Black poison The Factor
JF-Expert Member
- May 31, 2020
- 856
- 1,262
Nimekuwa najiuliza sana maswali bila majibu, hizi team za Singida zinakumbwa na tatizo gani?
Ilianza Singida united, ikaja vizuri kabisa na Mashabiki wa mpira wakajua kwamba mpinzani amekuja, badala ya Azam ambaye yupoyupo tu kama akina Kagera sugar ambao wao kikubwa wawepo ligi kuu tu.
Lakini msimu wa pili tu mambo yakawa tofauti Singida wakawa na migogoro ya ndani kwa ndani mpaka jahazi likazama.
Ikaja hii Singida big stars (Singida fountain gate) ikaonekana tena kwamba mshindani kaja, kabla hata ya kufika popote ikauzwa, mi nilijua kabisa kwamba yatatokea yaleyale tu. Wamekua kama vile wanatupima akili, wanaanza kwa kasi sana halafu wakipata ile attention ya Mashabiki wanaingia mitini.
Kwakweli kwa huu mchezo wao ni bora wasipewe umiliki wa team maana hata hii ikishuka watanunua tena na kuja kufanya madudu yao, maana wamiliki ni wale wale tu isipokua majina ya team ndo tofauti.
Nimeangalia mwenendo wao kwasasa kwenye ligi wana hali ngumu sana, imekuwa kichaka cha kugawa point.
Leo Simba ilikuwa ashinde hata 5 pale ila umakini wao umewanyima ushindi mkubwa,
Ile mechi kama ingekuwa ya yanga hata saba wangekula wale halafu maneno ya bahasha yaendelee, kama ilivyo kawaida.
Hizi team za mkoani Singida kama vipi zisipande daraja kabisa wala wasiuziwe team maana ni upuuzi tu unaofanyika.