Hizi sare za kijani za nini hapa?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Wadau,
Makamu wa Rais ailikuwa hapo Songea kwa ajili ya uzinduzi wa siku ya Mazingira duniani. Lakini ukijaribu kuiangalia hiyo picha kwa makini utaona kuna sare za kijani na njano za chama fulani. Nashindwa kuelewa kulikuwa na uhusiano gani wa hiyo sherehe na hizo sare!!
Nawakilisha.

7.jpg
 
acha wazivae vae mara ya mwishomwisho years to come watakuwa wanaona aibu hata kuziangalia zitakuwa doomed
 
Acha kufuatilia kazi za watu, hivi unajua kuvaa hizo sare ujira wake ni Tshs5,000 na zaidi ya hapo unaachiwa uende nazo zaweza kukusaidia mbele ya safari. Bei ya kofia sokoni ni wastani wa Tshs10,000 Tshirt Shs5000 jumla mtu anaingiza thamani jumla ya mavazi na pesa Ths20,000. Hii inalipa hata ikinikuta mimi nikiwa likizo kijijini kwetu sitoiacha.:pound:
 
Ni kweli kwamaba Rais na hata Makamu wa Rais wanatoka kwenye chama cha siasa, ni vizuri huo ukereketwa ukaonyeshwa wakti wa kampeni za uchaguzi, baada ya uchaguzi kiongozi ni wa watanzania wote hata wasio kuwa na chama cha siasa, labda kama sherehe zitakuwa za kichama. Lakini sherehe ya Kitaifa kama hii, tudumishe utaifa wetu kwa kuondoa siasa.
 
Ni umaamuma wa baadhi ya watu wasiojua kutofautisha shughuli ya kiserikali na ya chama
 
Acha kufuatilia kazi za watu, hivi unajua kuvaa hizo sare ujira wake ni Tshs5,000 na zaidi ya hapo unaachiwa uende nazo zaweza kukusaidia mbele ya safari. Bei ya kofia sokoni ni wastani wa Tshs10,000 Tshirt Shs5000 jumla mtu anaingiza thamani jumla ya mavazi na pesa Ths20,000. Hii inalipa hata ikinikuta mimi nikiwa likizo kijijini kwetu sitoiacha.:pound:

Yaani wewe umenichekesha sana. Na hivi tayari utakuwa umeshapata zako kilaji, weee!!!!! Kama nakuona mwenyewe unavyodundika nazo.
 
Mimi sina mapenzi na chama chenye hiyo sare lakini nashangaa kwann uhoji hao watu kuvaa hizo sare kwenye shughuri ya kiserikali wakati viongozi wengine wamegeuza sare za vyama vyao kama mavazi ya kawaida tena popote huyavaa: kwenye midaharo, makongamano, mahakamani, kwa waandishi wa habari nk. Tujadili mambo ya maana siyo kuvaa sare. Peoooooples' power!
 
ni adiction ndugu yangu...watu wengine kama hamnazo...wameishaona ndo nguo hata wakiingia kwenye mitumba wanachukua hizo hizo
 
Back
Top Bottom