Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 13,388
- 21,371
- Thread starter
- #41
Changamoto sana hivyo vitu mkuu!Hii imenichekesha!
Changamoto sana hivyo vitu mkuu!Hii imenichekesha!
Tatizo ni kwamba siamini katika uchawi mkuuWajuvi wa uchawi watakwambia mizimu ya ukoo inakuandama!
Uwe na amani, ni ndoto tu! Vipi mazingira ya chumba/ kitanda yakoje? Kuna hewa ya kutosha, na wewe uzito wa mwili ni wa kawaida au uliozidi?Changamoto sana hivyo vitu mkuu!
Baba wa mbinguni akabadilishe chumvi yako ikawe sukariPole sana mkuu. Ndoto hizi zimenisumbua kwa kipindi kirefu sana. Yaani huwa naota narudishwa shule ya msingi kabisa, nipo na wenzangu darasani, inafika kipindi cha mtihani najikuta sijasoma kabisa, au nashindwa kabisa kukamilisha mitihani.
Siku moja nikaota nimerudishwa shule yangu niliyosoma secondary O level, nimepigishwa goti na mwl mmoja ambae hadi jina nalikumbuka (Though hatukuwa na mwl mwenye jina hilo) Tupo wawili na mwenzangu, Mimi nikiwa uchi bila nguo lkn mwenzangu alikuwa angalau amevaa nguo ya ndani. Nililia sana kwa yule mwl nikamwambia mbona mmataka kunirudisha huku wakati Mimi niliendelea na masomo??? Akaniambia basi nilikuwa sijui, akaniachia, baada ya hapo nikapumzika ndoto zile kwa muda Fulani lkn baada ya muda zikarudi tena. Yaani kuna wakati ninaota mfululizo sana kwa wiki ninaota hata Mara 3.
Kuhusu maisha kiukweli nimejaribu biashara nyingi za mtaji mkubwa hakuna hata moja niliyofaniliwa, na hata nikizalisha vizuri nadhulumiwa na kuibiwa. Nimejaribu kilimo niishia kupata hasara kubwa. Nilijaribu kusoma course Fulani Masters nikamaliza coursework vizuri kwenye desertation nilijikuta nimepata mitihani hadi nikaamua kuiacha. Na kipindi hiki ninasoma ndoto hizo nilikuwa nazipata sana. Nakumbuka siku moja niliota sauti inaniambia nimtafute Dada mmoja tusaidiane kufanya maombi ili niweze kumaliza course yangu. (Huyo Dada ni mtu ambae namfahamu vizuri tulishawahi kusoma nae zamani) kiukweli alikuwa ni mtu anaempenda Mungu sana na alikuwa mtu anae sali sana. Nilimtamfua lkn alikuwa anaishi mkoa wa mbali na Mimi, na kipindi hicho nilisongwa na matatizo na misusuko nikakata tamaa na course niliiacha bila kujali gharama ambayo nilikuwa nimetumia-ambayo ilikuwa ni kubwa sana.
Kama ID yako inasadifu unachoona kwenye ndoto hivi..mkuu mbona ndoto ya kawida tu,wenzio tunaotaga mijoka mpaka tunakimbiaga na vitanda
Mkuu pga goti umshukuru Mungu kwa namna anavyokupenda, nilishaota sana na nilipata msaada kwenye moja ya vitabu vya Mwakasege. Pitia hz dondoo hapa chini, cha msing usidharau ndoto. Mungu ana mpango kabambe juu ya malengo ulonayo.Mm ni kijana in the late 30's nimepita pita school vya kutosha tu, kuanzia O level, Advance mpaka chuo kikuu na kote huku kulikuwa kitonga tu kutokana na juhudi zangu ktk masomo, kiukweli Nina miaka zaid ya mi5 toka nimalize chuo lakin Mara kwa Mara nimekuwa nikiota kwamba nakutana na changamoto nyingi sana hasa ninapofanya mitihani, mfano ni Jana tu nimeota niko kwenye mitihani ya Necta ya form 6, nimechelewa kuingia kwenye chumba cha mtihani kama masaa ma 2 huku mtihani ukiwa ni wa masaa 3 maana nilikuwa nimechelewa kuamka hostel,
Sasa ile kufika wasimamizi wakanigomea kuingia kwenye chumba cha mtihani, nikajaribu kuwaomba wakaniruhusu niingie huku ikiwa imebaki SAA 1 muda kuisha, nilipopewa mtihani kuna wanafunzi wakawa wamemaliza wanatoka nje, hicho kitu kilinipa stress mwisho wa mtihan msimamizi anakuja kusanya sijajibu swali hata moja ndio nikashtuka usingizini......
Huu ni mfano mmoja tu lakini nishaota nyingi za mtindo huu na zinanikera sana ukizangatia sikuwa kuwa na changamoto za aina hii kote nilipopita, labda kuna chochote zinamaanisha?
Ulichoandika, jinsi ulivyo na ndoto zako ni 100% kwangu pia.Mm ni kijana in the late 30's nimepita pita school vya kutosha tu, kuanzia O level, Advance mpaka chuo kikuu na kote huku kulikuwa kitonga tu kutokana na juhudi zangu ktk masomo, kiukweli Nina miaka zaid ya mi5 toka nimalize chuo lakin Mara kwa Mara nimekuwa nikiota kwamba nakutana na changamoto nyingi sana hasa ninapofanya mitihani, mfano ni Jana tu nimeota niko kwenye mitihani ya Necta ya form 6, nimechelewa kuingia kwenye chumba cha mtihani kama masaa ma 2 huku mtihani ukiwa ni wa masaa 3 maana nilikuwa nimechelewa kuamka hostel,
Sasa ile kufika wasimamizi wakanigomea kuingia kwenye chumba cha mtihani, nikajaribu kuwaomba wakaniruhusu niingie huku ikiwa imebaki SAA 1 muda kuisha, nilipopewa mtihani kuna wanafunzi wakawa wamemaliza wanatoka nje, hicho kitu kilinipa stress mwisho wa mtihan msimamizi anakuja kusanya sijajibu swali hata moja ndio nikashtuka usingizini......
Huu ni mfano mmoja tu lakini nishaota nyingi za mtindo huu na zinanikera sana ukizangatia sikuwa kuwa na changamoto za aina hii kote nilipopita, labda kuna chochote zinamaanisha?
Ahsante, nmekopi ushauri wako mkuu, ubarikiwe, na mtoa hoja abarikiwe pia.Mkuu pga goti umshukuru Mungu kwa namna anavyokupenda, nilishaota sana na nilipata msaada kwenye moja ya vitabu vya Mwakasege. Pitia hz dondoo hapa chini, cha msing usidharau ndoto. Mungu ana mpango kabambe juu ya malengo ulonayo.
Hebu tuangalie mfano juu ya Biblia inasema nini kuhusu tafsiri ya ndoto zinazohusu madarasa, au kusoma, au kufanya mitihani; na ujumbe uliomo ndani yake.
Ukisoma kitabu cha Danieli 1: 3 – 20 unaweza kujifunza yafuatayo juu ya ndoto hizo:
(i) Maandalizi yanahitajika kwa ajili ya hatua iliyo mbele yako, au hatua unayotaka Mungu akupe unapoomba katika maombi yako.
(ii) Kuota “shule” au “chuo” maana yake maandalizi ya hatua fulani iliyo mbele yako yanahitaji utaratibu maalumu.
(iii) Kuota “shule” au “chuo” ulichowahi kusoma zamani, ina maana kwamba kuna jambo lililotokea hapo ulilotakiwa “kuvuka” – lakini hukuweza kuvuka, na kwa hiyo kuna eneo limekwama kwenye maisha yako.
(iv) Watu mlio nao darasani katika ndoto ina maana watu mlio ngazi moja ya kimaandalizi
(v) Kuota ndoto uko darasani na watu uliowahi kusoma nao zamani au unaota unarudia darasa, au unarudia mtihani – ina maana umekwama mahali kimaisha na unahitaji maandalizi ili kuvuka hapo.
(vi) Ukiota hukai darasani wakati wengine wako darasani; au hukai kwenye mtihani wakati wengine wanafanya mitihani – ina maana huna utulivu unaotakiwa uwe nao ili uweze kujiandaa vyema kwa hatua iliyo mbele yako
(vii) Ukiota unafanya mtihani – ujue: au unapita mahali kimaisha ambapo unapimwa kiwango chako ulichofikia kimaandalizi; au mbele yako kuna kuja kipimo kwa ajili ya kujua ikiwa umefikia kiwango kinachotakiwa kwa wewe kuingizwa hatua nyingine ya maisha
(viii) Ukiota unaota unasoma, na ukaona na somo unalosoma, au ukaota unafanya mtihani na ukaona somo la mtihani huo – ina maana unaonyeshwa aina ya, au eneo la – maandalizi unalotakiwa kulifuatilia kimaandalizi