Hofu yatanda ujenzi wa bandari Bagamoyo

Hofu yatanda ujenzi wa bandari Bagamoyo

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,262
Reaction score
18,713
[h=2]
Ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, umezua hofu miongoni mwa watumishi wake, kuwa watapoteza kazi kwa kile kinachoelezwa kuwa ujio wa mradi huo.

Lakini pia bandari hiyo inatafsiriwa kama ‘kiama’ cha bandari kongwe zilizopo jijini Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Kazi hiyo itakayofanywa kwa mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni 16 (Dola bilioni 10 za Marekani), unagharamiwa kwa asilimia 100 na serikali ya China.

Fedha hizo ni sawa na bajeti ya serikali kwa mwaka huu wa fedha wa 2013/2014.

Wafanyakazi wa bandari hiyo waliokataa kutaja majina yao walipozungumza na NIPASHE Jumamosi, wanaitaka serikali iwaondolee hofu kutokana na taarifa zinazoeleza kuwa mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo, unakataza kuwapo kwa bandari nyingine zinazoshindani nayo.

“Kipengele kimojawapo cha mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, kinasema kwa umbali wa kilometa 200 za mraba kusini, mashariki, magharibi na kaskazini hakutaruhusiwa kuwapo na bandari ya namna hiyo wala kuendeleza bandari ya namna hiyo,” kinaeleza chanzo chetu.

Chanzo hicho kinasema, “bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara hazitapanuliwa, kuboreshwa wala kuendelezwa ili kutoa nafasi kwa bandari ya Bagamoyo kuwa ya kwanza kwa ubora na bila kuwa na mshindani kwa kipindi cha miaka 50.”

Msemaji huyo anaungwa mkono na mwingine aliyesema, wanaomba serikali iwaeleze ukweli na kuwaondolea hofu, kwa maana hawajajua hatima yao kutokana na mikataba hiyo kufichwa.

UPANUZI GATI namba 14 KUSIMAMISHWA

Wakielezea hofu yao zaidi juu ya mkataba unaokataza upanuzi wa bandari kwenye eneo la kilometa za mraba 200, walisema upanuzi wa gati au (lango) namba 14 katika bandari ya Dar es Salaam umesimamishwa au utasimamishwa mara moja.

Hatua hiyo itachukuliwa ili kuipa ama kuheshimu na kulinda mkataba wa Wachina kwa ajili ya bandari ya Bagamoyo.

WACHINA KUIENDESHA MIAKA 50

Wafanyakazi hao walisema walidokezwa na maofisa wa serikali waliouona mkataba huo kuwa Wachina watapata `ulaji’ unaowaruhusu kufanyakazi ya kuendesha bandari hiyo na kuimiliki kwa miaka 50 baada ya ujenzi kukamilika.

Walisema habari za ndani kutoka vyanzo vya serikalini kuhusu baadhi ya mikataba 16 iliyosainiwa na Rais wa China Xi Jinping, mwezi uliopita wakati alipoizuru Tanzania.

Zilibainisha kuwa ujenzi wa bandari hiyo una masharti magumu ambayo ni pamoja na kufanikisha mradi wa bandari ya Bagamoyo, Tanzania itachukua mkopo wa fedha na vifaa kutoka China.

Mkataba huo vyanzo, viliwaambia wafanyakazi hao kuwa unasisitiza kuwa ujenzi utafanywa na kampuni ya China na wahandisi wake watapewa jukumu la kujenga bandari hiyo pasipo kupitia zabuni.

“Serikali ya China ndiyo itakayoendesha bandari hiyo kwa muda wa miaka 50 kuanzia hapo itakapokamilika ili kurudisha fedha za mkopo zizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo .”

Wafanyakazi hao walisema chanzo kiliwadokeza kuwa, China italazimika kuendesha bandari ili kujirudishia fedha zake za mkopo ilizotoa.

“Lakini inashangaza kwa sababu hakuna kipengele kinachoeleza kuwa endapo watajirudishia mkopo wao na riba kabla ya miaka 50, watarejesha bandari hiyo mikononi mwa serikali,” kilisema na kuongeza kuwa inawezekana fedha hizo zikarudishwa hata kabla ya muda uliowekwa.

Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, anajiweka kando na kutoa ufafanuzi za suala hilo, akimuachia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA).

Dk Mwakyembe hakupinga wala kuzikataa hofu za wafanyakazi wa TPA.

ZIARA YA JINPING
Rais wa China Jinping akiwa nchini mwezi uliopita, alisema China imetenga Dola bilioni 20 za marekani kuisaidia Afrika na kwamba itakuwa na ushirikiano wa ulinganifu na wa manufaa kwa pande husika.

Akasema hakutakuwa na masharti magumu kama ambavyo nchi tajirii zimekuwa zikiilazimisha Afrika kuyafuata.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanapingana na hatua ya China na kueleza kuwa hiyo ni janja ya kuiingia Afrika na pale itakapofanikiwa kupenya, itakuwa na ukandamizaji na ubeberu utakaowaumiza Waafrika kuliko ule wa ukoloni mkongwe.

BANDARI YA BAGAMOYO KATIKA MITANDAO
Kwa mujibu wa mikataba 16 iliyosaibiwa baina ya Rais Jakaya Kikwete na Rais Jinping wa China, bandari hiyo itagharimu Dola bilioni 10 (sawa na Shilingi trilioni 16).

Taarifa hii imo kwenye tovuti za Tanzania, About Tanzania, Tanzania Investment Economic and Business News Interviews Reports Consulting na Military News Humor Photos - StrategyPage

Mitandao inawakariri maofisa wa Tanzania wakisema, China itawekeza zaidi ya Dola milioni 800 kujenga miundo mbinu itakayousukuma mbele uchumi wa taifa hili.

Kwa upande wa bandari ya bandari ya Bagamoyo inatarajiwa kukamilika 2017.

Chini ya makubaliano hayo ya Tan-cino (Tanzania na China) kutakuwa na mikataba mingine ya kukopa itakayofanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya China ya kuuza ng’ambo na kuagiza bidhaa nje.

Pia kuna mikataba ya kuanzisha viwanda vya kisasa, kanda za kiuchumi za kilimo na kufunguliwa kituo cha utamaduni na mila za watu wa China.

Makala haya yameandikwa na Gaudensia Mngumi, kwa msaada wa mtandao.

CHANZO: NIPASHE

​

​
​
[/h]
 
2015 sanduku la kura ndio mkombozi wako.
 
Ndio hapo sasa... Tulimchagua KIKWETE sababu ni KIJANA angalia anavyopeleka mali zote za kiujana BAGAMOYO - Kwani NYERERE alishindwa? Kwani MWINYI alishindwa au Mkapa alishindwa na MTWARA wana GAS???
 
Mkuu walikuwa wanasema rais ni handsome. Kazi tunayo
 
Huu mkataba ni mtego maridadi kwa mwalimu wa sheria Mwakyembe.
Halafu kaingia mwenyewe bila kulazimishwa.、
 
Hakuna kitu cha bure. Hata reli ya tazara ilijengwa ili kusafirisha makaa ya mawe... Hakuna mpuuzi atakayekupabpesa zake kiholela bila kuona faida mbele
 
KM za mraba 200 ndo zitafika mtwara na Tanga? Hata sidhani kama Bandari ya Dar itakua ndani ya eneo hilo kwani hapa tunaongelea kakipande ka eneo lenye Km zisizofika 15 kwa 15 kusini, kasikazini, magharibi, na mashariki.

Kinachotakiwa hapa ni ufanisi. Kama bandari ya Dar watakua na ufanisi basi wataendelea kuexist. Kama hawatakuwa na ufanisi watapotea.
 
bunge la mwaka 2015 litafuta kila kitu tuwe kama zimbabwe
 
Kwani hela tunapewa ama tunakopeshwa? Manake masharti nilidhaninyanapaswa kuwa juu ya ulipaji zaidi. Sasa kama hawataki bandari zingine ziendelezwe maana ya kujenga bandari mpya ni nini?

Mbona kama tunaingia mikataba ya kichawi sasa?
Hakuna kitu cha bure. Hata reli ya tazara ilijengwa ili kusafirisha makaa ya mawe... Hakuna mpuuzi atakayekupabpesa zake kiholela bila kuona faida mbele
 
Nashangaa wiki ya 3 sasa sijamsikia MBUNGE HATA MMOJA AKIHOJI MIKATABA YA TANZANIA NA CHINA,NA ILE YA TANZANIA NA CANADA KULE AMBAKO MKULU ALIPANDISHWA FARASI
 
Kwani hela tunapewa ama tunakopeshwa? Manake masharti nilidhaninyanapaswa kuwa juu ya ulipaji zaidi. Sasa kama hawataki bandari zingine ziendelezwe maana ya kujenga bandari mpya ni nini?

Mbona kama tunaingia mikataba ya kichawi sasa?

some time naona bora ya chief MANGUNGO
 
Oooo jamani prezidaa anamadaraka makubwa sana tumpunguzie jamaanai tutauzwa woote
 
Ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, umezua hofu miongoni mwa watumishi wake, kuwa watapoteza kazi kwa kile kinachoelezwa kuwa ujio wa mradi huo.

Lakini pia bandari hiyo inatafsiriwa kama ‘kiama' cha bandari kongwe zilizopo jijini Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Kazi hiyo itakayofanywa kwa mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni 16 (Dola bilioni 10 za Marekani), unagharamiwa kwa asilimia 100 na serikali ya China.

Fedha hizo ni sawa na bajeti ya serikali kwa mwaka huu wa fedha wa 2013/2014.

Wafanyakazi wa bandari hiyo waliokataa kutaja majina yao walipozungumza na NIPASHE Jumamosi, wanaitaka serikali iwaondolee hofu kutokana na taarifa zinazoeleza kuwa mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo, unakataza kuwapo kwa bandari nyingine zinazoshindani nayo.

"Kipengele kimojawapo cha mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, kinasema kwa umbali wa kilometa 200 za mraba kusini, mashariki, magharibi na kaskazini hakutaruhusiwa kuwapo na bandari ya namna hiyo wala kuendeleza bandari ya namna hiyo," kinaeleza chanzo chetu.

Chanzo hicho kinasema, "bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara hazitapanuliwa, kuboreshwa wala kuendelezwa ili kutoa nafasi kwa bandari ya Bagamoyo kuwa ya kwanza kwa ubora na bila kuwa na mshindani kwa kipindi cha miaka 50."

Msemaji huyo anaungwa mkono na mwingine aliyesema, wanaomba serikali iwaeleze ukweli na kuwaondolea hofu, kwa maana hawajajua hatima yao kutokana na mikataba hiyo kufichwa.

UPANUZI GATI namba 14 KUSIMAMISHWA

Wakielezea hofu yao zaidi juu ya mkataba unaokataza upanuzi wa bandari kwenye eneo la kilometa za mraba 200, walisema upanuzi wa gati au (lango) namba 14 katika bandari ya Dar es Salaam umesimamishwa au utasimamishwa mara moja.

Hatua hiyo itachukuliwa ili kuipa ama kuheshimu na kulinda mkataba wa Wachina kwa ajili ya bandari ya Bagamoyo.

WACHINA KUIENDESHA MIAKA 50

Wafanyakazi hao walisema walidokezwa na maofisa wa serikali waliouona mkataba huo kuwa Wachina watapata `ulaji' unaowaruhusu kufanyakazi ya kuendesha bandari hiyo na kuimiliki kwa miaka 50 baada ya ujenzi kukamilika.

Walisema habari za ndani kutoka vyanzo vya serikalini kuhusu baadhi ya mikataba 16 iliyosainiwa na Rais wa China Xi Jinping, mwezi uliopita wakati alipoizuru Tanzania.

Zilibainisha kuwa ujenzi wa bandari hiyo una masharti magumu ambayo ni pamoja na kufanikisha mradi wa bandari ya Bagamoyo, Tanzania itachukua mkopo wa fedha na vifaa kutoka China.

Mkataba huo vyanzo, viliwaambia wafanyakazi hao kuwa unasisitiza kuwa ujenzi utafanywa na kampuni ya China na wahandisi wake watapewa jukumu la kujenga bandari hiyo pasipo kupitia zabuni.

"Serikali ya China ndiyo itakayoendesha bandari hiyo kwa muda wa miaka 50 kuanzia hapo itakapokamilika ili kurudisha fedha za mkopo zizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo ."

Wafanyakazi hao walisema chanzo kiliwadokeza kuwa, China italazimika kuendesha bandari ili kujirudishia fedha zake za mkopo ilizotoa.

"Lakini inashangaza kwa sababu hakuna kipengele kinachoeleza kuwa endapo watajirudishia mkopo wao na riba kabla ya miaka 50, watarejesha bandari hiyo mikononi mwa serikali," kilisema na kuongeza kuwa inawezekana fedha hizo zikarudishwa hata kabla ya muda uliowekwa.

Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, anajiweka kando na kutoa ufafanuzi za suala hilo, akimuachia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA).

Dk Mwakyembe hakupinga wala kuzikataa hofu za wafanyakazi wa TPA.

ZIARA YA JINPING
Rais wa China Jinping akiwa nchini mwezi uliopita, alisema China imetenga Dola bilioni 20 za marekani kuisaidia Afrika na kwamba itakuwa na ushirikiano wa ulinganifu na wa manufaa kwa pande husika.

Akasema hakutakuwa na masharti magumu kama ambavyo nchi tajirii zimekuwa zikiilazimisha Afrika kuyafuata.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanapingana na hatua ya China na kueleza kuwa hiyo ni janja ya kuiingia Afrika na pale itakapofanikiwa kupenya, itakuwa na ukandamizaji na ubeberu utakaowaumiza Waafrika kuliko ule wa ukoloni mkongwe.

BANDARI YA BAGAMOYO KATIKA MITANDAO
Kwa mujibu wa mikataba 16 iliyosaibiwa baina ya Rais Jakaya Kikwete na Rais Jinping wa China, bandari hiyo itagharimu Dola bilioni 10 (sawa na Shilingi trilioni 16).

Taarifa hii imo kwenye tovuti za Tanzania, About Tanzania, Tanzania Investment Economic and Business News Interviews Reports Consulting na Military News Humor Photos - StrategyPage

Mitandao inawakariri maofisa wa Tanzania wakisema, China itawekeza zaidi ya Dola milioni 800 kujenga miundo mbinu itakayousukuma mbele uchumi wa taifa hili.

Kwa upande wa bandari ya bandari ya Bagamoyo inatarajiwa kukamilika 2017.

Chini ya makubaliano hayo ya Tan-cino (Tanzania na China) kutakuwa na mikataba mingine ya kukopa itakayofanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya China ya kuuza ng'ambo na kuagiza bidhaa nje.

Pia kuna mikataba ya kuanzisha viwanda vya kisasa, kanda za kiuchumi za kilimo na kufunguliwa kituo cha utamaduni na mila za watu wa China.

Makala haya yameandikwa na Gaudensia Mngumi, kwa msaada wa mtandao.

CHANZO: NIPASHE

​

​
​
Kilometa 200 kusini, mashariki, magharibi...!! Mbona huu ni mtaji tosha kwa CHADEMA kwa Wananchi wa LINDI, MTWARA na ZANZIBAR...!!?? Trillion 16 (10 Billion USD) mbona zingemaliza tatizo la umeme na miundombinu kwenye maeneo nyeti ya nchi hii? CHADEMA mpewe nini? Huo ni mradi binafsi aisee BANDARI & LAMI ya kutokea Bagamoyo mpaka Msata...!!
 
wanasubiri bajeti ya nwakyembe mbona analo hilo na serikali si ilisema itaweka mikataba yote wazi lakini mpaka leo sijaona
 
KM za mraba 200 ndo zitafika mtwara na Tanga? Hata sidhani kama Bandari ya Dar itakua ndani ya eneo hilo kwani hapa tunaongelea kakipande ka eneo lenye Km zisizofika 15 kwa 15 kusini, kasikazini, magharibi, na mashariki.

Kinachotakiwa hapa ni ufanisi. Kama bandari ya Dar watakua na ufanisi basi wataendelea kuexist. Kama hawatakuwa na ufanisi watapotea.

you are one of them why should they show the general public those contracts to reduce unnecessary doubts, let us an open government
 
Bandari za Tanga na Mtwara zipo sehemu nzuri sans, ni ujinga kuziacha bila kuziendeleza.
 
Kumbe,Yawezekana kabisa JK anataka kuigeuza Kanda ya Pwani(dar es salaam,pwani na morogoro) kuwa kanda yenye nguvu kubwa kiuchumi hapa Tanzania,Kuna kila dalili.Pwani Bandari kubwa kabisa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Morogoro Kituo kikubwa na cha kisasa kabisa cha Mabasi makubwa ya abiria katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
 
China imetenga USD 20 billion "kuisaidia" Africa, halafu kati ya hizo 10 billion zimeenda bandari ya Bagamoyo?

Serikali kwa kukataa kuweka mikataba wazi inatoa nafasi kwa yeyote kusema chochote na kukipitisha kama ukweli.

Wekeni mikataba wazi.
 
Back
Top Bottom