Hizi ndo athari za kupanda kwa bei ya umeme

Hizi ndo athari za kupanda kwa bei ya umeme

Pyepye

Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
78
Reaction score
10
Bei za kusaga na kuboa nazo juu,wenye visima vya maji baadhi wamepandisha kutoka sh.50 kwa ndoo hadi sh.100, bei za unga nazo zinaanza kupanda kwakuwa nao hutumia umeme ktk kukoboa na kusaga. Huu ni mwanzo tu mengi yanakuja... Mbebaji wa mizigo yote hiyo ni mwananchi wa kawaida.
 
Wa akina Zitto na Mbowe njoeni sasa mtutetee kuhusu umeme,yeyote mwananchi atakayeudhuria mikutano yao yenye ajenda zao za mipasho na wakasahau kuhusu kuzungumzia jinsi ya kuandamana kupinga ongezeko la bei ya umeme wewe mwananchi utakuwa mjinga wa kutupwa.
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.
 
Usisumbuke kuviorodhesha mkuu! Kila kitu bei juu kama hakijapanda leo bei kitapanda kesho mana umeme ndo kila kitu
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Nlidhani wabunge tu,kumbe hata walamba miguu mnaafiki ndiyooooooo
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Umeme umepandishwa ili serikali ipate fedha kuunganisha wengine au kucover gharama ya shirika?
Je unakumbuka kodi ya mafuta ya taa iliyoongezwa ili wapate fedha kupeleka REA fedha zilipelekwa huko kama ilivyobajetiwa ili kuongeza watumiaji umeme vijijini?
Je hauoni gharama ya maisha itapanda kiasi cha kwamba mwananchi wa kawaida atapigana nayo ili apate kukidhi mahitaji muhimu na wala si kuunganisha umeme?
"Umeme umepanda bei"
 
ROBERT MICHAEL kwanza nashukuru kwa kuwa wewe unaongea hoja pili hatuko mbali na hawa http://www.businessdailyafrica.com/...-boost/-/539552/2137774/-/t7d9ry/-/index.html
Pia nikukumbushe kwamba mwaka jana au juzi serikali ya Nigeria ilivyotoa ruzuku kwenye mafuta wananchi wake walikuja juu, lakini ukweli unabaki pale pale lazima walaji ndio walipie huduma sio watu wote, hivyo mimi naunga mkono serikali kutopeleka ruzuku TANESCO bali waibane TANESCO Ifanye kazi kwa ufanisi na
ufanisi utasababishwa na wananchi wanaolipa fully cost!
 
Last edited by a moderator:
Nlidhani wabunge tu,kumbe hata walamba miguu mnaafiki ndiyooooooo

Wengine tunaongozwa na ku-think Big na critically; TANESCO lazima tuipe uwezo iweze kukopesheka ili tuitoe kwenye mzigo wa kubebwa na serikali... na tunaweza tu kufanya hivyo kwa kuipa momentum. Ambayo ni kulipia huduma zake ili serikali ikate kupeleka ruzuku ambayo inachezewa, then tuibane TANESCO kwa huduma ambayo ni fully paid without subsidy!!!!
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

If this is your/Goverment's point mkuu, hadi kufika takribani asilimia 80 hadi tisini (80% -90%) wananchi watakuwa wameshavuja damu sana.
 
Bei za kusaga na kuboa nazo juu,wenye visima vya maji baadhi wamepandisha kutoka sh.50 kwa ndoo hadi sh.100, bei za unga nazo zinaanza kupanda kwakuwa nao hutumia umeme ktk kukoboa na kusaga. Huu ni mwanzo tu mengi yanakuja... Mbebaji wa mizigo yote hiyo ni mwananchi wa kawaida.

Maisha bora kwa kila mtanzania kwa ARI ZAIDI NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI, utatupenda sasahivi tunaandaa moto wa 2015.
 
Na wizi wa umeme umeongezeka hii nimeona itv nabari za saa
 
Wa akina Zitto na Mbowe njoeni sasa mtutetee kuhusu umeme,yeyote mwananchi atakayeudhuria mikutano yao yenye ajenda zao za mipasho na wakasahau kuhusu kuzungumzia jinsi ya kuandamana kupinga ongezeko la bei ya umeme wewe mwananchi utakuwa mjinga wa kutupwa.

waite kaka zako akina nape na nchemba
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Bei ikishushwa wengi wataweza kununua umeme na wigo utazidi.

TANESCO watapata economies of scale.

This is counterintuitive but true.
 
Bei ikishushwa wengi wataweza kununua umeme na wigo utazidi.

TANESCO watapata economies of scale.

This is counterintuitive but true.
Umetoa hoja nzuri sana. Lakini hiyo principle itafanya kazi pala tayari umeme, nguzo, nyaya, mita na internal wiring zimefanyika kwa waTanzania wengi, Other than that it does not apply. Nawakumbusha tu kwamba TANESCO inataka ku-kopa iendeleze generation, distribution na supply ya umeme majumbani na viwandani lakini wakopaji wanasema hawezi kopesha shirika ambalo haliwezi kujenereti its own money, linategemea hisani
ya waziri wa fedha. Hivyo kupanda huku kwa tarifu kutalitoa kampuni kwenye matatizo,
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Una uwakika na unachikisema?

Hela za Rea zinafanya nini?

Kwa taarifa yako hizi ni hela kwa ajili ya kulipia Mafuta maziti, kwani mwaka jana serekali kila mwezi ilikuwa inatoaMabilioni kununua Mafuta na sasa hawana hela tena.
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Sidhani kama ni busara kulipongeza hili, Hii ni hatari sana kwa ustawi wa maisha ya Watanzania Unapopongeza ni vema ukatafakari kwa kina kwani kuna mambo yaliyopita ambayo CCM wametuaminisha kuwa yatasaidia kupeleka umeme vijijini
1. Kikwete akiwa katika ziara zake kanda ya Ziwa alitamka kuwa Marekani (USA) imeisaidia Tanzania katika Mradi mkubwa wa umeme na ni nchi pekee Africa iliyopewa fedha nyingi katika Mradi huu wa Umeme. Kwa kauli hii kulikuwa na haja ya kuongeza gharama eti kusaidia kupeleka umeme vijijini?

2. Tunaponunua umeme kuna 3% REA ambayo tunaambiwa ni kwa ajili ya kusaidia kupeleka umeme Vijijini, Kato hili maana yake nini?

3. Nakumbuka Zanzibar walikuwa wanadaiwa na TANNESCO 50,000,000,000/= lakini cha kushangaza deni hili lilisamehewa na TANNESCO na mzigo huu ndio unatuangukia sisi kufidia.

4. TANNESCO wananunua umeme kutoka SONGAS na IPTL sisi kama wananchi hatujui wanauziwa kwa shillingi ngapi na wao wanaamua kula cha juu kutuuzia sisi, lakini cha msingi tungejiuliza hii Gesi inayozalisha umeme ule kule Songas ni ya kwetu lakini cha ajabu wageni wamemiliki mitambo hiyo kwa kutumia gesi yetu wanazalisha umeme na kutuuzia huu ni ujinga.

*** Namalizia kwa kukuambia na kaa ufahamu hivyo ongezeko hili ni kwa ajili ya kupata fedha za kuwagawia CCM kwa ajili ya matumizi ya uchaguzi 2015 kwani lile dili la line za Simu lilipogonga mwamba ndio maana wamehamia huku. Hakuna cha Umeme vijijini wala nini yote hii ni wizi na unyanyasaji kwa raia.
 
Nondo, cement navyo bei juu anayeumia mwananchi wa kawaida, jamani watanzania wenzangu kwa nini tusiwaadhibu hawa viongozi 2015?
 
Back
Top Bottom