Hizi propaganda zinakubalika kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi propaganda zinakubalika kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Du Bois ideas, Apr 27, 2011.

 1. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Mimi naomba mnisaidie kuelewa juu ya siasa zinazoelezwa na CCM hasa kila wanapokuwa katika mikutano yao iwe mijini au vijiji

  Kuhusu Amani Tanzania:

  Kila wanapokuwa katika majukwaa wanaeleza kuwa, Tanzania inaamani kwa sababu ya CCM na kwamba siku itakapoondoka CCM madarakani na kuchukuliwa na wapinzani nchi itakuwa katika vita na hatimaye watu kuacha makazi yao. Katika propaganda hii mini nina maswali ya kuujiuliza kwamba;

  1. Hivi CCM ikiondoka madarakani vita itatokeaje?

  1. Nani atasababisha vita hiyo ikiwa CCM itakubali kukabidhi madara kwa chama kilichoshinda bila kukatalia ikulu?
  Propaganda hii imekuwa ikitamkwa kila kunapokuwa na mikutano ya chama hiki. Katika kujiuliza kwangu nimekuja kugundua kuwa kumbe CCM ndiyo itakayosababisha vita katika nchi na siyo vyama vya upinzani. Na itasababisha kwa kuwa siku watakayoshindwa watakatalia Ikulu kama yule jamaa wa Ivory Coast na kwa njia hiyo watatoka kwa kuleta vita. Je, nyie wana JF, mnalionaje hili na propaganda hii nyepesi?

  Vyama vya upinzani kutumiwa na nchi za Magharibi:
  Hii nayo sasa inataka kuwa propaganda ya CCM katika mikutan yao kila sehemu kwa kuwatolea wananchi mifano ya Libya, Ivory cost, Misri, Tunisia n.k. Burunid na Rwanda sasa hawazitaji sana sijui kwa nini?

  Maoni yangu:

  1. Hiki chama kinachoongozwa kwa falsafa ya “NGUVU YA UMMA” naomba kijitahidi kupita kila kata na kijiji nchini ili kuondoa sumu ya hofu ambayo wananchi wamepandikizwa kutokana na ukosefu wa elimu ya uraia na kuwa wanyonge kwa CCM. Wana wake wengi nchini hasa wanaoishi vijijini wamepigwa na ganzi ya sindano hii na kupoteza haki yao ya kikatiba na hii imewapelekea kuwa wateja wa CCM.

  1. CDM watendaji wake wasikae ofisini bali wawe wanashinda katika vijiji na kata kutoa elimu ya uraia bila kutegemea ugeni wa Viongozi wa makao makuu, wabunge pia katika maene yao waendelee kuishambulia smu hii mbaya kwa Taifa letu, kwani CCM ina hati miliki na nchi hii?

  Naomba kuwasilisha.

   
 2. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Miaka hii mitano ni vyema ikatumika kuimarisha chama kwa kufungua matawi katika vijiji vyote vya Tanzania maana mijini kote wanakielewa chama na nguvu zake inafaa kwasasa viongozi na wote wenye nia njema na nchi yetu waeneze ujumbe wa NGUVU NYA UMMA ili ueleweke kila kona na watu wote hasa wa vijijini
   
 3. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kila kitu kinawezekana kwenye mipango thabiti na ya muda mrefu
   
Loading...