Kweli bana.Mwananchi walimaanisha URAFIKI WA MASHAKA!!!
Tecnolojia inaniumiza kicha sana ngoja nikatoe Lock halafu nitarejea!
Hiyo ni picha moja copy ya pili imefanyiwa kitu inaitwa "mirror effect" kama vile unapojitazama kwenye kioo, watu wa zamani ambao tunazijuwa "negative" ni rahisi kuelewa, siku hizi unacheza na vi "software" vya picha kwenye kompyuta vinakupa hiyo "mirror effect", tazama inayoonyesha wanasalimiana kwa mkono wa kushoto maandishi ukutani nayo yamebadilika.
yaelekea kijana wetu hazijui negative. Hata kioo hajui?
Ni picha mbili tofauti lakini hata hivyo hiyo picha ya chini ukitizama maandishi ya ukutani yanaashiria imekuwa 'mirrored'...sijui kwa nini! Hata kama wote wangekuwa ni left handed, sio 'utamaduni wetu' kusalimiana kwa mikono ya kushoto.
Mkuu, ukiangalia bacground banner utagundua kuwa picha moja wamei-flip horizontally.View attachment 42057
Hii picha ni kutoka gazeti la majira... ambayo nafikiri ipo sawa....hii ya chini sasa
View attachment 42058\
Hii picha imetoka gazeti la mwananchi....yapo mabo ya kujiuliza hapa... ni kweli hawa watu walikuwa wanasalimiana kwa mikono ya kushoto? kama ndio...kwa nini? kama picha imechezewa.....wahariri wa wa gazeti la Mwananchi walikuwa na maana gani?? nisaidieni.....
Wewe inaonekana mwalimu wako alipata tabu sana darasani, elewa anachotaka kufahamu muuliza swali, je hawa watu walisalimiana kwa kutumia mikono gani? ya kushoto au ya kulia? hajauliza hadithi za studio huwa kunafanyika nini.