Hofu kuu waliyonayo CCM kuhusu Tundu Lissu

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,179
Wakati uchaguzi mkuu ukiwa unakaribia ccm wameanza kupata hofu na Tundu Lisu,

Hofu hiyo inakuja ikiwa chama chake cha Chadema bado Hakijaweka wazi ni nani kitaenda naye kama mgombea urais wao mwakani.

CCM imekuwa ikimzungumzia sana Lisu kama mgombea urais wa upinzani, wakati wapinzani wenyewe hawajakaa chini kuamua ni nani apeperushe bendera yao ifikapo mwakani.

Kama wataalam wa mambo ya utabiri walivyo nao wameanza kubashiri uchaguzi mkuu ujao kuwa utakuwa mgumu Mara mbili kwa ccm kuliko ilivyokuwa mwaka 2015

Huku wengine wakidai huenda CCM ikashuhudia mgombea wao akiongoza kwa muhula mmoja tu tofauti na ilivyozoeleka.

Hayo na mambo mengine yameanza kuitia homa CCM juu ya ni mgombea gani upinzani utamsimamisha mwakani.

Huku upinzani ukiwa uko kimya kuhusu ni nani atasimama mwakani kama mgombea wao wa urais, CCM wao wana hofu na Tundu lisu, MTU ambaye aliponea chupuchupu kuuawa na wabaya wake kisiasa.

Je, ni kwa nini CCM wanamzungumzia sana Lisu, wakati upinzani bado haujaamua ni nani apeperushe bendera yao mwakani katika kinyang'anyiro cha urais.

Hii hofu inatoka wapi

Wakati huo huo chama chake cha CHADEMA wao wako bize na mikutano yao ya ndani kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi wa kumi.

FB_IMG_15297357686600491.jpg
 
Hofu yao kubwa wanajua kabisa Magufuli hana uwezo kwa kujenga hoja za ushawishi kwa wananchi kama alivyo Lissu. Sasa hivi wanabaki kuchomekea eti Magufuli amefanya maendeleo makubwa na kuwajali wanyonge. Je ni mnyonge gani kafaidika na Magufuli kiasi kwamba akija rais mwingine huyo mnyonge atakosa hiyo faida?

Na ukiwafuatilia sasa hivi wanajaribu kuwadanganya wapinzani eti mtu yoyote asigombee kisa Magufuli anakubalika sana. Magufuli anakubalika kwa viashiria gani? Maana kama ni siasa hayuko tayari wenzake wafanye, kama ni vyombo vya habari hataki vinavyotoa habari za upande wa pili bali zile anazotaka yeye.

Hofu yao nyingine ni kwamba Lisu atakapoingia kwenye uchaguzi itakuwa ngumu kumuhujumu kwani tayari jumuiya ya kimataifa itafuatilia nyendo zake. Na hatari kubwa iliyo mbele yao ni iwapo Lissu atakubali kuibiwa kura na kukubali kukaa kimya.
 
Lazima waweweseke wanakila sababu kwenye kampen zao 2015 wali ahidi mambo mengi sana mazuri baada ya kuchaguliwa wakafanya kinyume Mala kupoteza watu kuumiza watu na kuwafunga kwenye viroba kuminya vyombo vya habari nk haya sikuyasikia popote sio kwenye kampeni zao wala kwenye ilani ya chama chao na kabala ya awamu hii sikuwai kuyaona.

Jambo lingine kubwa kuliko yote vita ya kusimamisha uchumi aiwezi kuwaacha pia salama maisha magumu sana mtaana biashara zimefungwa kilakitu kimesimama kila mtu anauza alicho nacho ili kujikwamua tena kwa bei ya kutupa watoto wako majumbani nusu mwaka watu ada shida kodi za pango shida tafula kila kona.

Jambo lingine CCM sio chama cha kuaminika tena kipo kwajili ya kuongeza umasikini sio kama malengo yake yalivyokua mwanzo, mwisho Lissu hanunuliki hata apewe container 1000 za40ft zenye not za $ 100 nizaidi ya uzalendo kwa mazingira hayo toto Tundu akipitishwa tu na Chedama kugombea ccm imekula kwao anaenda kutibua mipango yao yote na CCM wanalijia ndio maana anawanyima usingizi pia Chadema wakijichanganya kwenye ili jambo pia na mimi sipangiwi kura yangu ni mpigie nani.
 
Hofu ya mapokezi na kuwania Urais si unajua ile ni mali binafsi ya wana CCM
 
CDM 2015 ni kama kama hakukua na kampeni kutokana na mgombea kuwa Lowasa, agenda za kuongea hazikuwepo.
2020 akiwa Lissu kila mkutano utakua ni moto wa kuotea mbali, wakati huo JPM atakua anaimba SGR, vyeti feki (isipokua cha bashite) na 'stiglaz goji', changanya na hukumu ya mahaka kuu kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi lazima wawe na hofu.
 
Hofu yao kubwa wanajua kabisa Magufuli hana uwezo kwa kujenga hoja za ushawishi kwa wananchi kama alivyo Lissu. Sasa hivi wanabaki kuchomekea eti Magufuli amefanya maendeleo makubwa na kuwajali wanyonge. Je ni mnyonge gani kafaidika na Magufuli kiasi kwamba akija rais mwingine huyo mnyonge atakosa hiyo faida?

Na ukiwafuatilia sasa hivi wanajaribu kuwadanganya wapinzani eti mtu yoyote asigombee kisa Magufuli anakubalika sana. Magufuli anakubalika kwa viashiria gani? Maana kama ni siasa hayuko tayari wenzake wafanye, kama ni vyombo vya habari hataki vinavyotoa habari za upande wa pili bali zile anazotaka yeye.

Hofu yao nyingine ni kwamba Lisu atakapoingia kwenye uchaguzi itakuwa ngumu kumuhujumu kwani tayari jumuiya ya kimataifa itafuatilia nyendo zake. Na hatari kubwa iliyo mbele yao ni iwapo Lissu atakubali kuibiwa kura na kukubali kukaa kimya.
They surely know kwamba lissu hatakubali na hatanyamaza kuibiwa kura. Lissu ni mmoja tu; ila walio nyuma yake ni maelfu kwa mamilioni ndani na nje ya nchi waliotayari kufanya lolote atamkalo.

Magufuli ana ulinzi mzito sana. He got money and power to do anything. Ila hana amani na utulivu wa moyo.
 
Wakati uchaguzi mkuu ukiwa unakaribia ccm wameanza kupata hofu na Tundu Lisu,
Hofu hiyo inakuja ikiwa chama chake cha Chadema bado Hakijaweka wazi ni nani kitaenda naye kama mgombea urais wao mwakani.
CCM imekuwa ikimzungumzia sana Lisu kama mgombea urais wa upinzani, wakati wapinzani wenyewe hawajakaa chini kuamua ni nani apeperushe bendera yao ifikapo mwakani.
Kama wataalam wa mambo ya utabiri walivyo nao wameanza kubashiri uchaguzi mkuu ujao kuwa utakuwa mgumu Mara mbili kwa ccm kuliko ilivyokuwa mwaka 2015
Huku wengine wakidai huenda CCM ikashuhudia mgombea wao akiongoza kwa muhula mmoja tu tofauti na ilivyozoeleka.
Hayo na mambo mengine yameanza kuitia homa CCM juu ya ni mgombea gani upinzani utamsimamisha mwakani.
Huku upinzani ukiwa uko kimya kuhusu ni nani atasimama mwakani kama mgombea wao wa urais, CCM wao wana hofu na Tundu lisu, MTU ambaye aliponea chupuchupu kuuawa na wabaya wake kisiasa.
Je, ni kwa nini CCM wanamzungumzia sana Lisu, wakati upinzani bado haujaamua ni nani apeperushe bendera yao mwakani katika kinyang'anyiro cha urais.
Hii hofu inatoka wapi
Wakati huo huo chama chake cha CHADEMA wao wako bize na mikutano yao ya ndani kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi wa kumi.
View attachment 1108032
Bila kujali kama chama chake kitampa ridhaa au la! Ila mi bado nashangaa uponyaji wake jinsi gani ni mkubwa mno. Juzi juzi tu niliweka uzi wa jinsi gani namstaajabu Mungu alivyomponya watu wengine walikejeli. Binafsi ninaamini kuna KUSUDI KUBWA LA MUNGU KUMPONYA HUYU MTU. SISEMI TU LA KISIASA ILA PENGINE LA KIROHO PIA. Muda utasema tu tusubiri
 
Hofu yao kubwa wanajua kabisa Magufuli hana uwezo kwa kujenga hoja za ushawishi kwa wananchi kama alivyo Lissu. Sasa hivi wanabaki kuchomekea eti Magufuli amefanya maendeleo makubwa na kuwajali wanyonge. Je ni mnyonge gani kafaidika na Magufuli kiasi kwamba akija rais mwingine huyo mnyonge atakosa hiyo faida?

Na ukiwafuatilia sasa hivi wanajaribu kuwadanganya wapinzani eti mtu yoyote asigombee kisa Magufuli anakubalika sana. Magufuli anakubalika kwa viashiria gani? Maana kama ni siasa hayuko tayari wenzake wafanye, kama ni vyombo vya habari hataki vinavyotoa habari za upande wa pili bali zile anazotaka yeye.

Hofu yao nyingine ni kwamba Lisu atakapoingia kwenye uchaguzi itakuwa ngumu kumuhujumu kwani tayari jumuiya ya kimataifa itafuatilia nyendo zake. Na hatari kubwa iliyo mbele yao ni iwapo Lissu atakubali kuibiwa kura na kukubali kukaa kimya.
Wanahofu kwelikweli. Wenye akili ndani ya ccm wanaona Jpm hana uwezo hata kidogo wa kujibishana kwa hoja na Lissu.
Katazo la vyama kufanya siasa dhidi ya CCM kwa kipindi chote hiki halikufua dafu wala kuua upinzani jee hiyo miezi mitatu ya kampeni ambayo hawawezi kuzuia sumu kumwagwa hali itakuwaje kwao?
Mbaya zaidi ni kuwa zaidi ya nusu wanachama wa ccm hawamuungi mkono tena Magu kwa jinsi alivyokwamisha maisha ya familia moja moja
 
Exactly! Hapo ndio hofu ya ccm academia chini ya jiwe wanapopata hofu. Na matumizi ya nguvu hayajakaa vizuri japo ndio mbinu yao kuu.
 
Suala la nguvu tena ni shaka kwao kwani macho ya kimataifa yako wazi kuliko nyakati zote. Wakurugenzi nao sasa stop. Kule Zenj nako hata walete kina Jecha 10 muziki hawatauweza kabisa.
Sasa ccm watabakia wapi? Kumbuka ccm bila kuwa chama tawala kinapotea kama upepo!
 
Chadema hata wamweke nani hawawezi kumshinda ccm.... 100% 2020 ccm itachukua majimbo mengi hata kuliko chaguzi zilizopita
 
Back
Top Bottom