Hobbie kidogo intoe Ben roho...

Hobbie kidogo intoe Ben roho...

Hahaaa..mkuu pole sana,
Umenikumbusha mwaka jana nlikua na mkutano Bangkok, tulikua wabongo wawili, na jamaa wengi toka nchi nyingine hasa ulaya. Basi yule jamaa yangu ilikua siku yake ya kuzaliwa (Birthday), jamaa wakamwandalia surprise ya kumtosa kwenye swimming, .. Wakavizia ile tunapata chai jion tuko karibu na swimming wakamshika jamaa juu kwa juu wakamtupia kwenye swimming.
Jamaa hakuwahi kuogelea maishani mwake,(yeye anapiga kazi Moshi-hakuna bahari then kuna baridi), hapo kilikua kituko cha mwaka, alipiga kelele kila mtu alishtuka, aliomba msaada, basi ikabidi jamaa mwingine ajitose kumuokoa. Kila mtu alikua hoi kwa kicheko, halafu jamaa alikua kavaa nguo zake za kuchomekea bado, simu, wallet na kila kitu vililowa.Nlicheka sana hasa alipokuwa anatapatapa na kuomba msaada kwa kiswahili wakati hakuna mtu anayejua kiswahili pale tofauti na mimi.
MAJI NOOOMA

ha ha ha ha ha mtu katoka moshi unamwingiza kwenye maji mmmh mngempeleka kupanda milima...... naogopa maji sana
 
Ben si nimekariri hobbies, sasa kila demu akiniuliza , "Ben hobbie yako nini"? majibu yanakuaga, Swimming, reading novels, listening to music and going out. Sasa kiranga kilichonipata jana usiombee kikikute yule demu anayeongea kizungu alitumia msg akiniomba outing mkuu nikajikoki nikajua itakua kama ya niliowazoeaga wa kwenda kwenye bar basi nimempitia bint kwake, kapendeza mwenyewe na kipensi chake na mawani meusi...mkononi kabeba kijikipapu flani namuuliza unapendeleaga wapi akaniambia beach ya kule mbali, nikasema sio ishu.

Haooo kufika ben naongoza njia kaunta binti kanishika mkono kaniambia "lets go and get some tan ben" mimi huyoo nakenua meno tu. Kumbe hiyo tan aliyoisema ni kwenda kujikaanga juani. Ben nimetoa nguo niko na boksa yangu basi na huu wembamba mbavu zimenitoka jua nalisikia mpaka kwenye maini. Kumbe binti kijikikapu alichobeba kimajaa novels, mimi na novel wapi na wapi, nikashikashika zilizokua na picha zikanichosha basi si nikasema ngoja nijipooze hapo kwenye swimming pool, kumbe wakati naelekea binti alininyemelea nyuma.

Wakati bado natafakari si akanisukuma kwenye maji, yalaaaa, kama sio wale jamaa waokoaji leo nisingekua hapa kwa kweli, basi ben mwanzoni ili kuua soo nilikua naomba msaada kishkaji..yaani kiaina si kwa sauti saaana, ili binti asishtukie sijui kuogelea, aaaa nilipooona hali inakua mbaya wacha nipige ukunga, watu wote walikusanyika poolini, basi baada ya kuokolewa kila mtu ananipa pole, nikazuga muscles zilinishika nikashindwa kukata maji, ni noma kuweni makini na hobbies mnazozisemaga jamani.
Unikumbusha mbali sana kujifanya ujuaji demu mmoja sista duu anajafanya anajua sana ung'eng'e akatolewa out one day kufika five star hotel jamaa akamwambia muudumu niletee menu kwanza basi demu wakamuliiza vipi na wewe dada akadakia nipe hiyohoyo menu ila usiweke pilipili tomatoo kwa mbali na mayoniza kidogo nusu nizimie kwa kicheko.
 
Mkuu you made my evening, nimecheka hoi hapa. Umenifanya nihadithie wafanyakazi wenzangu hapa maana walikuwa wanashangaa nilivyocheka. ha ha ha hah!!
 
Hahahahahaha we jamaa unajua kutunga comedies
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom