Hobbie kidogo intoe Ben roho...

Hobbie kidogo intoe Ben roho...

Hahaaa..mkuu pole sana,
Umenikumbusha mwaka jana nlikua na mkutano Bangkok, tulikua wabongo wawili, na jamaa wengi toka nchi nyingine hasa ulaya. Basi yule jamaa yangu ilikua siku yake ya kuzaliwa (Birthday), jamaa wakamwandalia surprise ya kumtosa kwenye swimming, .. Wakavizia ile tunapata chai jion tuko karibu na swimming wakamshika jamaa juu kwa juu wakamtupia kwenye swimming.
Jamaa hakuwahi kuogelea maishani mwake,(yeye anapiga kazi Moshi-hakuna bahari then kuna baridi), hapo kilikua kituko cha mwaka, alipiga kelele kila mtu alishtuka, aliomba msaada, basi ikabidi jamaa mwingine ajitose kumuokoa. Kila mtu alikua hoi kwa kicheko, halafu jamaa alikua kavaa nguo zake za kuchomekea bado, simu, wallet na kila kitu vililowa.Nlicheka sana hasa alipokuwa anatapatapa na kuomba msaada kwa kiswahili wakati hakuna mtu anayejua kiswahili pale tofauti na mimi.
MAJI NOOOMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom