Hofu ya CCM ya Magufuli 2020 ni Hatari kwa nchi

Shida ya wewe ndugu yangu Zitto ni kuweka mada mezani kisha unatokomea kusikojulikana..

Nadhani ingekuwa vyema unapoweka au kuanzisha mjadala then kaa tuudadavue kwa pamoja siyo kuturushia tu halafu unapotea.. ukifanya hivyo unakuwa huna tofauti na yule bongo muvi aliyewarushia fedha waandishi kisha kabaki pembeni akiangalia wanavyovunjiana vifaa vyao vya thamani..

Anyway narudi kwa hoja yako soon... Acha vijana tuufaidi uwezo wako wa kudadavua mambo usibane..!!

BACK TANGANYIKA
Wewe comment tu , atakujibu kwa ID tofauti.
 
CCM haiwezi kuondolewa au kushindwa kuendelea kuongoza bila kuvurugana Kwanza wao wenyewe
 
Dec 2016, sitaisahau. Ndio kikao cha kwanza kiliketi na kupendekeza mikakati. Model ya uturuki ilikuwa ni moja ya mkakati. Wasifikiri wao tu ndio wanaweza kudukua. Mdukuaji pia hudukuliwa wakati anadukua.
 
....mkitishiwa mtaogopa tu
....wapinzani wa TZ ni waoga pengine kuliko wapinzani wa nchi yoyote Africa
...kukaa sana CCM madarakani sio kwamba ni bora sana kuliko vyama vingine Africa vilivyoanguka NO...ni aina ya viongozi wa upinzani tulionao Tanzania -...mnataka kuonewa huruma na ccm .pathetic
Acha mawazo kama sabato masalia,nchi hii yetu sote.ccm waende nchi ibaki
 
Ni kwel ameanza kula na kunogewa kidg tu utawala alafu watu ndan ya chama tawala wanataka kumwaga mchele kwenye kuku wengi lazima wachachamae
 
Harakati za Musiba na wenzake zitaharakisha mipasuko ndani ya CCM. Options zilizopo kwa wana CCM wasioridhika na mambo yanavyokwenda ni kuhama na kuunda vuguvugu la upinzani lenye nguvu kama walivyofanya akina odinga wa kenya dhidi ya moi. Pili kosa kubwa la watawala wetu ni kutotambua umuhimu wa mageuzi ya katiba ambayo yangedhibiti hali ya imperial presidency iliyopo sasa na uminywaji wa separation of powers. Ni vizuri siku zote wakakumbuka ule msemo maarufu - what goes around comes around.
HOFU ya CCM ya Magufuli ni Hatari kwa Nchi yetu

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala mkali nchini kuhusu Tamko lililotolewa na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba. Wana CCM hao wameandika malalamiko yao kwa Baraza la Wazee wa Chama chao ili hatua zichukuliwe. Katika hali ya kawaida hili lilipaswa kuwa jambo la CCM na kushughulikiwa na chama hicho wenyewe. Hata hivyo jambo hilo limechukua mkondo wa kitaifa na haswa usalama wa watu na usalama wa Taifa.

Tamko la Kanali Kinana na Luteni Makamba limeujulisha Umma mipango dhalimu ya kubumba kesi za uhaini kwa Wanasiasa waandamizi nchini kutoka Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Pia baadhi ya wana harakati ambao Bwana Musiba amekuwa akiwataja kuwa ni watu hatari kwa nchi ni miongoni mwa wahanga wa mipango hiyo. Kina Kinana wametibua mpango huo ndio maana wafuasi au wanaojiita wanaomwunga mkono Rais Magufuli wametaharuki na wanajaribu sana mipango yao iendelee. Shabaha ya kesi ya uhaini ni kuhakikisha ama mwaka 2020 hapatakuwa na uchaguzi au uchaguzi ufanyike wakati wanasiasa wote waandamizi nchini wakiwa magerezani au wasiwepo kabisa.

Baadhi ya wanasiasa wameanza kujiokoa kwa kujiegemeza upande wa wenye mamlaka. Hata wale ambao kwa muda sasa wamekuwa ni tumaini la Wananchi kwa kuwa wakosoaji wakuu wa Serikali wamerudi nyuma na kutoa kauli za kujikosha . Kwa mfano mtu ambaye amekuwa akikosoa vikali Serikali kule mwanzo nia ilikuwa ni kumnyima uhalali Rais Magufuli ? Mbona wakati wa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alikuwa anashambuliwa sana na Wazee kama vile Mzee Butiku, Warioba nk lakini hatukusikia haya? Kitu gani ‘special’ wakati huu? Nadhani huu Ni wakati kwa wapenda demokrasia wote kutoogopa na kuwa pamoja.

Sisi wengine tunajua kitambo kuwa CCM imeshafika mwisho wake. Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli inataka kuondoka na nchi yetu. Tusikubali. Tumesoma kuwa kabla ya Wazee hao wastaafu wa CCM kuandika, waliomba ushauri na Mzee Pius Msekwa akawaambia ‘jibuni Mapigo’. Ina maana Msekwa naye anataka kuua Chama chao? CCM ianguke yenyewe na ituachie nchi yetu.

Hofu ya Watawala kuhusu 2020 isihatarishe nchi yetu. Mipango ya Kesi ya Uhaini iachwe mara moja. Ukosoaji ndani au nje ya vyama vya Siasa kamwe haiwezi kuwa uhaini. Acha demokrasia ishamiri

Zitto Kabwe

18/7/2019
 
Umejiridhisha kuwa hiyo mikakati siyo halisi imebumbwa na upande wa rais Magufuli? Huu uchambuzi wako umeuweka Kama vile unajua Sana au unataarifa halisi za mwenendo wa Jambo hili, siamini Kama unajua Sana!

Ingetosha tu kusema umetoa maoni binafsi ( personal opinions) ila sio ukweli halisi ( objective truth). Halafu mnaowashangilia Hawa wazee na kudhani kuwa wakimuondoa Magufuli mtanufaika kimaisha Hilo sahauni, kundi la Hawa wazee ni wachumia matumbo wasio na kujali umma.
 
Back
Top Bottom