Hofu ya mwaka 2006: Serikali, upinzani Vs Wanamtandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya mwaka 2006: Serikali, upinzani Vs Wanamtandao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Jan 21, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika tamko la CHADEMA kuhusu siku 100 za kikwete madarakani, tamko ambalo lilichapishwa katika gazeti hili, Mwenyekiti wa chama hicho Mheshimiwa Freeman au “mtu huru” kama mashabiki wake wanavyo muita siku hizi, alitoa maneno mazito! Mmaneno mazito sana kuhusu dhana nzima ya wanamtandao dhidi ya hatima ya taifa, hatima ya Tanzania!

  Freeman Mbowe alionyesha wasiwasi wake, na wa chama chake dhidi ya kundi hili na kwamba upo wasiwasi kuwa serikali inaongozwa na mifumo miwili inayofanya kazi sambamba, Freeman Mbowe alisema na namnukuu “Kwa upande mwingine CCM kama chama kinaelekea kusogezwa pembezoni na badala yake maamuzi ya msingi kuhusu mwelekeo wa kiutawala yanaelekea kufanywa na kundi ambalo halitambuliki linalojiita ‘wanamtandao’ambalo muundo na kanuni zake haziko bayana hali inayoelekea kuigawa serikali na inaweza kutishia mwelekeo wa usalama wa nchi ambao unapaswa kuongozwa na mifumo ya kikatiba” Alisisitiza kuwa “Inapofika mahala wananchi wanaelezwa kuwa nchi inaongozwa na kundi fulani lisilo fahamika agenda zake, ni hatari kwa usalama wa taifa”.Haya ni maneno mazito sana ambayo kimsingi serikali makini ilipaswa kutolewa ufafanuzi, serikali ilipaswa kuyatolea tamko!

  Hata hivyo, katika hali ambayo haikutarajiwa na watu makini, Tofauti na Freeman, viongozi wengine wa upinzani wanaonekana kutojali hofu hiyo, hofu ya wanamtandao! Lakini ukitumia darubini, utabaini kuwa baada ya kukatwa miguu wote wasio amini katika ‘uwanamtandao’ ndani ya CCM, hapana shaka kazi ya wanamtandao itabaki moja tu! Kukata miguu vyama vya upinzani.

  Na hiyo ndio Hofu ya Freeman! Hofu ya Wanamtandao!!

  Habari kamili bonyeza hapa: Hofu ya Wanamtandao! Kikwete, Mbowe Roho Juu!

  Asha
   
 2. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuwataja kwenye orodha ya mafisadi, Mwenyekiti wetu Kikwete kuwaondoa sasa hasira zote wamehamishia CHADEMA, mtakoma mwaka huu. Mara Mbowe akimbizwa na mapanga Tarime, mara waislamu hawataki Sangara. Kwisha habari yetu


  .......ndiyohiyo
   
 3. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wakati watu wanaongelea vitu vyenye masirahi ya taifa letu wewe unaleta utani ndani yake, wanamtandao ndio hao imeshindikana kuwapeleka mahakamani pamoja na kuwa na ushaidi unaonyesha kuwa RA alisaini kwa niaba ya kagoda ltd lakini wanasema hakuna ushaidi wewe unaingiza utani.

  Watu walishaona kuwa udhibiti wa kundi la wanamtandao ni kazi kwani wao ndio wanaendesha serikali na sio serikali iliyochaguliwa na wananchi, tusaidieni basi wanaCCM kuakikisha wausika kama sio nyinyi mlitumia hizo pesa kwenye kampeni wanashitakiwa kwa haki na sio kuonewa wala kupendelewa
   
Loading...