Hofu yangu Mtwa kwako Mzee Mkapa - part 1

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
Mzee wetu heshima kwako!

Kwanza nikupongeze kwa namna ulivyoweza kuifanya wiki hii kuwa ya kipekee. Tunatambua kuwa tulikuwa kwenye joto la kisiasa hakuna aliyekuwa anaweza kuzalisha habari kuu labda pengine ajali ( Mungu atuepushie) lakini wewe uliweza hongera Sana.

Mkuu leo vijana wote wameachana na upepo wa kisuli suli na ubaharia eti wanajadili kitabu eti kila kijana Ni msoma kitabu jamani heshima kwako mzee wetu.

Mkuu leo utawala wako umekuwa wa mfano, wanakuita Mr clean Tena unaonekana kama hujawahi kukosea hii inastaajabisha. Nitaongea machache mzee wangu yanayofanya niihofu awamu yako iliyotia doa maisha yangu na mengine nitakuja kuyasema nitakapo pata nakala ya kitabu chako.

Mzee wangu chuki yangu kubwa kwako Ni pale ulipofanya ubinafsishaji wa kikatili wa kiwanda Cha karatasi mgololo ndipo chuki yangu dhidi yako ilipo zaliwa. Nilijiuliza kuwa wewe Ni kiongozi wa namna gani kuuza kiwanda, mashamba, makazi na watu.. ukawaacha kwa fedhuri muhindi wasio na muangalizi lakini kitabu chako kimejibu kuwa eti unasikitika baada ya ubinafsishaji uliziba macho yako na kujifanya Kama huoni yanayoendelea huko uliko binafsisha.

Wewe Ni kiongozi wa aina yake kupata kutokea by the way tunamshukuru kijana wako Magufuli kwa kuwakumbuka wazee hawa hata kwa kidogo bila Shaka wewe usingewakumbuka hata mwisho wa dahari. By the way tumeshafukia wazee wetu zaidi ya 300 udongoni wakiwa na hali ngumu kutokana na maamuzi yako na karibu kila wiki tunaendelea kufanya hivyo.

Mzee mkapa uliwezaje kumfanya mstari wa mbele mtu mwenye akili ndogo Kama F. Sumaye? Au ndio mbinu ya kuteua mtu unae mmudu aliyotufundisha Machievel katika kitabu Cha the prince?

Mkuu tukiacha Hilo la Kwanza nilichokiona kwa kitabu chako Ni kuwa utawala wako ulikuwa shamba la Bibi, kila mtu alipiga tuu Tena pengine kwa idhini yako. Hata hizo authorities bodies ilikuwa mipigo tuu ya watu. Leo yule msomi wa WB Daudi Balali uliyemuomba aje ajenge BOT yenye msimamo, tena unaemjua kwa tabia yake ya kutoshiriki ubadhirifu aliyeachia mipigo yote baada ya kuagizwa na wewe na vigogo wako Leo Mkapa pasi na haya unamtaja kuwa alikushauri vibaya? Kama mmemsababishia maisha ya Giza kwanini msimuheshimu kwa hata machache aliyoyafanya.?

Mzee mkapa. Kwanini usimkemee kiongozi wa majambazi aliyekuwa mstari wa mbele eti mlinzi wa raia hawa akatikisa usalama wa Dar es salaam na Morogoro mfanyaji biashara ya silaha?

Mzee Mkapa sijakisoma kitabu chako ila endapo hakitazungumzia kutoweshwa kwa makamu wako wa rais ama kama hakitazungumzia kifo chenye utata Cha kipenzi chetu mzee wetu Kama ambavyo umekuwa na maneno maneno sikuhizi Basi kitabu chako kitakuwa kwangu utenzi kama tenzi nyingine.

By the way enzi yako maisha yalikuwa matamu sana hata RTD na TVT zilikuwa tamu Sana nyakati zile.
 
Hivi hicho kitabu kinapatikana wapi?
Bei yake inakwendaje?

Ova
 
Samahani mkuu, kuna sehem unaeleza kana kwamba umekisoma kitabu wakati huo huo unamalizia kwa kusema hujakisoma kitabu. Hii imekaaje, unaweza kuweka sawa maandishi kama hutajali.
 
Taaluma yake ni Uandishi ingeshangaza asingefanya hichi alichofanya nampa hongera ngoja tukisome ingawa kitakua mengi yamefichwa ila tutapata mawili matatu ya kuongezea kwenye vichwa vyetu
 
Taaluma yake ni Uandishi ingeshangaza asingefanya hichi alichofanya nampa hongera ngoja tukisome ingawa kitakua mengi yamefichwa ila tutapata mawili matatu ya kuongezea kwenye vichwa vyetu
Mimi naulza kwa wale wa Aruah, kitabu hiki kinapatikana duka gani?
 
Back
Top Bottom