Hizi ni dalili za mwanamke anayekupenda kwa dhati toka moyoni, ila hawezi kukuambia

Mambo ya kizamani hayo....

Kukuangalia na kuchekacheka hata kwa vitu visivyochekesha...!? Hii sasa ni ujuha na umwehu
 
Kumekuwa na imani potofu kwa wanawake kwamba hawawezi kumwambia ukweli mwanaume anampenda kwanza mpaka mwanaume aanze lakini ukweli usiopingika ni kwamba wao pia hupendi na mara nyingi wao wakianza kupenda hupenda kweli kufikia stage hata ya kuhisi kuumwa. Hizi ni dalili za mwanamke anaekupenda ila anagoma kukwambia tu.

1. KUKUTEGA ILIKUJUA THAMANI YAKE KWAKO
Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda na kumthamini au la mfano wa mambo hayo ni kama kujifanya anaumwa na kauangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake.

2. KUPENDA KUCHEKA TENA MUDA MWINGINE KWA NGUVU
Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli.

3. WIVU
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi na hupenda yale afanyiwe yeye tu hata kama sio mpenzi wako.

4.HUKUMBUKA MATUKIO MUHIMU YOTE KUHUSU WEWE
Anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifauli mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza.

5. HUPENDA KUANGALIANANA WEWE MUDA MWINGI
Eye contact hupendelea sana kukuangalia machon muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utamuelewa ni kiasi gani anakupenda kupitia vile anavyokuangalia. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda hivyo huweka jicho la wizi na kukuvizia.

6. HUPENDA KUKAANA WEWE MUDA MWINGI NA KUKUJUAZAIDI
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe na akikaa na wewe hupendelea sana mwanzoni kukujua wewe zaidi na hukujengea mazingira ya wewe uwemuwazi ili umwambie mengi kuhusu wewe na pia akiwa na wewe atakuwa muwazi zaidi hadi mavazi aliyovaa hupenda sana kujua yako na kukuambia yake na hupenda kujua ni mavazi gani yeye akivaa anakuvutia zaidi na atajitahidi kuwa anavaa ya style hiyo kukufurahisha.

7.YUPO TAYARI KUJISACRIFICE
Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utamuona vipi huyo msichana alivyo kwako na kwa wengine. Yaani yupo tayari akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwambia hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.

8. HUPENDA KUTATUA MIKWARUZANO YENU KWA AMANI
Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia nakupenda.Kwa kuwa anakupenda endapo ikitokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.

9. HUPENDA KUKUNUNULIA ZAWADI ZA MITEGO
Mwanamke anaekupenda hupenda kujua mengi sana kuhusu wewe na hapo inamsaiia kukununulia zawadi za mitego kama boxer , na mara nyingi hupenda rangi nyeupe, au kukununulia perfume , sabuni ya kuoge ya manukato,soksi, vest, bukta, saa,raba, t-shirt. Na kama mkitoka wote mkaenda shopping ataakutega kwa kukuonyesha vitu na wewe ukionekana umependa kitu hatonunua siku hiyo ila atanunua siku inayofuata na kukuletea kama suprise.

10. KUPENDA MLE WOTE
Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi hupendelea msosi mle sehemu mmoja na kama ikitokea mwanaume hawezi kuhama sehemu anayokula mwanamke yupo radhi kubadili na kumfuata mwanaume hatakama sehemu hiyo yeye haipendi na kama unakula kwako basi atakutega na kuja kupika kwako ili mle na atakuwa anapenda kununua vitu vya kupika ili tu akutekena uone upendo wake.

Ukiona Dalili kama Hizi Mwanaume Tafadhali Fanya mpango wa kumweka ndani (oa) Mwanamke huyo kabla ujachelewa alafu ukaja kuangukia kwa wale wanawake wenye sifa ya Pasua kichwa!!!!

Good Thread.. Kwa siku hizi not all of them are like that, things change.. Nimegundua Nina 5 ya hayo uliyoweka juu ..hahahaaahaa... I will try nireach hizo 10 ila kupretend sitaki.. I will try my best kujifunza muweka Uzi ., kama nitaweza jifunza , haaahahahaaa... Thanks..
 
Wana mbinu nyingi sana. Kuna mwanamama mmoja tulikuwa tunafanya nae kazi eneo moja; akiniona nipo mahali, atasalimia wengine wote, kutoa mimi. Halafu ata-front tu kiaina (indirectly). Boss wake ni mchizi wangu, so katika story akawa anajua vituko vya yule manzi, akawa anatukutanisha kiaina. Eventually nilikuja kugundua kwanini yule bibie alikuwa anafanya vile.
Ulijua nn sasa weka wazi
 
Hakuna formula! Mwingine anakuwa hajakupenda anataka kuchop ur money so anakuonesha dalili zote hapo juu, unajua yuko real! Mwingne anakuwa na true feelings lakini hawez dare kufanya chochote, ataishia tu kuwa anakuangalia sana na kuumia tu moyon
Ukiwa makin utamgundua tu ukiona yupo kivibuti zaid basi yatakikana umpige chini mapema
 
Yote hayo na zaidi wengine tumefanya ila unakutana na wanaume wasio na shukrani, hawapendeki. Au huwa hawajali hisia au mambo mazuri wanayotendewa. Sijui niseme ni washamba au ni wapori. Yaani ukimpata anayekuelewa mwanamke unafurahi na mapenzi tele ndani ya nyumba.
 
11. Asiyekupiga mizinga jioni yake au kesho yake baada ya TONGOZO.
 
Yote hayo na zaidi wengine tumefanya ila unakutana na wanaume wasio na shukrani, hawapendeki. Au huwa hawajali hisia au mambo mazuri wanayotendewa. Sijui niseme ni washamba au ni wapori. Yaani ukimpata anayekuelewa mwanamke unafurahi na mapenzi tele ndani ya nyumba.
Dada ukimpenda mtu yeyote hakikisha na yeye anakupenda usipende sehemu usiyopendwa utaumizwa moyo lakin ukimpata Yule ambaye wewe unampenda na yy amekufa na ameoza kwako maisha ndani nyumba huwa yanaenda vizuri
 
Yaani umenena sana kwa kweli. Hivi hawa wanaopenda kwa kweli kwa kufia wapo tena duniani au walishakufa wote? Ningempata mmoja tu wa namna hii basi maisha yangekuwa mazuri sana. Kweli unampenda mtu ila haoni mpaka unataka kupata kichaa au kichwa kinapata moto. Kuna rafiki yangu alipata mpenzi, wakawa na mapenzi motomoto kwa kipindi cha miezi mitatu tu. Baadaye yule jamaa akaanza kutoa visingizio kuwa mara hiki mara vile hakuna tena mapenzi motomoto ila rafiki yangu akitaka kujitoa basi mwenzie anakuwa hataki na kumwambia anampenda ila ana shida mara kichwa hakija kaa sawa. Huu ni mwaka wa pil bado rafiki yangu ana imani kuwa jamaa anampenda. Nimeshauri amwache lakini hataki kabisa anasema ninasubiri atabadilika tu. Kweli ukipenda mtu haelewi maana ya kupenda ni shida sana. Wanaume muwe wa wazi kama humpendi au mapenzi yameisha sema wazi ili mwenzio achape lapa awe huru.
 
Ukiona upo kwenye uhusiano na mwanaume alafu yy ni wa kukuomba compan ya kwenda kula weekend na kuomba mzgo alafu hanampango wa kuja kuonana na wazee jua huyo anajuchezea na nyinyi mabinti msiwe wepesi kuwavulia watu kufuli mpaka muoane kwasababu mwanaume akisha kuonja na akaona udhaifu fulan bas atatumia iyo point of weakness kukuumiza ww
 
Wana mbinu nyingi sana. Kuna mwanamama mmoja tulikuwa tunafanya nae kazi eneo moja; akiniona nipo mahali, atasalimia wengine wote, kutoa mimi. Halafu ata-front tu kiaina (indirectly). Boss wake ni mchizi wangu, so katika story akawa anajua vituko vya yule manzi, akawa anatukutanisha kiaina. Eventually nilikuja kugundua kwanini yule bibie alikuwa anafanya vile.
Malizia palipobakia....
 
Back
Top Bottom