Hofu ya COVID0-19: Baadhi ya Hospitali kukataa wagonjwa wapya, maiti kukataliwa mochwari, sisi wanyonge tumwangukie nani?

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Habari WanaJF,

Tokea Ugonjwa wa COVID-19 ulete taharuki nchini, hali ya huduma ya afya nayo imezidi kudorora kwa namna moja au nyingine. Baadhi ya Hospitali za Serikali na Binafsi zimegeuka kuwa mwiba kwa wagonjwa kwa kutowapatia huduma hasa unapoonesha dalili yoyote ya COVID-19, imefika hali mpaka mgonjwa anafukuzwa hospitali hata kabla hajaelezea shida yake. Mathalani na miili ya wapendwa wetu imekuwa ikikataliwa kuhifadhiwa kwa visingizio mbalimbali ambavyo havikuwepo kabla ya janga la COVID19

Binafsi nina visa kadhaa vya kuunga hoja yangu ninayoiwasilisha.

Kuna jamaa yangu kwa jina la Y, mwanaye alipata shida kidogo na akaamua kumpeleka Hospitali ya Tumbi, Kibaha. Alivyofika pale akaambiwa kwamba mhusika anayeshughulika na watoto hayupo kabisa. Na kwa muda aliofika pale, kila aliyekuwa anakuja pale hospitali alikuwa akirudishwa nyumbani bila hata kuuliza tatizo lililomleta pale. Inahuzunisha sana.

Jamaa yangu Y aliamua kwenda Hospitali ya Bochi, huku nako alikatishwa tamaa baada ya kuambiwa kwamba hawapokei wagonjwa wapya na akashauriwa kwamba akatafute huduma kwenye Hospitali nyingine.

Hizi Hospitali tajwa hapo Juu(Tumbi na Bochi) pia zilishiriki kumhujumu jamaa yangu mwingine ambaye sasa ni marehemu. Kwa sasa tunasubiri vipimo vya mamlaka kututhibitishia sababu za kifo chake japokuwa wote tunajua kilichomuua ni kale kaugonjwa kanakopaswa kusemewa na Waziri Mkuu na Waziri wa Afya.

Hospitali kubwa na Muhimu kama Muhimbili, Aga Khan, SALI hazipokei wagonjwa wapya sana sana utarudishwa. Kwa wale wenye jamaa wanaohudumu kwenye hospitali kubwa kubwa wanaweza kuthibitisha kwa kuwauliza. Sitaki niongee mengi nikawa mbuzi wa kafara.

Naomba Mamlaka husika kulitafutia ufumbuzi haraka sana suala hili, hofu ni kubwa sana mtaani na mpaka kwenye Hospitali zetu ambazo sasa ni kimbilio muhimu.

Mamlaka itoe vifaa tiba kwa wahudumu wetu ili wapate ujasiri na moyo wa kutuhudumia. Nakumbuka Rais wa Shirikisho la Madaktari Tanzania (MAT) alilalamikia hili suala mchana kweupe. Wahudumu pia wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu hawakuwa nyuma kuilalamikia Serikali kwa namna isivyowajali watoa huduma hao juu ya vifaa vya kujikinga na Corona.

Waziri Ummy Mwalimu huko nyuma alisisitiza kwamba watoa huduma wasiwakimbie na kuwafukuza wagonjwa kwani siyo kila anayeumwa homa ana COVID-19 lakini nipende kumhakikishia kwamba endapo msipowajali hawa watoa huduma wa afya, sisi wananchi mnaotuita wanyonge tutaendelea kukimbiwa na kufukuzwa.

HOFU IMEKUWA KUBWA NA HATARI SANA KULIKO UGONJWA WENYEWE. Tumebaki kununua dawa famasi na kutumia dawa bila ushauri wa daktari. Dispensary nyingine zinazotuhudumia hazikidhi vigezo vya kutoa huduma kwa baadhi ya magonjwa.

Nawashauri kufuata tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya na wale wenye mamlaka ili kuweza kujiweka salama wewe pamoja na jamaa zako dhidi ya kaugonjwa haka ka COVID-19

Nawatakia wakati mwema.


Mnaweza kusoma hizi mada pia

- Wauguzi na Madaktari msiposema ukweli COVID-19 itawapukutisha
- Ummy Mwalimu: Watoa huduma za afya wasikimbie wagonjwa, sio kila homa kali ni Corona
- Wafanyakazi Hospitali ya Mbagala Rangi tatu walalamika kutopewa vifaa vya kujikinga dhidi ya washukia wa virusi vya Corona
 
Inakerehesha sana, juzi kuna mwana kapukutika, maiti ilivyopelekwa Tumbi wakagoma kuipokea na kusema hawataki maiti za vile labda wapeleke Mloganzila. Sasa unakaa unajiuliza hizi mochwari zina kazi gani! Wakati mwingine unawaelewa halafu lawama unaitupia Serikali.
 
Back
Top Bottom