Sir R
JF-Expert Member
- Oct 23, 2009
- 2,175
- 300
Katika michango mingi ya wana CCM, asilimia kubwa ni kumshambulia Dr Slaa kuliko hata Mbowe. Nimetafakari sana ni kwanini Dr Slaa anashambuliwa sana. Haiwezekani mtu mmoja ashambuliwe kiasi hiki bila sababu.
Naamini CCM wamegundua Dr Slaa ana nguvu ya kuiangusha CCM kama atagombea katika uchaguzi ujao. Njia walioona ni sahihi kumdhoofisha ni kumtukana na kumchafua kwa namna yoyote ile. Tunakumbuka vizuri walianza kupambana Dr Slaa wakati wa uchaguzi wa 2010 lakini hawakufanikiwa kama walivyotarajia.
Hofu kuu ya CCM ni uchaguzi unaokuja. Wanatamani Dr afe kabla ya uchaguzi. Wanamwombea kila aina ya balaa. Wanachoshindwa kuelewa ni kuwa Dr ni mtu mmoja ndani chama kikubwa.
Tufuatilie michango ya wana CCM hapa JF, kila post linamtaja Dr Slaa kwa kejeli. Nafikiri wamemkoza Dr Slaa kwa matukano yao kuliko kumdhoofisha.
Nawasilisha.