Hobbie kidogo intoe Ben roho...

Hobbie kidogo intoe Ben roho...

benteke

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
1,305
Reaction score
1,069
Ben si nimekariri hobbies, sasa kila demu akiniuliza , "Ben hobbie yako nini"? majibu yanakuaga, Swimming, reading novels, listening to music and going out. Sasa kiranga kilichonipata jana usiombee kikikute yule demu anayeongea kizungu alitumia msg akiniomba outing mkuu nikajikoki nikajua itakua kama ya niliowazoeaga wa kwenda kwenye bar basi nimempitia bint kwake, kapendeza mwenyewe na kipensi chake na mawani meusi...mkononi kabeba kijikipapu flani namuuliza unapendeleaga wapi akaniambia beach ya kule mbali, nikasema sio ishu.

Haooo kufika ben naongoza njia kaunta binti kanishika mkono kaniambia "lets go and get some tan ben" mimi huyoo nakenua meno tu. Kumbe hiyo tan aliyoisema ni kwenda kujikaanga juani. Ben nimetoa nguo niko na boksa yangu basi na huu wembamba mbavu zimenitoka jua nalisikia mpaka kwenye maini. Kumbe binti kijikikapu alichobeba kimajaa novels, mimi na novel wapi na wapi, nikashikashika zilizokua na picha zikanichosha basi si nikasema ngoja nijipooze hapo kwenye swimming pool, kumbe wakati naelekea binti alininyemelea nyuma.

Wakati bado natafakari si akanisukuma kwenye maji, yalaaaa, kama sio wale jamaa waokoaji leo nisingekua hapa kwa kweli, basi ben mwanzoni ili kuua soo nilikua naomba msaada kishkaji..yaani kiaina si kwa sauti saaana, ili binti asishtukie sijui kuogelea, aaaa nilipooona hali inakua mbaya wacha nipige ukunga, watu wote walikusanyika poolini, basi baada ya kuokolewa kila mtu ananipa pole, nikazuga muscles zilinishika nikashindwa kukata maji, ni noma kuweni makini na hobbies mnazozisemaga jamani.
 
mmmmhhh benteke vipi sasa baada ya hapo uliendelea kutembea kwa kujidai kama kawadia yako au kujidai kote mfukoni?
 
Last edited by a moderator:
mmmmhhh benteke vipi sasa baada ya hapo uliendelea kutembea kwa kujidai kama kawadia yako au kujidai kote mfukoni?

Blue G nilitembea kwa kuchechemea......ilibidi wahudumu wanishike mpaka kwene gari......nilisema muscles zimenishika....🙂
 
Last edited by a moderator:
OOOOOOhhhh benteke u made my day

be urself bhana blah blah blah za nni
 
Last edited by a moderator:
Mimi kuogelea sijui kabisa. Kuna siku tumeingia kwenye pool mie na madogo bana nikajifanya nashindana nao nikasogea nikateleza mamaaaaa nilikunywa kama robo lita ikabidi ninvute dogo nikapanda juu yeye chini sababu anajua ogelea. Tokea siku hiyo maji nisiyoogopa ni ya kwenye beseni tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom