Apologise lady
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 5,980
- 3,115
Kuna tabia humu zinakera sana, zikome haraka sana.
- Tabia ya kila ukiletwa uzi na mwanaume kuhusu mke wake wanaume karibu wote wanamshauri mwenzao amwache mke wake, hiyo tabia mkome mkome, hamjui upande wa pili upoje wala kama yaliyosemwa ni ya kweli au mtu anatafuta sababu tu nyie mnapigilia msumari wa moto.
Acheni hiyo tabia kabisa, humu tumo na fake id unaweza kuta unaropoka ropoka kumbe unavunja ndoa ya dada ako, shangazi yako na acheni kabisa hii tabia.
- Tabia ya mtu anaamua tu kuja kudhalilisha wanawake humu nayo ikome haraka, palipo na mwanaume lazima kuna mwanamke.
Sasa iweje kila siku wanaume muishi kwa kuwakashifu wanawake etii kisa tu mtu kakunyima papuchi basi unakuja kutukana wanawake woteee duniani.
Hii tabia ikome haraka.
- Tabia ya watoto wadogo kuingilia mada za watu wazima ikome, subirini ikifika wakati wako utachangia, acha kujikomaza, ka jogoo anayejifunza kuwika, anawika hata saa 7 mchana.
- Mwisho: Tabia ya mtu kuja pm wakati hUjui amekuja pm kufanya nini ikome, au mtu unakuja pm kuleta ubabe nayo ikome Ubabe peleka ulingoni.
Pm ni sehemu ya kuongea faragha na jambo la msingi, sio kuja kujikanyaga kanyaga na kumaliziana charge OVER.
Angalizo: Kama nimekukera kuwa mpole usije na matusi hapa.
[/SIZE][/COLOR]