Hofu ya CCM ya Magufuli 2020 ni Hatari kwa nchi

Isemwe ukweli tu, makundi hasimu na wenye mitazamo tofauti ndani ya CCM yamekuwepo toka enzi za Mwalimu.
Tofauti iliyopo saa ni kushindwa kwa Mwenyekiti kuyabalance makundi hayo kwa kuyapa vyeo, nyadhifa na hata kuyakusanya kwa dinner pamoja.

Kutumia mabavu si suluhisho maana hiyo italeta mtafaruku mbaya aidi.
Hivi kuna ubyaa gani Mwenyekiti akiwaita wale anaotofautiana nao ndani ya CCM, wakakaa pamoja, pasuliana ukweli behind closed doors na kutoka na tamko la Umoja?

Yanayoendelea yataliangamiza Taifa na Umoja wake kama tunavyolifahamu.
Tatizo la jiwe anataka kuunda ccm ya kwake itakayoabudu na kutukuza kila aina ya uchafu, sasa hawa ma bright hawakubaliani na huo ujuha.
 
Yaani Rais ambaye ndiye Mwenyekiti atoswe?? aaaaa tuheshimiane!!

CCM mnalo...mliambiwa mtofautishe kofia tangu 1985 mkagoma..haya mziki huo.

Siyo rahisi kabisa kwa Mwenyekiti na Amiri jeshi Mkuu kutoswa...yeye ndiye ameshika mpini...Ila wapo watu muhimu wanaweza wakatoswa au hata kuswekwa ndani...Mimi binafsi sitashangaa hili likitokea....
 
Lakini busara itumike, huyu bwana magufuri wote tayari tunajua yuko tayari kuua watu ilimradi analotaka yeye liwe, sasa hii hofu yake inavyoongezeka ndio raia wengi zaidi uhai wao unakuwa matatani.

Nashauri, kama inawezekana ahakikishiwe kuwa rais mpaka 2025 akili yake itulie, nashauri tu.
Hapana apigwe yeye mapema na sniper au mtu ajitoe kafara
 
HOFU ya CCM ya Magufuli ni Hatari kwa Nchi yetu

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala mkali nchini kuhusu Tamko lililotolewa na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba. Wana CCM hao wameandika malalamiko yao kwa Baraza la Wazee wa Chama chao ili hatua zichukuliwe. Katika hali ya kawaida hili lilipaswa kuwa jambo la CCM na kushughulikiwa na chama hicho wenyewe. Hata hivyo jambo hilo limechukua mkondo wa kitaifa na haswa usalama wa watu na usalama wa Taifa.

Tamko la Kanali Kinana na Luteni Makamba limeujulisha Umma mipango dhalimu ya kubumba kesi za uhaini kwa Wanasiasa waandamizi nchini kutoka Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Pia baadhi ya wana harakati ambao Bwana Musiba amekuwa akiwataja kuwa ni watu hatari kwa nchi ni miongoni mwa wahanga wa mipango hiyo. Kina Kinana wametibua mpango huo ndio maana wafuasi au wanaojiita wanaomwunga mkono Rais Magufuli wametaharuki na wanajaribu sana mipango yao iendelee. Shabaha ya kesi ya uhaini ni kuhakikisha ama mwaka 2020 hapatakuwa na uchaguzi au uchaguzi ufanyike wakati wanasiasa wote waandamizi nchini wakiwa magerezani au wasiwepo kabisa.

Baadhi ya wanasiasa wameanza kujiokoa kwa kujiegemeza upande wa wenye mamlaka. Hata wale ambao kwa muda sasa wamekuwa ni tumaini la Wananchi kwa kuwa wakosoaji wakuu wa Serikali wamerudi nyuma na kutoa kauli za kujikosha . Kwa mfano mtu ambaye amekuwa akikosoa vikali Serikali kule mwanzo nia ilikuwa ni kumnyima uhalali Rais Magufuli ? Mbona wakati wa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alikuwa anashambuliwa sana na Wazee kama vile Mzee Butiku, Warioba nk lakini hatukusikia haya? Kitu gani ‘special’ wakati huu? Nadhani huu Ni wakati kwa wapenda demokrasia wote kutoogopa na kuwa pamoja.

Sisi wengine tunajua kitambo kuwa CCM imeshafika mwisho wake. Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli inataka kuondoka na nchi yetu. Tusikubali. Tumesoma kuwa kabla ya Wazee hao wastaafu wa CCM kuandika, waliomba ushauri na Mzee Pius Msekwa akawaambia ‘jibuni Mapigo’. Ina maana Msekwa naye anataka kuua Chama chao? CCM ianguke yenyewe na ituachie nchi yetu.

Hofu ya Watawala kuhusu 2020 isihatarishe nchi yetu. Mipango ya Kesi ya Uhaini iachwe mara moja. Ukosoaji ndani au nje ya vyama vya Siasa kamwe haiwezi kuwa uhaini. Acha demokrasia ishamiri

Zitto Kabwe

18/7/2019
Unakera
Kazi kurukia hata husiyoyajua
Ya chama chako yamekushinda, ya ccm utayaweza?
Rejea ccm enzi za marehemu Kolimba
Usilolijua sawa na usiku wa giza
 
Ni kweli umoja wa kisiasa ni muhimmu...Lakini tangu enzi za Nyerere mpaka sasa, wakati mwingine, ni muhimu kuwatosa baadhi kutoka kwenye kundi...Mfano Abdul (?) Jumbe wakati wa Nyerere (1984), Horace Kolimba wakati wa Mwinyi (miaka ya 1990), Malecela wakati wa Mwinyi (miaka ya 1990), Lowassa wakati wa Kikwete (mwaka 2008???), wakati nikiwa mdogo kuna wabunge saba waliwahi kufukuzwa (wakiwemo Kibuga, Anangisye na wengine)...Orodha ni ndefu kabisa...Kwa namna mambo yanavyoendelea sitashangaa NEC au mkutano mkuu wa CCM ukaitishwa kufanya maamuzi muhimu...aliyeshika mpini ndiye ambaye siku zote hushinda kwenye historia ya nchi hii na siyo vinginevyo....
Mkuu you are dead wrong!
Na analogies unazotoa hazina basis kwa tatizo tulilonalo sasa ndani ya CCM.
Nikuulize, hivi mdomo wa jipu lenyewe Musiba, ni kwa kanuni ipi ya chama?
Tofauti ndani ya chama zinatatuliwa na Musiba?
Kama tofauti zipo si wahusika waitwe wahojiwe.
Na wakikosa wanachukuliwa hatua stahiki.
Hicho ndo chama tunachokifahamu.

I will not mince my words, kumtumia Musiba ni uoga wa kutowaface mahasimu wako katika vikao.
 
Mmmmmh Dah....Kwanza nayaheshimu mawazo ...una uhuru wa kusema unachoelewa wewe na pia kufanya analysis kwa kuzinatia unachofahamu...Lakini hivi kwanini watu mnakimbilia kumsema Musiba...Kwa maoni yangu ishu siyo Musiba ila ishu ni kama anayosema Musiba ni ya kweli au siyo kweli..Hao wazee waliotajwa, kwa maoni yangu, wamekosea mno njia waliyotumia....Kumsema Rais kwa namna ile walivyofanya it is wrong....Kwa maoni yangu wanalazimika kuomba radhi...vinginevyo nakuhakikishia watazama na kusahaulika kabisa...Nimeisoma barua ile ambayo imo mitandaoni na bila shaka ndiyo hiyo...Kwa maoni yangu barua ile ina maneno yenye mwelekeo wa usaliti au hata uhaini...At the end of the day they will have to face the music...Tatizo lililomo ndani ya CCM ni mazoea ya unafiki, upigaji na umimi...Awamu hii, kwa maoni yangu, inajaribu kuondoa hilo...hapo ndipo lilipo tatizo...waliozoea ulaji hawataki kuguswa...Nakuthibitishia jambo moja nalo ni kwamba yeyote yule ambaye atajaribu 'kumgusa' JPM atapambana na wimbi kubwa la 'nguvu ya umma'...JPM ni very popular hivi sasa, ni popular mno kwa watu wa kawaida...akiguswa tu itakula kwao....
 
Huyu tapeli kashaandaa tamko kwa manyumbu wake..

Naona wameshaanza kuimba na kusherekea..haya vigelegele viendelee
 
Mkuu lazima utambue, chama kwanza mengine baadaye.
Na maana ya chama kwanza ni ule Umoja uliomo ndani ya chama.
Going solo......kama kutumia self styled propaganda instruments kama Musiba, hilo linaweza kubackfire.

Tuambie kwanza chama kinamtambua Musiba au la?
Kama kinamtambua basi Polepole na Bashiru wa kazi gani?
Sina wasiwwasi JPM anapendwa na lazima aendelee mpaka 2025, lakini kukinyanyapaa chama kutakuwepo gharama zake.
 
Muvi hii inaweza kuwa ya mipango ya baada ya 2020, ili asiwepo wa kukemea watakapokuja na wazo la kutaka kumsimika Museveni au Kagame wetu.
 
Isemwe ukweli tu, makundi hasimu na wenye mitazamo tofauti ndani ya CCM yamekuwepo toka enzi za Mwalimu.
Tofauti iliyopo saa ni kushindwa kwa Mwenyekiti kuyabalance makundi hayo kwa kuyapa vyeo, nyadhifa na hata kuyakusanya kwa dinner pamoja.

Kutumia mabavu si suluhisho maana hiyo italeta mtafaruku mbaya aidi.
Hivi kuna ubyaa gani Mwenyekiti akiwaita wale anaotofautiana nao ndani ya CCM, wakakaa pamoja, pasuliana ukweli behind closed doors na kutoka na tamko la Umoja?

Yanayoendelea yataliangamiza Taifa na Umoja wake kama tunavyolifahamu.
Ushauri mzuri wa kukaa pamoja, lakini utafanyiwa kazi? Nakumbuka comment ya mkuu kuwa ingekuwa yeye in 2015 angewafukuza wanachama wote walioimba "tuna imani na Lowasa". Kama ataendelea na kuamini mabavu bila busara, tutarajie makubwa zaidi. Hofu yangu ni kuterereka kwa umoja wa taifa hasa ikitiliwa maanani kuwa siasa za kutugawa, kikanda, kikabila na hata kidini zimeanza kuota mizizi.
 
Mungu wetu mwema atatuvusha tu na hili balaa lililokuja kutuvurugia nchi! Inaudhi zaidi eti kuna wengine wanajifanya hawaoni, eti wanamuunga mkono, maana "anaendeleza nchi na kupambana na ufisadi"; hivi ni kweli hawajui kuwa yeye ni fisadi tangu awamu iliyopita na kwa sasa ndo fisadi papa?
 
HOFU ya CCM ya Magufuli ni Hatari kwa Nchi yetu

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala mkali nchini kuhusu Tamko lililotolewa na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba. Wana CCM hao wameandika malalamiko yao kwa Baraza la Wazee wa Chama chao ili hatua zichukuliwe. Katika hali ya kawaida hili lilipaswa kuwa jambo la CCM na kushughulikiwa na chama hicho wenyewe. Hata hivyo jambo hilo limechukua mkondo wa kitaifa na haswa usalama wa watu na usalama wa Taifa.

Tamko la Kanali Kinana na Luteni Makamba limeujulisha Umma mipango dhalimu ya kubumba kesi za uhaini kwa Wanasiasa waandamizi nchini kutoka Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Pia baadhi ya wana harakati ambao Bwana Musiba amekuwa akiwataja kuwa ni watu hatari kwa nchi ni miongoni mwa wahanga wa mipango hiyo. Kina Kinana wametibua mpango huo ndio maana wafuasi au wanaojiita wanaomwunga mkono Rais Magufuli wametaharuki na wanajaribu sana mipango yao iendelee. Shabaha ya kesi ya uhaini ni kuhakikisha ama mwaka 2020 hapatakuwa na uchaguzi au uchaguzi ufanyike wakati wanasiasa wote waandamizi nchini wakiwa magerezani au wasiwepo kabisa.

Baadhi ya wanasiasa wameanza kujiokoa kwa kujiegemeza upande wa wenye mamlaka. Hata wale ambao kwa muda sasa wamekuwa ni tumaini la Wananchi kwa kuwa wakosoaji wakuu wa Serikali wamerudi nyuma na kutoa kauli za kujikosha . Kwa mfano mtu ambaye amekuwa akikosoa vikali Serikali kule mwanzo nia ilikuwa ni kumnyima uhalali Rais Magufuli ? Mbona wakati wa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alikuwa anashambuliwa sana na Wazee kama vile Mzee Butiku, Warioba nk lakini hatukusikia haya? Kitu gani ‘special’ wakati huu? Nadhani huu Ni wakati kwa wapenda demokrasia wote kutoogopa na kuwa pamoja.

Sisi wengine tunajua kitambo kuwa CCM imeshafika mwisho wake. Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli inataka kuondoka na nchi yetu. Tusikubali. Tumesoma kuwa kabla ya Wazee hao wastaafu wa CCM kuandika, waliomba ushauri na Mzee Pius Msekwa akawaambia ‘jibuni Mapigo’. Ina maana Msekwa naye anataka kuua Chama chao? CCM ianguke yenyewe na ituachie nchi yetu.

Hofu ya Watawala kuhusu 2020 isihatarishe nchi yetu. Mipango ya Kesi ya Uhaini iachwe mara moja. Ukosoaji ndani au nje ya vyama vya Siasa kamwe haiwezi kuwa uhaini. Acha demokrasia ishamiri

Zitto Kabwe

18/7/2019
Yona Atoswe baharini ili merikebu isizame
 
Mkuu lazima utambue, chama kwanza mengine baadaye.
Na maana ya chama kwanza ni ule Umoja uliomo ndani ya chama.
Going solo......kama kutumia self styled propaganda instruments kama Musiba, hilo linaweza kubackfire.

Tuambie kwanza chama kinamtambua Musiba au la?
Kama kinamtambua basi Polepole na Bashiru wa kazi gani?
Sina wasiwwasi JPM anapendwa na lazima aendelee mpaka 2025, lakini kukinyanyapaa chama kutakuwepo gharama zake.

Dah...Musiba ni nani jamani? Kwanini watu mmnamshupalia Musiba? Kama mtu umeumizwa na Musiba si uende mahakamani??? Musiba wala hajasemma anaongea kwa niaba ya CCM wala serikali....yeye ni mwanaharakati tu na amejitambulisha kuwa anamuunga mkono Rais...sasa hapa ndipo lilipo tatizo...tumezoea kuwaona wanaojiita wanaharakati wakimponda Rais, CCM na serikali...na wanaharakati hawa mara nyingi huwa wanafadhiliwa na nchi za ulaya na Marekani...lakini huyu amesema kuwa yeye yuko na Rais na anaunga mkono Rais...sijui Musiba anafadhiliwa na nani lakini alichokifanya Musiba ni kitu ambacho hakijazoeleka...Tumezoea kuona magazeti yanayompinga Rais, serikali na CCM...lakini huyu Musiba na gazeti la Tanzanite wanamuunga mkono Rais...sasa baadhi hawapendi hii....Lakini after a seccond thought upo wakati Lowassa alisemwa sana kuwa ni fisadi, je aliwahi kulalamika wapi?! Sasa hao wazee wammeshutumiwa halafu wanataka kutuaminisha kuwa Musiba ametumwa na Rais...Ukisomma ile barua yao ni wazi mlengwa ni Rais...

Unauliza kuwa CCM ijitokeze na kusma hadharani kuwa kama inamtambua au haimtambui Musiba....Mimi najiuliza kwanini CCM ilazimishwe kujipa kazi hiyo ya mwanaharakati?

Kwa maoni yangu hao wazee inabidi waombe radhi vinginevyo dhoruba dhidi yao inawahusu
 
Shida ya wewe ndugu yangu Zitto ni kuweka mada mezani kisha unatokomea kusikojulikana..

Nadhani ingekuwa vyema unapoweka au kuanzisha mjadala then kaa tuudadavue kwa pamoja siyo kuturushia tu halafu unapotea.. ukifanya hivyo unakuwa huna tofauti na yule bongo muvi aliyewarushia fedha waandishi kisha kabaki pembeni akiangalia wanavyovunjiana vifaa vyao vya thamani..

Anyway narudi kwa hoja yako soon... Acha vijana tuufaidi uwezo wako wa kudadavua mambo usibane..!!

BACK TANGANYIKA

Bora umesema, anakuja hapa jf kuweka mada, kisha anaenda kushinda tweeter!
 
Nchi imevurugwa vurugwa imekua tatizo kubwa sana jamaa angeongoza kirahisi sana kama angewaacha vyama vya upinzani viongee wanavyotaka na sio kama ilivyo sasa hata wastaafu wa ngazi za juu CCM wanasemwa vibaya kwa kutumika tuu huku kila mtu akijua kinachoendelea sasa kazi yake imekua ngumu na mambo ya kutekana na kubambikiana kesi yakikua kwa kasi ya ajabu sana.Nchi imepoteza muelekeo tunashuka chini badala ya kupanda juu...
 
Back
Top Bottom