi. Hakuna tena atakaeamini kwamba akiongoza CUF hatoacha tena kabla uchaguzi mkuu 2020. Profesa amerudi kukimaliza chama siyo kukijenga. Asionewe Maalim Seif. CCM si mjinga wa kumjenga Profesa kwa matumaini kwamba amuachie serikali ya CCM 2020. Hizo ni ndoto za alinacha. Profesa akimaliza kazi ya kukiuwa CCM hawana habari nae kama vile wasivyo na habari na wale waliotumika huko nyuma ndani ya chama hiki.

Ahsante sana.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]: Imenukuliwa kutoka kwa Mjelajela [HASHTAG]#Juma[/HASHTAG] Duni Haji, Ni Elimu kubwa sana kwa watafutao maarifa….
Maneno meeengi mpaka cjamaliza kusoma ila ww utakua ndio waleee
 
Siku hizi sipendi kusikia wala kusoma habari ya Prof. Mapumba, maana amekuwa kielelezo cha UJINGA.
Asante Mzee Duni kwa hoja zako makini, iko siku ccm itakuja kufa tu! Innalilaah Maaswabirina!
Hayo utajua mwenyewe kwanza lipumba hajui kama kuna mtu anaitwa Mapuma miyoga
 
Anayemshabikia Lowasa akapimwe akili ------Msigwa


Ni heshima kwa Mungu kumzomea fisadi Lowasa -------Lema


Kwa nini vibaka wanafungwa na kumuacha fisadi Lowasa akikamua mtaani?? --------Mbowe


Kama Lipumba ni pandikizi, basi lema, msigwa na Mbowe ni mababu wa mapandikizi duniani.

Babu duni anza na hao jamaa kwanza kuwanywesha kikombe cha loliondo
 
Back
Top Bottom