Hizi Ndoto Zinanikera Sana

Hizi Ndoto Zinanikera Sana

Marco Polo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
13,214
Reaction score
20,988
Mm ni kijana in the late 30's nimepita pita school vya kutosha tu, kuanzia O level, Advance mpaka chuo kikuu na kote huku kulikuwa kitonga tu kutokana na juhudi zangu ktk masomo, kiukweli Nina miaka zaid ya mi5 toka nimalize chuo lakin Mara kwa Mara nimekuwa nikiota kwamba nakutana na changamoto nyingi sana hasa ninapofanya mitihani, mfano ni Jana tu nimeota niko kwenye mitihani ya Necta ya form 6, nimechelewa kuingia kwenye chumba cha mtihani kama masaa ma 2 huku mtihani ukiwa ni wa masaa 3 maana nilikuwa nimechelewa kuamka hostel,
Sasa ile kufika wasimamizi wakanigomea kuingia kwenye chumba cha mtihani, nikajaribu kuwaomba wakaniruhusu niingie huku ikiwa imebaki SAA 1 muda kuisha, nilipopewa mtihani kuna wanafunzi wakawa wamemaliza wanatoka nje, hicho kitu kilinipa stress mwisho wa mtihan msimamizi anakuja kusanya sijajibu swali hata moja ndio nikashtuka usingizini......

Huu ni mfano mmoja tu lakini nishaota nyingi za mtindo huu na zinanikera sana ukizangatia sikuwa kuwa na changamoto za aina hii kote nilipopita, labda kuna chochote zinamaanisha?
 
Maisha ni ya kawaida tu mkuu, nimeajiriwa kipato changu si chini ya 700,000/ mwezi japo changamoto zipo.
basi ndugu yangu ndoto hiyo inamaanisha ulitakiwa kuwa mbali zaidi ya hapo katika nyanja zote kimaisha, kuna mambo/jambo linakurudisha nyuma ndio maana unaota upo level za chini na unakwama.

Kama ni mtu wa imani, unatakiwa usali/dua sana na mwenyezi mungu mwingi wa rehema atakusaidia
 
Mkuu ulikua na uoga/fear kipindi unafanya mitihani...matukio mengi ya emotions huwa yanabakigi kwenye kumbukumbu kwa muda mrefu,,,,sijajua kama kuna vitu/cues kwenye mazingira yako ambayo yana trigger hayo mawazo pengine??
Sikuwa muoga mkuu maana kama mtu ulikuwa unajiandaa vyema sidhan kama utakuwa na hofu na mitihani, japo mitihani ikikaribia akili yako inakuwa inafanya kazi kwa msaada wa vichocheo( stress hormones) na ndio maana mtu anaweza soma counter zima kwa muda mchache sana,
 
Daah wewe unaota unafanya mitihani, mimi mara kwa mara naota naendesha gari tena gari kali tu, sasa sijui na mimi ndoto yangu ina maana gani? 😐
 
Mimi ndoto hizo nilikuwa naota sana mfano naenda shuleni (primary) nafika shule ile kujiangalia eti nilisahau kuvaa nguo Niko uchi , nachelewa mtihani(secondary) nazinguliwa kuingia nalialia naingia Mara najikuta Nina karatas za summary kwenye pepa msimamiz anazidaka najitetea naomba msamaha msimamiz anagoma nafutiwa matokeo, nachelewa necta form 4 najilaumu ndotoni ,nalala Massa 48 naikosa necta ya Jana yake naomba msimamizi anisaidie na Mimi nifanye mtihan wa Jana anazngua, Mara nasahau no mtihani gani naenda kufanya najua kiswahili kuingia kwenye pepa nakuta physics. aisee na wakati huo nlikuwa napasua kweli skuli ,ndoto zimeanza kufanya kaz saiz nikiwa chuo kupata tu 50 ni kaz, kusoma bila kuelewa, kukosa ham ya shule sababu ya kusoma sana alaf nafeli sana .his ndoto zina maana sana .LABDA NTAFANIKIWA KUPITIA KITU KINGINE SIO ELIMU .....NGOJA NISUBIRI
 
Sikuwa muoga mkuu maana kama mtu ulikuwa unajiandaa vyema sidhan kama utakuwa na hofu na mitihani, japo mitihani ikikaribia akili yako inakuwa inafanya kazi kwa msaada wa vichocheo( stress hormones) na ndio maana mtu anaweza soma counter zima kwa muda mchache sana,

Mkuu stress some time it means emotion,na vitu ambavyo huwaga tunavikumbuka ni vitu significant katika Maisha yetu,ndio maana unaweza ukasahau last week ulikula nini..lakini huwezi kusahau ulivyopata matokeo ya mitihani yako ulikua wapi au unafanya nini,hata kama ni miaka 20 baadae…...kama hakuna linalokukumbusha mitihani yako/cues then sijui tatizo litakua nini mkuu...
 
basi ndugu yangu ndoto hiyo inamaanisha ulitakiwa kuwa mbali zaidi ya hapo katika nyanja zote kimaisha, kuna mambo/jambo linakurudisha nyuma ndio maana unaota upo level za chini na unakwama.

Kama ni mtu wa imani, unatakiwa usali/dua sana na mwenyezi mungu mwingi wa rehema atakusaidia
Asante sana mkuu, kuna ka ukweli flani ktk maelezo yako, maana kiukweli kuna wenzangu niliosoma nao wako mbali sana kimaendeleo inafika wakat huwa sitaman kukutana nao nawakimbia kila wanaponihitaji huku nikitoa visingizio vingi vya ku cancel appointment zao
 
Mimi ndoto hizo nilikuwa naota sana mfano naenda shuleni (primary) nafika shule ile kujiangalia eti nilisahau kuvaa nguo Niko uchi , nachelewa mtihani(secondary) nazinguliwa kuingia nalialia naingia Mara najikuta Nina karatas za summary kwenye pepa msimamiz anazidaka najitetea naomba msamaha msimamiz anagoma nafutiwa matokeo, nachelewa necta form 4 najilaumu ndotoni ,nalala Massa 48 naikosa necta ya Jana yake naomba msimamizi anisaidie na Mimi nifanye mtihan wa Jana anazngua, Mara nasahau no mtihani gani naenda kufanya najua kiswahili kuingia kwenye pepa nakuta physics. aisee na wakati huo nlikuwa napasua kweli skuli ,ndoto zimeanza kufanya kaz saiz nikiwa chuo kupata tu 50 ni kaz, kusoma bila kuelewa, kukosa ham ya shule sababu ya kusoma sana alaf nafeli sana .his ndoto zina maana sana .LABDA NTAFANIKIWA KUPITIA KITU KINGINE SIO ELIMU .....NGOJA NISUBIRI
Mkuu tunafanana vitu vingi sana, ngoja tusubiri wajuzi watufumbue
 
Asante sana mkuu, kuna ka ukweli flani ktk maelezo yako, maana kiukweli kuna wenzangu niliosoma nao wako mbali sana kimaendeleo inafika wakat huwa sitaman kukutana nao nawakimbia kila wanaponihitaji huku nikitoa visingizio vingi vya ku cancel appointment zao

This is me 200% sema sasa hv hzo ndoto zimekwama, by the way mm pia niliosoma nao wapo mbali sana kimaendeleo mm naogopa hata kukutana nao mpka best friends nimewapoteza sababu ya fear wanataka kuwa karibu na mm lakin nawakwepa maisha ni ya kawaida sana sawa silali njaa ila sina maendeleo yoyote kulinganisha na wenzangu hata ambao kimasomo nilikuwa juu yao
 
Daah!! changamoto sana mkuu
 
Ndoto za type hyo zinatesa sana sana na nimeota sana mpka nikanunua kitabu cha tafsiri ya ndoto cha mwakasege nikasoma soma ila ndoto zikakoma ila maisha bado ni magumu no progress na umri umesogea sana lakin mafanikio ni kidogo sana ila madogo waliokuwa nyuma yangu wametoboa sana, wapo walioniambia nisali sana ninafanya hvyo, ila pia wapo walionishauri niangalie upande wa pili ( wazee wa nyanga) hilo nimeligomea bado naona sijafika huko ila nashukuru ndoto zimegoma ila maendeleo nayo yamesimama hela napata ila sijui inapoelekea kila nikipata hela haikai matatizo yanaibuka
 
Back
Top Bottom