Hofu ya Mbowe na CHADEMA juu ya Zitto

Hofu ya Mbowe na CHADEMA juu ya Zitto

Ally Kanah

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Posts
1,479
Reaction score
388
Asalaam aleikhum wanajukwaa

Kwa takribani kipndi kama cha mwezi mzima uliopita kumeibuka msuguano mkubwa sana hasa kwenye mitandao ya kijamii kati ya wafuasi wa CHADEMA dhidi ya wafuasi wa chama cha ACT.

Msuguano huo hasa unahusisha wale wafuasi wa CHADEMA kurusha tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu Zitto kwa kumuita -------, Anatumiwa na CCM kuuwa upinzani, Anaandaliwa mikutano yake na CCM na shutuma nyinginezo nyingi nyingi tu sina haja ya kuzirudia hapa.

Lakini kwa upande wa huyo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA yeye alishapigia mstari kule alikokuwepo na ameanza safari yake mpya katika chama kipya na ambacho amakiasisi yeye mwenyewe wakati akiwa bado na kesi dhidi ya CHADEMA na hatukuwai kumsikia ama haijathibitishwa ya kwamba huko ACT alipohamia amekuwa akiwatuhumu ama kuwashambulia viongozi wa chama chake cha zamani lakini pia chama chake cha zamani.

Sasa nirudi katika hoja ya kwanini Mbowe, Slaa na baadhi ya wanachama wa chadema walio watiifu kwa Mbowe na wale wafuata mkumbo wanahofu dhidi ya ZITTO?

Ni ukweli usiopingika Mbowe na Zitto ndio waliotumia muda mwingi kukijenga chama hicho na kuwaaminisha Watanzania kwamba muarubaini wa matatizo yao umepatikana na katika pilika za kukujenga chama hicho ndugu Zitto aliwavutia vijana wengi sana kuipenda siasa hasa ikizingatiwa kipindi kile hakukuwa na vijana waliokuwa wanavutiwa na siasa.

Kwa mantiki hiyo ndani ya CHADEMA kuna viongozi wengi ambao wamekuwa wakinungunika muda mrefu sana kutokana na aina ya uongozi wa mabavu ambao mwenyekiti na katibu wake pamoja na wale vipenzi vyao wanaoutumia.

Na wamekuwa hawana sehemu ya kusema kwa kuwa wako ndani ya chama lakini wametengwa na ni wanamageuzi wa ukweli kabisa nikiwa na maana hawawezi kuhamia chama tawala kwa hiyo wamekuwa kwa muda mrefu wakivumilia vurugu zote na mabavu ya Mwenyekiti na genge lake.

Sasa hofu inakuja zaidi kwa Mwenyekiti na genge lake kwa kuwa wale Makamanda sasa wanamahali pakuelekea na hasa baada ya kuona mwanzo wa ziara za ACT na hali yakuwa Makamanda hao wanaushawishi mkubwa sana katika jamii inayowazunguka.

Wasalaam
 
Wasalamaleku sisi ni waarabu sisi waafrica vipi wewe au hauna lugha ya Kabila lako unatuletea mambo ya jihad hapa kwani umeambiwa nani tunataka kujilipua mabomu ili twende peponi ??
 
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani ana mambo muhimu ya kufanya hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu - yaani uwe na wasiwasi na chama ambacho hakina hata kiongozi mmoja wa mtaa nchi nzima!! maajabu.

Mwacheni kijana ahangaike akichoka atakaa kama walivyokwisha kaa wengine!! Siasa za nchi hii si za kuingilia kichwa kichwa - angepata ushauri toka kwa kina Lamwai and the like!!
 
Wasalamaleku sisi ni waarabu sisi waafrica vipi wewe au hauna lugha ya Kabila lako unatuletea mambo ya jihad hapa kwani umeambiwa nani tunataka kujilipua mabomu ili twende peponi ??

Ndugu acha ubaguzi sisi wote ni wamungu na kwa mungu tutarudi
 
Chadema Tunawaza Kupambana Na Ccm, Hatuwazi Kupambana Na Tuvikundi Twa Maigizo, Tunatocheza Na Uhalisia Wa Maisha Ya Watu.
 
Poleni CDM hiyo ni NGO na siyo chama, iweje leo muasisi wa chama anakuwa na pensheni ndani ya mapato ya chama???
 
Makao Makuu ya Chadema kila siku vikao namna ya kumdhibiti Zitto.
 
Asalaam aleikhum wanajukwaa

Kwa takribani kipndi kama cha mwezi mzima uliopita kumeibuka msuguano mkubwa sana hasa kwenye mitandao ya kijamii kati ya wafuasi wa CHADEMA dhidi ya wafuasi wa chama cha ACT.

Msuguano huo hasa unahusisha wale wafuasi wa CHADEMA kurusha tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu Zitto kwa kumuita -------, Anatumiwa na CCM kuuwa upinzani, Anaandaliwa mikutano yake na CCM na shutuma nyinginezo nyingi nyingi tu sina haja ya kuzirudia hapa.

Lakini kwa upande wa huyo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA yeye alishapigia mstari kule alikokuwepo na ameanza safari yake mpya katika chama kipya na ambacho amakiasisi yeye mwenyewe wakati akiwa bado na kesi dhidi ya CHADEMA na hatukuwai kumsikia ama haijathibitishwa ya kwamba huko ACT alipohamia amekuwa akiwatuhumu ama kuwashambulia viongozi wa chama chake cha zamani lakini pia chama chake cha zamani.

Sasa nirudi katika hoja ya kwanini Mbowe, Slaa na baadhi ya wanachama wa chadema walio watiifu kwa Mbowe na wale wafuata mkumbo wanahofu dhidi ya ZITTO?

Ni ukweli usiopingika Mbowe na Zitto ndio waliotumia muda mwingi kukijenga chama hicho na kuwaaminisha Watanzania kwamba muarubaini wa matatizo yao umepatikana na katika pilika za kukujenga chama hicho ndugu Zitto aliwavutia vijana wengi sana kuipenda siasa hasa ikizingatiwa kipindi kile hakukuwa na vijana waliokuwa wanavutiwa na siasa.

Kwa mantiki hiyo ndani ya CHADEMA kuna viongozi wengi ambao wamekuwa wakinungunika muda mrefu sana kutokana na aina ya uongozi wa mabavu ambao mwenyekiti na katibu wake pamoja na wale vipenzi vyao wanaoutumia.

Na wamekuwa hawana sehemu ya kusema kwa kuwa wako ndani ya chama lakini wametengwa na ni wanamageuzi wa ukweli kabisa nikiwa na maana hawawezi kuhamia chama tawala kwa hiyo wamekuwa kwa muda mrefu wakivumilia vurugu zote na mabavu ya Mwenyekiti na genge lake.

Sasa hofu inakuja zaidi kwa Mwenyekiti na genge lake kwa kuwa wale Makamanda sasa wanamahali pakuelekea na hasa baada ya kuona mwanzo wa ziara za ACT na hali yakuwa Makamanda hao wanaushawishi mkubwa sana katika jamii inayowazunguka.

Wasalaam

Kwa jinsi ninavyo mjua Zitto labda awe ame change sidhani kama ana muda wa kuwaza haya unayo yaandika . Zitto anakazana kukitangaza chama chake kipya mpeni nafasi . Zitto ni Kiongoz mkuu wa Chama na naamini atahitaji kusema a viongozi wenzake wa vyama . Acheni ujinga mtandaoni wekeza nguvu kuijenga ACT . Kwa hali hii yaonekana wazi nyie ndiyo mna wasi wasi na watu binafsi ndani ya Chadema .Maana kila siku Chadema na Mbowe na Slaa lakini sijamsikia kiongozi yeyote wa Chadema akisea juu ya Zitto wala ACT .
 
YUDA Eskarioti hakuna kitu hapo na CDM inapambana na CCM na hakuna hata siku moja itapambana na ACT, nyie endeleeni kumlamba miguu YUDA.

Na endeleeni kujipa moyo ila October itafika, na hapa ndo kitaeleweka.

Ndugu ingekuwa vyema japo kidogo ukatafakari haya yaliyomo kwenye hili bandiko...

Na kwa kuongezea tu humu humu jukwaaani walitokea watu wengi sana kuishauri chadema hasa kwa wakati huu wasimfukuze ila wakapuuza na niko na wasiwasi mkubwa sana kama Lissu hajui alilokuwa analifanya...

Na swali kwako wewe ndugu Lissu kuwa kiherehere katika sakata la Zitto je alikuwa anatumiwa na nani?? Ni kweli Mbowe alikuwa anamtumia Lissu?? Ama ni watawala walikuwa wanamtumia Lissu??
 
Mbowe amekasirika sana kazi aliyowapa Bavicha ya kumchafua Zitto mitandaoni imefeli, matokeo yake Watanzania wanazidi kumpenda
 
Ninavyojua mimi hakuna kiongozi yeyote wa CHADEMA anayepambana na Zitto wala ACT. Mtakumbuka katibu mkuu alisema suala la Zitto limekwisha na mjadala umefungwa.Sijamsikia Mbowe, Slaa, Lissu wala kiongozi yeyote wa ngazi za juu WA CHADEMA akimzungumza Zitto. Ni kweli pia Zitto hazungumzii CHADEMA wala viongozi wake. Ila Ni kweli msuguano haina ya wafuasi WA vyama hivyo upon lakini hauwahusu viongozi Bali wanachama wa kawaida. Kwa hiyo Mbowe wala Slaa hawana hifu yoyote na Zitto na ndiyo maana wanaendelea na kazi zao za kawaida. Hivi Slaa yuko ziarani marekani na Mbowe yuko jimboni kwa kazi za kibunge.
 
Ndugu ingekuwa vyema japo kidogo ukatafakari haya yaliyomo kwenye hili bandiko...

Na kwa kuongezea tu humu humu jukwaaani walitokea watu wengi sana kuishauri chadema hasa kwa wakati huu wasimfukuze ila wakapuuza na niko na wasiwasi mkubwa sana kama Lissu hajui alilokuwa analifanya...

Na swali kwako wewe ndugu Lissu kuwa kiherehere katika sakata la Zitto je alikuwa anatumiwa na nani?? Ni kweli Mbowe alikuwa anamtumia Lissu?? Ama ni watawala walikuwa wanamtumia Lissu??

Nina swali. Kama Zitto alikuwa na ufuasi mkubwa kama mnavyosema, ilikuwaje 2010 majimbo mengi Kigoma yalichukuliwa na NCCR-Mageuzi?? Huo ufuasi uko wapi ni kwa maneno au matendo?
 
Mbowe halali sikuhizi yani pale ufipani hata mbege hazinyweki,babu slaa hali inazidi kuwa mbaya kaenda kutibiwa usa wenyewe wanadai eti kaenda kikazi nani hajui kama huyu babu afya inazidi kuzorota kila siku
 
Nina swali. Kama Zitto alikuwa na ufuasi mkubwa kama mnavyosema, ilikuwaje 2010 majimbo mengi Kigoma yalichukuliwa na NCCR-Mageuzi?? Huo ufuasi uko wapi ni kwa maneno au matendo?

Kama huamini katika hilo basi wafuasi watiifu wa Mbowe wasingekuwa wanahangaika humu kumchafua Zitto bali wangekuwa deep kumwaga sera za chama chao
 
Chadema Tunawaza Kupambana Na Ccm, Hatuwazi Kupambana Na Tuvikundi Twa Maigizo, Tunatocheza Na Uhalisia Wa Maisha Ya Watu.

Mkuu unatumia imagination ama uhalisia?? Au humu jukwaani na katika mitandao mbalimbali ya kijamii huwa haupiti??
 
Nina swali. Kama Zitto alikuwa na ufuasi mkubwa kama mnavyosema, ilikuwaje 2010 majimbo mengi Kigoma yalichukuliwa na NCCR-Mageuzi?? Huo ufuasi uko wapi ni kwa maneno au matendo?

zitto alisababisha.
 
ZZK ni mfa maji huku kwetu tunasema hivyo, kwani prukushani zake zinafika hata 1% ya mrema? au 1% za wengine waliohama CDM?? hakuna
 
Kama huamini katika hilo basi wafuasi watiifu wa Mbowe wasingekuwa wanahangaika humu kumchafua Zitto bali wangekuwa deep kumwaga sera za chama chao
Kama Nyinyi wafuasi wa Zitto mnavyomchafua Mbowe! Kama wafuasi WA Zitto wanaendelea kuichafua CHADEMA na viongozi wake humu Hakika msuguano hautakwisha. Sera ya jino itaendelea mpaka October na watakaopoteza pambano ni act kwa kuwa wao Ni chama kipya badala wajenge chama wanahangaika na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom