Hodi mi nasema hodi


JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
43
Points
0
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined Nov 18, 2012
43 0
Hodi naipiga humu,JENDALUJEJE nasema,
:violin:Imeniingia hamu,Jukwaani kuja sema,
Mawazo mengi matamu,ya kumeza si kutema,
Hodi mi nasema hodi,ndio kwanza naingia.

Jamvini nasogelea,KARIBU naisubiri,
Kwa pupa sitoingia,subira yavuta heri,
Enyi mlotangulia,nasema SABALKHERI,
Hodi mi nasema hodi,ndio kwanza naingia.

Midomo mkifungua,tabasamu mkaweka,
:violin:Woga shaka nitavua,na imani nitaweka,
Ndugu mkinitambua,makazi nitayaweka,
HODI MI NASEMA HODI,NDIO KWAANZA..NAINGIA!
 
BHULULU

BHULULU

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Messages
4,904
Points
1,250
BHULULU

BHULULU

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2012
4,904 1,250
Karibu, lakini najiuliza swali hili,siku hizi hakuna jukwaa la utambulisho?Maana naona wageni wanapotea kila siku.
 
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Messages
8,113
Points
1,500
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2011
8,113 1,500
Karibu sana jamvini, jisikie uko nyumbani, wala usiwe na soni kumwaga yako maoni, nasema tena karibu ukaribie jamvini.
 
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
43
Points
0
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined Nov 18, 2012
43 0
Karibu, lakini najiuliza swali hili,siku hizi hakuna jukwaa la utambulisho?Maana naona wageni wanapotea kila siku.
Kama njia mepotea,mwenyeji ngesaidia,
Vipi wanitangazia,jamvini kuniumbua?
Taratibu ngenambia,wapi pa kuingilia,
Haya sasa nasubiri,mjuzi nielekeze.
 
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
43
Points
0
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined Nov 18, 2012
43 0
Karibu sana jamvini, jisikie uko nyumbani, wala usiwe na soni kumwaga yako maoni, nasema tena karibu ukaribie jamvini.
Asante kwa ukarimu,jamvini ngoja nikae,
Umeona umuhimu,mgeni kulonga nae,
Hakika umenikimu,BHULULU achana nae,
Kwa hakika sitasita,maoni yangu kutoa.
 
Jidu

Jidu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Messages
1,179
Points
1,500
Jidu

Jidu

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2011
1,179 1,500
Hodi naipiga humu,JENDALUJEJE nasema,
:violin:Imeniingia hamu,Jukwaani kuja sema,
Mawazo mengi matamu,ya kumeza si kutema,
Hodi mi nasema hodi,ndio kwanza naingia.

Jamvini nasogelea,KARIBU naisubiri,
Kwa pupa sitoingia,subira yavuta heri,
Enyi mlotangulia,nasema SABALKHERI,
Hodi mi nasema hodi,ndio kwanza naingia.

Midomo mkifungua,tabasamu mkaweka,
:violin:Woga shaka nitavua,na imani nitaweka,
Ndugu mkinitambua,makazi nitayaweka,
HODI MI NASEMA HODI,NDIO KWAANZA..NAINGIA!
Salam twaitikia, huu ndio ufunguo,
Acha woga karibia,hapa ndipo kimbilio,
Usihofu nakwambia,hutopata karipio,
Karibu ndugu karibu,uje pata matukio.
 
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
43
Points
0
JENDALUJEJE

JENDALUJEJE

Member
Joined Nov 18, 2012
43 0
Salam twaitikia, huu ndio ufunguo,
Acha woga karibia,hapa ndipo kimbilio,
Usihofu nakwambia,hutopata kalipio,
Karibu ndugu karibu,uje pata matukio.
Asante JIDU pokea,kwa hofu kuniondoa,
Funguo nishapokea,na ndani nimeingia,
Roho imenitulia,mazuri nasubiria,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.

Nimeanza pitapita,huku kule humu ndani,
Ya busara kutafuta,yafaayo maishani,
Mengi nimeshayapata,na hayana nuksani,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.

Vyumba vingi nimeona,ila hiki chanivuta,
Kidogo nimesonona,wengi wanaokipita,
Najua wanakiona,ila lugha mewapita,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.

JIDU na wewe GLOBU,hakika mmenivuta,
Kuwasifu ni wajibu,subira mmeivuta,
Acha nende taratibu,uzoefu kutafuta,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.
 

Forum statistics

Threads 1,294,755
Members 498,034
Posts 31,187,163
Top